Pambana bila hofu. Bila soni

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,548
Reaction score
860,682
Usione aibu kwa HUSTLE zako. kuuza nguo, kuuza chakula, kuuza vipodozi, kuuza kuku, kuuza chaja za simu, kufanya kilimo, kufanya muziki, kuwa mchekeshaji nk.

Usione aibu jinsi unavyotengeneza pesa, Ni njia ya kujikimu. Usiruhusu kazi/hustle zako zikunyime furaha yako. Unafanya kazi ili uishi huishi ili ufanye kazi. Usione aibu, watu hawatakulipia bili zako au kukulisha au kukununulia nguo.. ukiwaendekeza hustle zako zitakushinda.

Kumbuka: Una bili za kulipa na familia ya kulisha sio jamii ya kufurahisha.

Changamkia dili hizo maana The end justifues the means.. Mwisho wa siku utaangaliwa una nini kibindoni..!
 
Nakuunga mkono hoja yako
 
Usione aibu kwenye pesa hata siku moja, heshimu pesa usiitupe hovyo maana pesa hupenda kukaa mahali penye akili. Fursa sometimes hutengenezwa, lazima uwe umejiandaa Ili kuitumia fursa vizuri hivyo lazima uwe na subra kwenye mambo yako mengi ya kimafanikio.

Kitu wengi wasichokijua, mafanikio siyo bahati, lazima uwe na determination Ili kuyafikia na kuyavutia, kwenye huu ulimwengu wa material things hakuna bahati bali ni vile mtu hajui kuwa ameyavutia mafanikio Kwa namna Fulani, kumbuka Iko pumzi ya kimungu ndani yetu hivyo unavyofikiri na kutenda ndivyo hivyo hivyo utakavyokuwa.
 
 
Huyu chui anawakilisha ubaya wa njaa.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…