Skendo ya ngono inaitikisa Kanisa la Katoliki, Parokia ya Mburahati
lililopo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam na kusababisha
mgawanyiko mkubwa kwa waumini.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu zimebaini kuwa skendo hiyo ya
ngono inamhusisha Padri Paul Njoka na mhudumu wa nyumba za mapadri
ambaye pia ni muumini wa kanisa hilo aliyejulikana kwa jina moja la
Mwasiti.
Taarifa zilizopatikana kanisani hapo zinadai kwamba padri huyo
alimjaza mimba mhudumu huyo na hivi sasa amezaa naye mtoto.Habari hizo
zilienea kanisani hapo na kusababisha baadhi ya waumini kutaka suala
hilo liwekwe wazi ili kiongozi huyo achukuliwe hatua zaidi, jambo
lililomfanya kasisi huyo atafute jinsi ya kujihami.
Chanzo chetu cha habari kinasema kwamba baadhi ya viongozi wa kanisa
hilo walifikia hatua ya kutafuta jinsi ya kumficha mtoto huyo baada ya
kuzaliwa ili kupoteza ushahidi. Imeelezwa kwamba Februali 4, mwaka huu
Padri Njoka akiwa na muumini aliyejulikana kwa jina la Maria Kaswela
walichukua gari na kumsaka Mwasiti, walimpata na kumuingiza katika
gari hilo.
Imedaiwa kwamba katika mzunguko wao, Mwasiti hakujua ni kitu gani
alichotakiwa kufanyiwa na mtoto wake bali yeye alijua ni matembezi ya
kawaida huku akifurahia ni jinsi gani padri anavyompenda mtoto wake na
kuamua kuzunguka naye jijini kwa siku hiyo. Chanzo kilidai kwamba siku
hiyo padri huyo na mzazi mwenzake walielekea Sinza,Manzese kisha
Magomeni.
MTOTO ATEKWA
Walipofika Magomeni habari zinasema walimtuma dukani mama wa mtoto
(Mwasiti) na mtoto akawa amebebwa na Maria. Chanzo kiliendelea kudai
kwamba padri aliendesha gari na kuondoka eneo la Magomeni kwa kasi
kuelekea kusikojulikana na Mwasiti alipotoka dukani na kwenda sehemu
lilipoegeshwa gari hakuwaona na alipowapigia simu hawakupatikana.
TAARIFA YAFIKA POLISI
Hata hivyo, Mwasiti alipatwa na hofu kwani ilimchukua muda mrefu bila
kuwaona, kitendo kichomfanya aende Kituo cha Polisi, Wilaya ya
Kipolisi ya Magomeni kutoa taarifa ya kutekwa kwa mtoto wake wa siku
28 tangu azaliwe.
Mwasiti alifunguliwa jalada lenye kumbukumbu MG/RB/2430/2012 ndipo
polisi walipoanza kazi ya kuwatafuta padri na Maria bila mafanikio.
Habari zinasema polisi walifanikiwa kumuona Padri Njoka akiwa kanisani
siku ya Jumapili akiendesha ibada ila ilishindikana kumkamata kwa
sababu misa ilikuwa ikiendelea. Kutokanana kitendo cha padri huyo
kuendesha misa, askari hao waliacha taarifa kwa mlinzi wa kanisa hilo
kwamba baada ya kumaliza ibada afike Kituo cha Polisi Magomeni akiwa
na Maria.
Hata hivyo, hawakwenda siku hiyo badala yake walienda kesho yake
Jumatatu ya Februali 6, mwaka huu.“Mara walipofika kituoni waliwekwa
chini ya ulinzi, walibanwa ili waonyeshe alipo mtoto ambapo walisema
kwamba yupo Kigamboni kwa ndugu wa padri huyo,” chanzo hicho kilisema.
Polisi waliwaamuru watoe namba ya simu ya watu walio na mtoto huyo ili
wapigiwe, padri alitoa, ilipopigwa aliye na mtoto akaamriwa amlete
kituoni hapo na akafanya hivyo saa 5.00 usiku padri akiwa chini ya
ulinzi. Hata hivyo, polisi walipomkabidhi Mwasiti mtoto wake alikataa
kumpokea na kudai kwamba akapimwe afya yake kwanza kwa vile hakujua
alichofanyiwa huko na alikua katika mazingira gani.
Chanzo kiliendelea kusema kwamba hapo polisi Magomeni alikuwepo pia
Paroko Timoth Nyasulu Maganga ambaye ni mkubwa wake wa kazi Padri
Njoka.
Habari zinasema Padri Maganga alimbembeleza Mwasiti amchukue mtoto
wake ambaye alikubali kisha alikwenda naye Kinondoni kwa dada wa mzazi
huyo. Uchunguzi wetu umebaini kuwa kesi hiyo ipo chini ya mpelelezi
mwenye namba WP697 Tiba.
WARAKA KWA PENGO
Kutokana na kitendo hicho, baadhi ya waumini wa kanisa hilo waliamua
kumuandikia barua Februali 8, mwaka huu Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es
Salaam Muadhama Askofu Polycarp Kadinali Pengo kuhusu udhalilishaji wa
Kanisa Katoliki waliodai kufanywa na padri huyo kwa kumteka mtoto.
Katika barua hiyo (Nakala tunayo) waumini hao wameeleza jinsi wachunga
kondoo walivyofikia hatua ya kufanya mapenzi na wafanyakazi, wahudumu
wa nyumba ya mapadri na kuwapa mimba. Hata hivyo, katika barua hiyo
waumini hao wamesikitishwa na kitendo hicho na kudai kuwa gharama
kubwa za fedha za kanisa zimetumika kushughulikia suala
hilo.''Tunakuomba ufanyie kazi jambo hili kwa haraka inawezekanavyo
ili kuepusha uvunjifu wa amani endapo viongozi hao wachafu watabaki
hapo parokiani,” ilisema sehemu ya barua hiyo.
Barua hiyo imeendelea kueleza kuwa mapenzi yanayofanyika kanisani hapo
kati ya viongozi na waumini yamesababisha utoaji hovyo wa mimba hadi
wengine kuzalishwa, kitendo ambacho kinalitia aibu Kanisa
Katoliki.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles
Kenyela hakupatikana kuzungumzia tukio hilo lakini afisa mmoja wa cheo
cha juu wa jeshi hilo alithibitisha kuwepo kwa madai hayo kuongeza
kuwa upelelezi bado unaendelea.
Aidha, Kadinali Pengo hakuweza kupatikana kuzungumzia malalamiko hayo
ya waumini wake.Gazeti hili linaendelea kufuatilia sakata hilo kwa
undani zaidi ili kujua ni hatua gani zitachukuliwa dhidi ya
mtuhumiwa.skendo ya ngono yatikisa kanisa katoliki.