Pakistan hali tete

HIMARS

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
73,321
Reaction score
103,591
Imran Khan adai anataka uawa

Wafuasi wake zaidi ya 61 wakamatwa

Nyumba yake yavamiwa, silaha zakutwa

Vyombo vya habari vimezuiwa kurusha habari za maandamano

Yuko Lahore Mahakamani
 
Imran Khan adai anataka uawa

Wafuasi wake zaidi ya 61 wakamatwa

Nyumba yake yavamiwa, silaha zakutwa

Vyombo vya habari vimezuiwa kurusha habari za maandamano

Yuko Lahore Mahakamani
Huyu jamaa anapambana mno kurejea madarakani...ila jeshi halimtaki kabisa huku likimuona kama mtetezi wa magaidi.
 
Wabunge wa vyama vya upinzani katika Bunge la Pakistan waliazimia kumuondoa madarakani Waziri Mkuu, Imran Khan wakidai kuwa sera zake zinachochea kuongezeka kwa mfumuko wa bei nchini humo na hatimaye Bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.
 
Huyu jamaa anapambana mno kurejea madarakani...ila jeshi halimtaki kabisa huku likimuona kama mtetezi wa magaidi.
Tatizo lilianza kuonekana kati ya Jeshi la Pakistan na Imran Khan, baada ya Idara ya ujasusi wa jeshi la Pakistani (ISI) kutangaza jina la mkurugenzi mkuu wao Luteni Jenerali Nadeem Anjum alieteuliwa kuchukua nafasi ya Jenerali Faiz Hameed kama mkuu wa idara ya ujasusi wa jeshi. Isipokuwa uteuzi huu haukufuata hatua na utaratibu wa kawaida.
 
Imran alifurahia mno Taliban kurejea madarakani huko Kabul, hakukumbuka kuwa magaidi wa Ttp na Taliban ni washirika wa karibu.

Leo Ttp wanaitumia Afghanistan kama uwanja wa kuishambulia Pakistan, tena wamiliki silaha nyingi za kisasa zilizoachwa na Marekani walipoondoka.
 
Khan anang'ang'a kurudi madarakani wakati alifukuzwa kutoka kwenye nafasi ya waziri mkuu wa Pakistan baada ya bunge kuidhinisha kura ya kutokuwa na imani naye.
Anadai Marekani walichochea mapinduzi ya kumtoa.

Huyu babu kaipa nguvu Ttp kwa sera zake akidhani Taliban kurejea madarakani huko Kabul ni kuzima ushawishi wa India.
 
Mbona unarazimasha mawazo unayo yawaza ww mkuu kilicho fanya jeshi limpindue ni jaribio lake la kutaka kuondoa ushawishi wa jeshi ndani ya siasa za taifa hilo hicho ndo kimemponza.
 
Mbona unarazimasha mawazo unayo yawaza ww mkuu kilicho fanya jeshi limpindue ni jaribio lake la kutaka kuondoa ushawishi wa jeshi ndani ya siasa za taifa hilo hicho ndo kimemponza.
Hayo pia ni mawazo yako tu ila mfumuko wa bei, mdororo mbaya wa Uchumi, kurozota kwa hali ya usalama, tuhuma za rushwa yalichangia Sana kumtoa.

Halafu ni kura za wabunge zilimtoa sio jeshi.
 
Hayo pia ni mawazo yako tu ila mfumuko wa bei, mdororo mbaya wa Uchumi, kurozota kwa hali ya usalama, tuhuma za rushwa yalichangia Sana kumtoa.

Halafu ni kura za wabunge zilimtoa sio jeshi.
Hayo yote yamechangia ila hilo ndo kubwa, alafu kuhusu usalama hakuna kipindi ambacho Pakistan ilitulia kama kipindi cha Khan.
 
Kumbe jamaa anasiasa za mlengo mkali hivi binafsi sikumjua vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…