Pacemaker ni nini?

Pacemaker ni nini?

Life2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,387
Reaction score
4,881
Siku za karibuni tulisikia upasuaji uliofanyika Hospitali ya Muhimbili kitengo cha magonjwa ya Moyo kwa mtoto kuweka kifaa cha bandia ndani ya Moyo Wake.

Je, Pacemaker ni nini? Moyo umeundwa na kitu kina kinachoitwa #SINOATRIAL NODE ambacho kazi yake ni kuzalisha umeme ili kusaidia moyo kusukuma Damu vizuri kwa mapigo yanayotakiwa sehemu za mwili.

Sinoatrialnode ipo chumba/chamber ya juu upande wa kulia (right atrium) wa moyo, sinoatrialnode ni pacemaker ya asili ya moyo(natural).

Endapo pacemaker ya asili inashindwa kufanya kazi kutokana na magojwa ya moyo ndipo pacemaker ya kutengenezwa (artificial) hupandikizwa katika moyo ili kusaidia Moyo kufanya kazi sawasawa kifaa hiki huzalisha umeme ambao husaidia moyo kusukuma damu hufanya kazi sawa na kile cha asili, kimeundwa na betri ambazo huweza badilishwa baada ya miaka 5-6 ukifanikiwa kukaa karibu na mtu mwenye hiki kifaa utasikia kikipiga kama mishale ya saa za ukutani pakiwa na utulivu na pale betri zinapoisha hubadilishwa na kifaa kuendelea na kazi zake hiyo ni Pacemaker.

Wataalamu tujuzane zaidi.
 
Kinaconectiwaje ili moyo upate chaji/ uwezo wa kupiga.

maana moyo hauna nyaya kwamba kitaungwa.

sijui nimeeleweka.
 
Pacemaker kwa kiswahili chepesi ni kama switch ya Moyoo hiki kidude hutumika kama njia isiyo ya asili ya Kuanzisha mapigo ya moyoo maana kiasili moyo hujiendesha wenyewe bila kutegemea ubongo au kiungo chochote kile..!!

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom