Pale mgombea urais anapotoka kijijini/wilayani/mkoani kwako

BOD

JF-Expert Member
Oct 13, 2016
222
164
Wakati wa kura za maoni(CCM) huku mkoa wa Mara ulizuka uvumi kuwa anko Makongoro, atapeperusha bendera ya CCM,hali ya hewa ilibadilika sana hata kwa waliokua wakisupport upinzani wakasema kama atapitishwa watamuunga mkono.

Nikaongea na rafiki yangu mmoja aliyekuwa Arusha( wakati wa kura za maoni CCM) akaniambia kama CCM itampitisha EL, Arusha na sehemu nyingine Kaskazini, CHADEMA watampigia kura, na kura za ubunge ndio zingeenda upinzani.

Kanda ya Ziwa( Shy, Mwz, Geita n.k) kulikuwa na mwamko mkubwa sana wa mageuzi kuelekea upinzani lakini baada ya kusikia mgombea urais kupitia CCM anatoka Kanda ya Ziwa watu walichanganyikiwa kwa furaha na kampeni zikaanza kupigwa kwa kisukuma. Jamaa 1 akasikika akisema kupata rais kutoka wilayani/kijijini kwako ni baraka mkubwa.

Kupitia hilo nikajifunza kitu kuhusu vita ya undugu TZ namna inavofanya kazi kwenye kura za urais,though jukwaani wanasiasa wanapinga jambo hili lkn mioyoni mwa wa TZ jambo hili bado ni kubwa.
 
Umenikumbusha mbali mkuu.
Ukweli nilishindwa kabisa kumuangusha jamaa japo tayali nilikuwa nsha kata tamaa na hiki chama chao.
 
Back
Top Bottom