Othman Chande, Jaji Mkuu wa Tanzania - Mahakama ya Rushwa na Ufisadi itazinduliwa lini?

kimwela

Member
Mar 25, 2016
17
25
Awali ya yote nikupongeze wewe Mh. Jaji Mkuu na Mahakama unayoiongoza kujitahidi kusimamia haki, hasa haki za wanyonge wa taifa hili, ambao hustakiwa na kutiwa hatiani kwa makosa ambayo hawakuyafanya, hata kama waliyafanya adhabu zinazotolewa pengine huwa kubwa mmo na kuyajaza Magereza yetu wafungwa wengi na kuongeza matumizi makubwa ya Serikali.
Napenda kujua toka kwako Mh. Jaji Mkuu, Mahakama tajwa hapo juu ambayo ilikuwa ni ahadi ya Mh. Rais itaanza lini?, kwani hivi sasa tunashuhudia wala rushwa na mafisadi wanapelekwa Mahakamani kwa makosa ya ubadhirifu waliyoyafanya.
Tamaa yangu kubwa si tu kuona wanapewa haki wanayostahili, bali mali walizochuma kwa njia zisizo halali zinarudishwa katika hazina kuu ya taifa ili ziwasaidie wanyonge wa taifa hili kupata tiba bora, elimu bora, umeme nafuu, barabara imara, maji salama, n.k.
Shime Mh. Jaji Mkuu Mahakama ya rushwa na ufisadi inasubiriwa kwa hamu na gamu.
 
Back
Top Bottom