kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 11,190
- 24,620
Pakistan yaiambia UAE: Katu hatutaitambua Israel
Dec 22, 2020 07:23 UTC
Kwa mara nyingine tena, serikali ya Pakistan imesisitiza kuwa, kamwe haitoutambua utawala wa Kizayuni wa Israel licha ya mashinikizo ya nchi ajinabi.
Akiongea na waandishi wa habari jana Jumatatu katika mji wa Multan, Shah Mahmood Qureshi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan ameuhutubu Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kuuambia: Tumeweka wazi na tumeiambia bayana Imarati kuwa, kamwe Islamabad haitoitambua Israel hadi pale mgogoro wa Palestina utakapopatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Amesema Pakistan haitakubali mashinikizo ya nchi yoyote ya kuitaka iutambue utawala ghasibu wa Israel unaokanyaga haki za wananchi wa Palestina kila leo.
Waziri wa Mashauri wa Kigeni wa Pakistan ameeleza bayana kuwa, msimamo wa taifa la Pakistan la kuwaunga mkono Wapalestina uko wazi na madhubuti.
Hivi karibuni pia, Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan alikanusha kuwepo mashinikizo ya aina yoyote ya kuitaka nchi hiyo ijiunge na safu ya nchi zinazofanya mapatano na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Alisema wananchi wa Pakistan wako bega kwa bega na wananchi wa Palestina na wanawaunga mkono kikamilifu katika kuhakikisha wanarejeshewa haki zao.
Tags
Soma zaidi[emoji1313]
Kutangaza msimamo wa wazi Pakistan wa kupinga kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni
Dec 23, 2020 13:01 UTC
Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan amepinga aina yoyote ya mashinikizo ya nje dhidi ya nchi hiyo kwa ajili ya kujiunga na safau ya nchi zinazoanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni na kueleza kuwa: Islamabad katu haitaitambua rasmi Israel.
Akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari katika mji wa Multan, Shah Mahmoud Qureishi Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan kwa mara nyingine tena amepinga mashinikizo ya nchi ajinabi kwa nchi hiyo ili ijiunge na safu ya nchi zilizoanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni na kuongeza kuwa: sisi tumewaeleza Imarati kwamba Pakistan inataka kupatiwa ufumbuzi wa kudumu kadhia ya Palestina na katu haitaitambua rasmi Israel.
Shah Mahmoud Qureish akiwa na Waziri mwenzake wa Imarati, Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan huko Abu Dhabi
Qureishi aidha amebainisha kuwa: Pakistan haiafiki kushinikizwa kivyovyote katika mjadala wa kukubali mpango huo wa mapatano; na ina misimamo thabiti na ya wazi katika kuwaunga mkono wananchi wa Palestina na Kashmir.
Matamshi ya wazi ya bila kupepesa macho ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan katika kupinga kufikiwa mpango wowote wa mapatano kati ya nchi hiyo na utawala wa Kizayuni na kusisitiza kwake kutoutambua rasmi utawala huo haramu yametolewa baada ya ziara ya karibuni aliyofanya Qureishi huko Imarati ambapo baadhi ya vyombo vya habari vilieneza uvumi vikiihusisha ziara hiyo na kitendo cha kudhalilisha cha nchi hiyo ya Kiarabu cha kuanzisha uhusiano wa kisiasa na kiuchumi na Israel.
Baada ya Marekani kuzishinikiza baadhi ya nchi za Kiarabu zianzishe uhusiano na utawala ghasibu wa Kizayuni; kulienezwa tetesi kwamba White House inafanya jitihada kwa ajili ya kupanua satwa yake ya kisiasa na hivyo imeliweka katika ajenda ya kulifanyia kazi suala la kuanzishwa uhusiano kati ya nchi mbalimbali na utawala huo na ndio maana inaishinikiza Pakistan pia kuchukua hatua ili kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel.
Matamshi ya wazi ya Shah Mahmoud Qureishi katika mazungumzo na waandishi wa habari katika mji wa Multan yameweka wazi siasa thabiti za Pakistan katika kuunga mkono na kutetea malengo ya wananchi wa Palestina na kupinga kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni; na kwa msingi huo matamshi ya Qureishi yamehitimisha uvumi wote uliokuwa umeenezwa na vyombo vya habari vya kieneo kuhusu ajenda kuu ya mazungumzo yake na viongozi wa Imarati haswa kuhusu suala la kufikia mapatano na Israel.
Kabla Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan kutangaza msimamo rasmi na wa wazi wa nchi yake wa kwamba yeye ameisisitizia Imarati kuwa Islamabad katu haitautambua rasmi utawala wa Kizayuni, kulienezwa uvumi juu ya uwezekano wa Pakistan kubadili msimamo wake kuhusu kutetea na kuunga mkono kwa pande zote malengo ya Palestina. Hasa ikizingatiwa kuwa baada ya kufichuliwa uvumi huo na vyombo vya habari, kuliripotiwa habari ya kuibuka wasiwasi pia miongoni mwa wananchi wa Pakistan kuhusu suala la nchi yao kufikia mapatano na Israel.
Licha ya serikali ya Donald Trump kutumia nyenzo zote; serikali ambayo siku zake za mwisho za kuwepo huko White House zinakaribia kumalizika; suala la kuanzisha uhusiano wa kawaida kati ya nchi za eneo la Mashariki ya Kati na utawala wa Kizayuni limekuwa gumu kwa Marekani kwa sababu siasa za vitisho na hongo za serikali ya nchi hiyo dhidi ya nchi mbalimbali kwa ajili ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel zimeshindwa kuzaa matunda inayoyataka Washington na Tel Aviv.
Pamoja na Marekani kustafidi na mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa na rushwa; lakini ni Imarati, Bahrain na Morocco pekee ambazo zimenasa kwenye mtego huo wa kuanzisha uhusiano na utawala wa KIzayuni; na katika mazingira kama hayo viongozi wa nchi tatu hizo wanakabiliwa na upinzani wa ndani ya nchi zao kwa sababu ya suala hilo.
[https://media]Jitihada za Trump za kuzishawishi nchi za Kiarabu kuanzisha uhusiano wa utawala wa Kizayuni
Kufuatia ziara hiyo tajwa ya Mahmoud Shah Qureish huko Abu Dhabi; vyombo vya habari vyenye mfungamano na Marekani katika eneo vilitabiri kuwa, Pakistan nayo kutokana na kupokea misaada ya fedha kila mwaka kutoka nchi hiyo itaafiki na kutekeleza siasa za mashinikizo ya juu za viongozi wa Washington ili kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni. Hata hivyo msimamo wa wazi na usioyumba wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan katika kupinga kuutambua rasmi kivyovyote vile utawala haramu wa Israel unaonyesha kuwa Islamabad haiko tayari kukiuka misingi yake ya kuunga mkono haki zilizoporwa za wananchi wa Palestina kwa sababu ya mashinikizo ya White House.