ozil atatesa sana kwenye Assist kuliko mchezaji mwingine duniani

Jospina

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
2,421
1,387
Ozil atatesa kwenye assists kwa sababu ana akili nyingi mno. Hatoi pasi za mwisho bila kuwa na uhakika wa asilimia nyingi kwamba atakayempasia ana nafasi kubwa ya kuweza kufunga kuliko wengine. Hutoa pasi za mwisho si kwa kubahatisha.

Wakiwa kwenye nafasi za kufunga Giroud, Walcott na Ramsey kwa mfano, atampasia yule anayeamini atafunga.

Akiona hakuna mwenye nafasi ya kufunga miongoni mwao, ataanzisha move kwingineee kama kushoto kwa Monreal au kulia kwa Bellerin ama nyuma kwa Flamini ili watu wajiweke sawa kufunga.

Hujaribu kufunga mwenyewe anapoona yeye ana uwezo mkubwa zaidi wa kufanya hivyo kuliko wengine na hufanya hivyo akiwa tu na uhakika wa kufunga.

Kuna shabiki mwenzangu wa Arsenal aishie nje ya nchi aliwahi kuniambia kwamba Ozil akishatoa pasi ya mwisho humwambia aliyempasia "score" akiwa na uhakika akitekeleza ushauri wake ata-"score".
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom