Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,464
- 6,775
Wakuu,
Makamu wa kwanza wa Rais, Othman Masoud Othman, amejiandikisha katika Daftari la Wapigakura wapya katika kituo cha uandikishaji Shule Mpendae, visiwani Zanzibar.
Akizungumza baada ya kujiandikisha, leo, Masoud ambae pia ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, amesema kujiandikisha katika hilo, haina maana ya kwamba hakuwahi kupiga kura.
Amesema uchaguzi uliopita wa mwaka 2020 hakupiga kura, kwa sababu hakuwapo nchini.
Alisema tangu uchaguzi wa mwaka 1990 ameshiriki kupiga kura katika chaguzi zote isipokuwa uchaguzi wa mwaka 2020.
Othaman, amejiandikisha leo, ikiwa ni siku ya mwisho ya uandikishaji wa Daftari la Wapigakura, Zanzibar.
Source: Nipashe