Pande Game Reserve hifadhi Pekee jijini Dar es Salaam

Pande Game Reserve hifadhi Pekee jijini Dar es Salaam

bomouwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Posts
1,149
Reaction score
800
Habari!
Je wajua kua katika jiji la Dar es Salaam kuna Hifadhi ya Pori la Akiba Pande?Ni mojawapo ya Pori linalosimamiwa na MAMLAKA YA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI TANZANIA (TAWA).Ni kilometa 45 tu kutokea mjini Askari monument kuelekea Bagamoyo na unapokaribia kufika Kituo cha Bunju B mkono wa kushoto kuna Bango kubwa linaloonyesha njia ya MabwePande ambapo ni km8 mpaka hifadhini.

Ni hifadhi yenye wanyama wadogo kama bushbuck,duikers,dikdiks,nyoka kama cobra,black&green (mambas),pythons achilia mbali mijusi,vipepeo na miti ya Tao la Pwani.

Pori la Akiba Pande kuna vivutio kama:
1.Mimea ya aina tatu ambayo inapatikana Pande pekee dunia nzima
2.Mbega weupe na weusi yaani Black and White Colobus Monkeys.
3.Bonde (Crater) iliyojaa uoto wa asili ndani yake

Shughuli za kitalii zinazofanyika ni pamoja na
1.Camping
2.Nature Walk Safaris
3.Bird watching
4.Photography and Videography
5.Cycling

Katika jitihada za kutangaza Pori la akiba Pande kwa kushirikiana na Dar Running Club, mnamo tarehe 13 mwezi wa Disemba kutakua na michezo ya kukimniza baiskeli pamoja na kukimbia ndani ya hifadhi ikiwa ni kuhamasisha Utalii wa ndani ambao ni ECO-FRIENDLY kwa wakazi wa Dar na hata walio nje pia.

Unaweza fanya registration kwa kuingia dartrail.fasthub.co.tz kwa kujiwekea nafasi ya kushiriki.

Nyote Mnakaribishwa


IMG-20200916-WA0013.jpg
 
Achana na complication za kuregistar,wewe weka namba ya whatsapp kurahisisha mawasiliano
Hii ipo kwenye mfumo chief hakuna malipo ya kwenye simu personal.Ndio maana hiyo website imetengenezwa.
 
Gharama za kushiriki ni sh ngapi?
Ingia hapo dartrail.fasthub.co.tz kuna details zote.Lakini kwa kukujibu tu gharama ni 49,500TZS na hii inajumlisha
1.Entry fee
2.Medali
3.Beeps
4.Vinywaji (kwa wanaokimbia na waendeshaji baskeli katika vituo)
 
Niamini mimi, au wewe unajua kila kitu!
Kuna nilipoandika najua kila kitu?Wanasayansi hatuamini kirahisi.Nipe link nami nielimike.I studied Wildlife Science na sijawahi sikia.Sasa kma ndugu unajua basi unanijuza.Au sio chief?
 
Kuna nilipoandika najua kila kitu?Wanasayansi hatuamini kirahisi.Nipe link nami nielimike.I studied Wildlife Science na sijawahi sikia.Sasa kma ndugu unajua basi unanijuza.Au sio chief?

Tukutane disemba 13, Pande Game Reserve... count me in.

Registered!
 
Back
Top Bottom