MTV MBONGO
JF-Expert Member
- Feb 18, 2016
- 1,261
- 1,222
Mahakama ya uhalifu wa kimataifa iliyopo The Hague, Uholanzi imepata pingamizi kubwa kutoka viongozi wa mataifa mbalimbali duniani hasa Africa. AU imekuwa ikiipinga kwa kigezo kuwa inaonea Africa zaidi. nionavyo mimi bila mahakama hii nchi nyingi hasa za Africa zingekuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na machafuko ya kutisha. Hii inatokana na kwamba viongozi wengi wa mataifa mbalimbali hasa Afrika wanaogopa kutenda uhalifu kwa kuhofia watapelekwa huko. Mahakama hii imefanikiwa kuwatia hatiani viongozi mbalimbali wakiwemo majirani wenzetu na wapinzani wa chinichini kiuchumi KENYA. japo wameshinda ktk kesi hiyo lakini wamepata fundisho na viongozi wengi wameiogopa mahakama. napingana na viongozi wa Kiafrica kuikana mahakama hii kwani ina mchango mkubwa kwa nchi zetu zinazoendeshwa bila kufuata sheria hasa za Kiafrika. kumbuka wote waliohusika na uhalifu,mahakama imewatia hatiani. Big up mama Fetouh Bensouda, mwendesha mashtaka mkuu na jopo lako!