PAC yashtushwa na mtaji wa 150,000 wa mwekezaji Mlimani City

Tuwashangae wote wanaosema 'madudu yanagunduliwa'. Yanagunduliwa vipi haya kwa sasa wakati yakitendeka watu walipigia kelele wizi huo wa wazi; lakini masikio yao yalizibwa na waliopiga kelele waliitwa wapinzani. Sasa wao wamegeuka na 'kuyaona' hayo madudu na wale walioyasema huko nyuma wanaitwa wachochezi na siyo wazalendo. What a crooked world.
 
ile karma ya watumishi hewa bado mbichi sana......nchi hii watu wanaamini makaratasi kuliko uwezo...kuwa na phd ni jambo moja but kuitumia hiyo phd kuwa na tija ni issue nyingine kabisa...nchi hii ina maprofessor hewa na phd hewa nyingi....natamani sana Tanzania itakayopima watu kwa uwezo na matokeo badala ya huu upuuzi wa vyeti...kuna majitu ya ovyo ovyo yamejaa kwenye taasisi za umma yanafanya maamuzi ya kibatamzinga kisa masters, na phd....inashangaza sana UDSM inashindwa kusimamia kamlimani city....ndo haya haya maprof uchwara yalikuj na hesabu zao za noah moja moja kwa kila mtz .....yaani bora hata siko huko maana ningekata shingo tu mpaka waliobakie warudishe phd waanze ipya kutafuta weledi....hii nchi inapotezwaga nao wasomi hewa...mnafukuza watu wasio na vyeti vya form 4 bt degree ni zao mnaacha makina lipumba mtaani ...yaani ningewafanya kitu cha*#@#%%#@*##%%
 
Mwekezaji alikuja na $75, kwa hiyo nani kajenga pale Mlimani?
 
Aiseeeee imagine na hapo ndio UDSM.. Home of intellectuals.. na wanaibiwa/wanaiba hivi..!? Sbb hilo ni dili la wazi kabisa, OMG..!!

I believe Mh. Rais wetu atatumbua watu hapa na kuwa kamata akina Mkandara..!! This is shame!! Inatia aibu sana jamani.. Yaani nchi hii, aisee
 
Hii hoja ya kuwa eti mwekezaji alikuja na mtaji wa 150000 ni dhaifu kbs. Wenzetu huwa hawaangalii mtaji wanachoangalia ni Idea. Mzungu alikuja na idea wakampa ardhi akaenda bank akapata pesa ndo maana leo mlimani city inapeform.
Kamati ya kina Lusinde (zero brain) isiangalie tu investment in terms of money, it should look on idea that investor imposed.
Labda tujadili hoja ya gawio na miaka lkn hii ya alikuja na shilingi ngapi ni si hoja. Mtaji wa kwanza kwa mzungu ni Akili.
 
Mwekezaji alikuja na $75, kwa hiyo nani kajenga pale Mlimani?
Swali hilo lafanana na wale Wadosi Airtel...
Wanadai Mwekezaji alitumia rasilimali za UDSM kuombea mikopo na kujenga hapo!
Ni Tanzania tu kwa kweli, yaani tuna umaskini wa kujitakia kwa kweli...hata hao hao Wazungu wanatushangaa tunapoenda na bakuli kuomba misaada, tunatia aibu...
 
Ni nani alijenga Mlimani City. Ni mwekezaji au serikali?
Aliyejenga ni mwekezaji lakini bila shaka alikopa pesa kutoka mabenki ya ndani na kujenga! Hilo jengo la mlimani city siyo jengo Bali ni banda kubwa! Halina thamani kubwa na life span yake ni ndogo sana. Mkataba ukiisha na jengo litakuwa lime-expire! Ni ajabu na kweli! Mikataba mingi ikiwemo ya madini ambayo imebaki kuwa ni siri ya wanufaika wachache (waliokuwa na dhamana kama vile joka la makengeza), ina vituko ambavyo vikiwekwa wazi hakuna anayeweza kuamini kilichomo!
Ndiyo maana hakuna anayethubutu kuruhusu mikataba ya madini na gesi kupelekwa bungeni!!!
 
CCM inafilisi nchi
 
halafu tunawasifia kina Profesa Kabudi, he was the in-house lawyer aliyebariki hii mikataba
 
Another usanii wa kiwango cha lami... udsm ndyo ilotoa aslimia kubwa ya wateule wa sasa does it mean hawakuona huu mtaji?? Serikali iliyoingia huo mkataba ni ya Chama hiki hiki cha sasa haikuona?? Hivi wahusika wa wakati ule na wasasa wanatofauti?? USD 75 ardhi yote ile tuna shida mahali aseee
 
Hawa hawana mpango wowote kazi yao kubwa kuwaza matumbo yao huku nchi ikiteketea kwa sababu ya udhaifu wa muhimili wanaoutumikia
 
Ww naona ni walewale tu! sasa hapo chuoni hakuna ma phd holder na wanafanya nn km hata kuwa idea km hiyo ya kujenga shoping malls walikua hawana. Alipo kuja huyo mwekezaji na idea yake huku hana mtaja si wangempiga chini wakasimamia wao.Kwa hapo broo hakuna la kujitetea tuna wasomi fekiiiiii ambao elimu haijawakomboa sio siri naionea sana huruma Tz Yetu km ndo wasomi dizain ya vyuo vyetu tunaowategemea.FULL KUKARIRI TU.
 
Upuuzi... Yaani uje na vihela vyako mbuzi uhonge wapumbavu wachache upewe ardhi yetu kijinga uende bank pengine za ndani uchukue hela alafu usifie idea? Kumbaaafu in tz ardhi yote ni ya raisi # Mrpresident we need our land at mlimani city
 
Watanzania tusiwe wanafki kwenye hili mtu amecreate idea na akaweza kuandaa proposal na kuipresent ipasavyo mpaka UDSM wakampa ardhi kutekeleza idea yake then taasisi nyingine ndio ichukuwe huo mradi na kuutekeleza it's not good

Cha kuhoji hapo ni mikataba waliyoandikishiana ili kuwa fair in both side but kujaji kwamba why udsm hawakujenga wenyewe ni unafki na wivu wa maendeleo ya mtu

Poor thinking ndio maana hatuendelei.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…