Oya hamjambo lakini?

Oya hamjambo lakini?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
63,006
Reaction score
126,389
Haya tuachane na ya Jana (hasa humu Mitandaoni) tuamke na tukafanye Kazi ili kujiletea Vipato, kutunza Familia zetu na kuimarika Kimaendeleo.
 
Mimi ndio nimeamka salama Alhamdulillah sasa najiandaa niende shule
 
Jana , tumethibitisha kuwa vijana wa Tanzania ni nguzo ya mshikamano, tumetii sheria, tumedumisha utulivu, na tumeonesha uzalendo wa kweli kwa taifa letu. Tuendelee kuwa mfano wa kuigwa, tukilinda amani yetu na kuimarisha umoja uliotuleta hapa. Kumbuka, vijana ndio mashine ya maendeleo ya nchi, tuzidi kusimama pamoja kwa upendo, hekima na ujenzi wa taifa letu. MUNGU IBARIKI TANZANIA , MUNGU IBARIKI AFRIKA. #TANZANIA #AFRIKA #AMANI
wavimba_20251210_062702_0000.png
 
Ndugu yangu GENTAMYCINE tusameheane sana kwa haya yaliyotokea hapo nyuma, ningependa tufahamiane zaidi, ikiwezekana angalau tukutane tupige vyombo hata chupa mbilimbili, moja moto moja baridi unaonaje ndugu yangu? NYUMA YA PAZIA.
 
Acheni kuteka na kuua watu 📌
Tendeni haki 📌
Wasikilizeni wananchi 📌
Punguzeni ufisadi 📌
Ruhusuni katiba mpya 📌
Inueni uchumi wa watu wenu 📌
Ruhusuni tume huru ya uchaguzi 📌
Shughulikeni na ajira kwa vijana 📌
Punguzeni nepotism 📌


Kutoyazingatia haya machache kutazidi kuchochea moto mioyoni mwa watu. Na nchi haitakuwa salama. Kunaweza kuwa na utulivu lakini kusiwe na amani. Ni kama kuwa na bomu chini ya kitanda chako!

Kwa sasa mnaweza kufurahi na kupongezana kuwa mmefanikiwa kuzuia maandamano tena kwa gharama kubwa ya ku-mobilize jeshi utafikiri nchi imo vitani lakini wananchi mnaowaongoza wana hasira na visasi. Na huwezi kutawala watu ambao hawakukuchagua na hawakutaki. Wengi walishajaribu wakashindwa na hawakuwa na mwisho mwema.

Samia atajaribu kutawala kwa kutumia mitutu ya bunduki, kuteka na kuua watu lakini hataweza na, kama historia ni mwalimu sahihi, hatakuwa na mwisho mzuri. Na ataishia katika pipa la takataka la historia kama kiongozi katili, muuaji, fisadi na asiyejali.

Anajua hakuchaguliwa na wananchi. Anajua hakupata kura milioni 32. Anajua hakushinda kwa 98%. Anajua uchaguzi ulivurugika. Anajua alijiapisha kimagumashi. Anajua siyo rais halali. Anajua anaongoza serikali haramu. Basi angalau ajaribu kutenda haki ili ajikongoje na hii miaka mitano yake ambayo itakuwa mirefu na ya mateso sana kwake hasa akiendelea na huu udikteta wake.

Mungu Aendelee kuibariki nchi yetu hii nzuri yenye kila kitu lakini inaharibiwa na wanasiasa wasio na maono, walafi, wauaji, mafisadi na wasiojali! 🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿

IMG-20251209-WA0008.jpg
 
Back
Top Bottom