maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Katika hotuba yake kama mwenyeji katika sherehe za ufunguzi wa daraja la Kigamboni, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amejidhihirisha kama mmoja wa vijana wachapa kazi wasiotafuna tafuna maneno.
Kwa kumwambia hadharani mheshimiwa Rais jinsi wezi wanavyokula pesa za makusanyo ya ushuru wa mabasi katika stendi ya Ubungo na parking katika jiji ni kitendo cha ushujaa na uzalendo mkubwa na hii imethibitisha uozo anaouzungumza kila siku mheshimiwa Rais kwamba umetapakaa kila pahala.
Nina hakika Makonda atawanyoosha wapiga dili katika jiji la Dsm, watafanya na kutumia kwa nidhamu kodi wanazolipa wanajiji wa Dsm.