Panya amepewa jina

Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,750
2,000
PANYA AMEPEWA JINA.

1)Panya amepewa jina.
Msimwone wamsema.
Aachi pewa lawama.
Vibaya kumsakama.

2)Panya amepewa jina.
Subirini akitoka.
Jina le litapanuka.
Na wao watapasuka.

3)panya amepewa jina.
Amefungiwa tunduni.
Alijiweka mwibani.
Abandikwe mtaani

4)Panya amepewa jina.
Msidhani mwamtesa.
Kijanja amewanasa.
Msipojua kwa sasa.

5)Panya amepewa jina.
Wala yeye hakutaka.
Japo amekurupuka.
Mfupa usiolika.

6)Panya amepewa jina.
Alilowaza zamani.
Akitembea jini.
Na kukaa vijiweni.

7)Panya amepewa jina.
Kwa miguvu ya mabavu.
Na akili za wavivu.
Huwinda tembo kwa nyavu.

8)Panya amepewa jina.
Kesho mtaja mwelewa.
Mtawa mmechelewa.
Na maovu mkilewa.

9)Panya amepewa jina.
Siasa nguo chakavu.
Hupambwa na ndizi mbivu.
Kumbe ndani ni mafuvu.

10)Panya amepewa jina.
Toka Moshi na Arusha.
Juzi amewaangusha.
Leo awa washa washa.

Shairi=PANYA AMEPEWA JINA.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
13,809
2,000
Hupambwa na ndizi mbivu
:D no escape ikiwa imeiva au haijaiva inasadiki rangi ileee
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom