Panone hali ni mbaya.....

Panone hali ni mbaya.....

M4C ARUSHA

Member
Joined
Apr 27, 2012
Posts
38
Reaction score
4
HATIMAYE wafanyakazi wa kampuni ya kusafirisha na kuuza mafuta ya jumla na reja reja Panone and company limited wamejikuta wakiumaliza vibaya mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka mpya 2013 wakiwa katika hali mbaya ya kiuchumi huku mmiliki wa kampuni hiyo akijenga maghorofa mithili ya uyoga jicho la m4c linakutiririshia habari kamili.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vyenye kuaminika vimeeleza kuwa ndani ya uongozi wa kampuni hiyo yaani panone and company limited kumekuwa na madaraja ya watumishi ambao ni wakenya na wazawa yaani watanzania huku malipo ya mishahara ikiwa ni tofauti tofauti huku mishahara ikizidi kushuka kila kukicha hususani kwa wazawa.

Wafanyakazi kutoka vituo vya Tunduma mkoani mbeya dar es salaam ARUSHA manyara kiteto na Kilimanjaro wamekumbwa na dhahma hiyo ya kushushwa kiwango cha mishahara huku ya wageni ikibaki pale pale kwa kigezo kuwa kampuni haina hela.
Vyanzo hivyo vya habari vinafafanua kuwa mmiliki wa kampuni hiyo (jina tunalo)amekuwa jeuri sana hataki kusikiliza wafanyakazi kila wanapotaka kukutana nae na amekuwa akiwataka waache kazi na badala yake aajiri wafanyakazi kutoka nje kwani wazawa wao ni maneno maneno.
Chakusikitisha zaidi ni kuwa pale wafanyakazi walipoenda ofisi ya utumishi kitengo cha idara ya kazi katika mikoa tofauti tofauti lakini inasemekana mmiliki wa panone tayari alishapita huko na kumalizana na wakubwa hivyo ni sawa na kazi bure

Katika kudhihirisha hilo baadhi ya wafanyakazi wamekuwa wakilipwa bila kufuatwa kwa taratibu za ulipwaji wa fedha ikiwa ni pamoja na kuzipitisha benki ili mapato ya nchi yapatikane ambapo taarifa za ndani meneja mkuu Genestio Sombemshahara wake ni zaidi ya milioni tano mkaguzi wa ndani bwana J KIRAI mshahara wake ni milioni nne na laki nane.

Watumishi wa kitanzania ambao wamefanya kazi zaidi ya miaka mitano wamekuwa wakilipwa kima cha chini cha shilingi 80000 hadi 120000 kitendo ambacho ni kinyume na sheria ya shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini tucta.
Kwa mujibu wa meneja mkuu baada ya m4c kumdodosa amekiri na kuomba habari hizi zisifike sehemu yoyote kwani anamwonea huruma bosi wake kutokana na biashara anayoifanya anakwepa ushuru mkubwa sana wa serikali kwa kisingizio kuwa kampuni ni ya wakubwa huku akijidai anasambza mafuta nchini kumbe yanapelekwa nje ya nchi kama Rwanda,Kenya na drc hali kadhalika Zambia

“najua mna nia kweli ya kuwatetea watazania wenzenu ila oneni hayo maghorofa yanavyoota mtafuteni mmalizane nchi yenu si ya kitu kidogo?’alisema bwana Sombe Meneja mkuu
Kwa mujibu wa taarifa za ndani zaidi zinaonyesha kwamba ana mkopo katika benki mbali mbali lakini utajiri wake una mashaka kwani mikopo hiyo haiendani na uatajiri alio nao wakutisha hapa naomba vyombo husika viingilie kati yaani usalama wa taifa takukuru na tra .
 
kweli: kwa muda mfupi niliokaa katika mazingirafulanifulani katika utendaji kazi wangu Kampuni ya Panone haifai, siyo siri mmiliki hana ushirikiano mzuri na mamlaka zilizo wekwa, ukiachilia mbali maneno yanayosemwa kwamba Ofisi za serikali zote ameishaziweka kiganjani.anyway kwa vile limeanzishwa ngoja tuendelee kulijadiri.
 
tra je imekuwa ikilipwa kodi?je idara ya kazi kwanini haitaki wala kujishughulisha na migogoro y awafanyakzi hawa kuna vyama vya wafanyakazi kama ilivyo kwa taasisi mbali mbali?takukuru mpo wapi?ila kama takukuru na polisi wanapewa mafuta na huyu bwana uchunguzi utafanyikaje hapa sasa na kama idara ya uhamiaji haiko makini mtu anatoka kenya anadai kuwa ni mlinzi akija hapa ni meneja au mhasibu huoni kuna siri kubwa hapa
 
HATIMAYE wafanyakazi wa kampuni ya kusafirisha na kuuza mafuta ya jumla na reja reja Panone and company limited wamejikuta wakiumaliza vibaya mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka mpya 2013 wakiwa katika hali mbaya ya kiuchumi huku mmiliki wa kampuni hiyo akijenga maghorofa mithili ya uyoga jicho la m4c linakutiririshia habari kamili.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vyenye kuaminika vimeeleza kuwa ndani ya uongozi wa kampuni hiyo yaani panone and company limited kumekuwa na madaraja ya watumishi ambao ni wakenya na wazawa yaani watanzania huku malipo ya mishahara ikiwa ni tofauti tofauti huku mishahara ikizidi kushuka kila kukicha hususani kwa wazawa.

Wafanyakazi kutoka vituo vya Tunduma mkoani mbeya dar es salaam ARUSHA manyara kiteto na Kilimanjaro wamekumbwa na dhahma hiyo ya kushushwa kiwango cha mishahara huku ya wageni ikibaki pale pale kwa kigezo kuwa kampuni haina hela.
Vyanzo hivyo vya habari vinafafanua kuwa mmiliki wa kampuni hiyo (jina tunalo)amekuwa jeuri sana hataki kusikiliza wafanyakazi kila wanapotaka kukutana nae na amekuwa akiwataka waache kazi na badala yake aajiri wafanyakazi kutoka nje kwani wazawa wao ni maneno maneno.
Chakusikitisha zaidi ni kuwa pale wafanyakazi walipoenda ofisi ya utumishi kitengo cha idara ya kazi katika mikoa tofauti tofauti lakini inasemekana mmiliki wa panone tayari alishapita huko na kumalizana na wakubwa hivyo ni sawa na kazi bure

Katika kudhihirisha hilo baadhi ya wafanyakazi wamekuwa wakilipwa bila kufuatwa kwa taratibu za ulipwaji wa fedha ikiwa ni pamoja na kuzipitisha benki ili mapato ya nchi yapatikane ambapo taarifa za ndani meneja mkuu Genestio Sombemshahara wake ni zaidi ya milioni tano mkaguzi wa ndani bwana J KIRAI mshahara wake ni milioni nne na laki nane.

Watumishi wa kitanzania ambao wamefanya kazi zaidi ya miaka mitano wamekuwa wakilipwa kima cha chini cha shilingi 80000 hadi 120000 kitendo ambacho ni kinyume na sheria ya shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini tucta.
Kwa mujibu wa meneja mkuu baada ya m4c kumdodosa amekiri na kuomba habari hizi zisifike sehemu yoyote kwani anamwonea huruma bosi wake kutokana na biashara anayoifanya anakwepa ushuru mkubwa sana wa serikali kwa kisingizio kuwa kampuni ni ya wakubwa huku akijidai anasambza mafuta nchini kumbe yanapelekwa nje ya nchi kama Rwanda,Kenya na drc hali kadhalika Zambia

“najua mna nia kweli ya kuwatetea watazania wenzenu ila oneni hayo maghorofa yanavyoota mtafuteni mmalizane nchi yenu si ya kitu kidogo?’alisema bwana Sombe Meneja mkuu
Kwa mujibu wa taarifa za ndani zaidi zinaonyesha kwamba ana mkopo katika benki mbali mbali lakini utajiri wake una mashaka kwani mikopo hiyo haiendani na uatajiri alio nao wakutisha hapa naomba vyombo husika viingilie kati yaani usalama wa taifa takukuru na tra .

Wacha maneno ya kuchonga wewe! uliomba kazi ya shilingi ngapi. Kama unaona mshahara ni kidogo si uondoke ? Kama wakenya wanalipwa vizuri, basi nawe sema ni Mkenya ili ulipwe zaidi. Maneno ya watanzania meengi. Mpe kazi afanye ,,, ,,,, ,,,, Ooh nimefiwa na jirani, naenda ubarikio, nampeleka mama kutibiwa .. ... .. Tija kidogo, maneno mingi! Siamini unachikisama .. Fanyeni kazi bana.
 
Panone kuna mkono mkubwa wa rizi1 kikwete, ndio chanzo kikubwa cha jeuri hiyo
 
Huyo mwandishi wa hii mada ana wivu wa kike mzee patrick ndio mmiliki wa hyo kampuni ni mzee mcha mungu hivi y mwandishi unaandika bila kupima ama kwa sababu mzEe pAnone ni mtu wa kaskazini mzawa wa moshi ndio unamuonea gere nishawahi kufanya nae kazi za kiuhasibu hayuko kama unavomchafua
 
Panone kuna mkono mkubwa wa rizi1 kikwete, ndio chanzo kikubwa cha jeuri hiyo

sidhani kama ni kweli kuna mkono wa riz1,ungesema kidogo EL kungekua na ukweli fulani... kuhusu vyombo vya usalama kuchunguza hizo tuhuma pengine baada ya kuondolewa utawala wa CCM...
 
M4C, kuna sehemu moja umenichanganya kidogo,umesema jamaa anasambaza mafuta kupeleka nchi jirani badala ya kusambaza nchini,sijui kama unafahamu kuwa mafuta ya hapa nchini yanakua yamelipiwa kodi, tofauti na yale yanayopelekwa nchi jirani huwa hayalipiwi ushuru wa aina yeyote.SIJUI KAMA ULIKUA UNAMAANISHA KUWA ANASAMBAZA NCHINI MAFUTA YA KWENDA NCHI JIRANI, AMBAYO KIUTARATIBU NDIYO HAYANA USHURU WA FORODHA, kwa hivyo basi ndio KAMA ANGEYAUZA HAPA NCHINI, ndio angekua anakwepa ushuru.jaribu kufuatilia hilo kimakini.,Ki uhalisia mafuta ya hapa nchini ni aghali kuliko yaendayo nchi jirani
 
Back
Top Bottom