Panda mti mmoja tu

Panda mti mmoja tu

Women time

Member
Joined
May 17, 2019
Posts
35
Reaction score
32
Fanya Tafakuri athari watakazozipata wajukuu na kizazi chako utakachokiacha hapa duniani kutokana na miti inayozidi kupotea kila kukicha.

Tumia mvua hizi alizozileta mwenyezi Mungu kwa makusudi ili kutafta mvua ya kesho.

Bila ya kusimamiwa unaombwa kuchukua hatua ili usiache deni hapa duniani kuwa haukutengeneza mazingira. Dunia ni mimi na wewe.

Rafiki Mlioko humu kuwa mabalozi wa hili jambo.

Mr. Damas ametukumbusha ingawaje yeye kapanda Mkrismas, wewe unapanda mti gani?
IMG_20191207_094448_173.jpeg
 
Fanya tafakuri athari watakazozipata wajukuu na kizazi chako utakachokiacha hapa duniani kutokana na miti inayozidi kupotea kila kukicha.

Tumia mvua hizi alizozileta Mwenyezi Mungu kwa makusudi ili kutafuta mvua ya kesho.

Bila ya kusimamiwa unaombwa kuchukua hatua ili usiache deni hapa duniani kuwa haukutengeneza mazingira. Dunia ni mimi na wewe.

Rafiki mlioko humu kuwa mabalozi wa hili jambo, Mr. Damas ametukumbusha ingawaje yeye kapanda mkrismas wewe unapanda mti gani?

IMG_20191207_094448_173.jpeg
 
Ethiopia ndio wanashikilia record ya upandaji wa miti mingi duniani.

Walipanda miti milioni 350 kwa siku moja
Ndiyo, 350m kwa siku.
 
Asante bwana mazingira kwa kutuhamasisha tupande miti
 
Shukrani kwa kutuhamasisha Bwana mazingira,umenifanya nitafakari mengi.wakati nasoma shule ya primary kipindi hicho ilikuwa ndio inaanzishwa 2003 .Kulikuwa Hakuna mti hata mmoja eneo la shule.wazazi na walimu wakakubaliana wachangie shilingi 20 kwa Kila mwanafunzi ili inununliwe miti na ipandwe Kila mwanafunzi alipewa kazi ya kuimwagilia Sasa ni 2019.miti hiyo ikiiona Leo hii imekuwa mikubwa Sana.Imesaidia kuleta kivuli,kupendezesha mazingira na hewa Safi.Pia wanafunzi wa Sasa wanafahidi juhudi za waliotangulia.
*Miti ina faida nyingi Sana hutupatia mbao,hutupatia kivuli,husaidia kuleta mvua,hutupatia matunda,kuzalisha hewa,pia hupunguza ongezeko la joto duniani linalozalishwa na shughuri za viwandani.Pia huzuia tabaka la ozone lisiyeyuke.Kuongezeka kwa joto husababisha maji ya bahari yaongezeke,hii inatokana na bara la Antaktika ambalo ni barafu huanza kuyeyuka kidogokidogo.Bara la Antaktika Hakuna kiumbe chochote kinachoishi ni barafu tu.misitu Kama Amazon ulioko nchini Brazil bara la South America na msitu wa Congo ulioko bara la Africa miti yake huzalisha kiwango kikubwa Cha hewa ya oksijeni duniani.Matumizi ya miti hayakwepeki ukikata mti usisahau kupanda mwengine hii itasaidia kunusuru nchi kukumbwa na desert.

#Kuwa mzalendo ipende nchi yako.Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika
 
Aisee Barikiwa sana kwa elimu uliyotoa. Nahisi wenye uzalendo wa kweli watafanyia kazi

Kwa sababu walijitoa kutokomeza majanga yanayoikabiri dunia kutokana na ukosefu wa miti.

Mnaonaje na sisi watanzania tulikofanyia kazi kwa kuguswa

Penye nia pana njia na hata sisi tukiamua tunaweza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom