"Vita vya kesho yako; Hag 2:9"
Mungu akitaka kukufanikisha anakuletea wazo kama mbegu/wazo la kukufanikisha.
-Wazo lolote la kukufanikisha Lina vita vyake,
-Adui akitaka kupambana na kesho yako atapambana na wazo lolote la kukufanikisha.
-Njia moja wapo ya Adui kupambana na wewe ni kupambana na wazo alilokuletea Mungu la kukufanikisha hivyo Adui anafanya yafuatayo;
Anazuia usisikie hata Mungu akikusemesha.
Anazuia usielewe
Anazuia usitii
Anaondoa utayari wa kulifuatilia na kulitendea kazi lile wazo.
Unapoona uzito wa kutekeleza jambo fulani ujue hilo jambo limebeba kesho yako.