mwembemdogo
JF-Expert Member
- Feb 28, 2016
- 2,282
- 1,252
Nimeshangazwa na wabunge wa CCM kuipinga serikali yao inayotaka wakatwe kodi kwenye kiinua mgongo chao pindi wamalizapo ubunge wao.Naamini ubunge sio utumishi kama utumishi mwingine na kila mapato ni lazima yakatwe kodi iweje wao wasikatwe kodi?
CCM inajinadi kuwa ina uchungu na walalahoi sasa iweje wabunge wake hawana uzalendo wa kuchangia mapato yao kwa kukatwa kodi ili kodi hizo ziboreshe hospitali,barabara,shule na huduma nyingine?Mbona walipiga makofi na vigeregere wapinzani kukatwa posho? Nilitegemea wabunge wa CCM wangerukaruka kwa nderemo na vifijo kusikia sheria hiyo.
HAPA KAZI TU