Orodha ya walipa kodi:utata mtupu!

SUPERUSER

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
960
304
Habari wakuu,

Ivi ni kwanini Vodacom haiko kwenye orodha ya makampuni 15 ya walipa kodi bora iliyotajwa na pm?.Mimi najua vodacom ni kampuni kubwa kuliko airtel kwa kuwa mtandao wake unaongoza kwa kuwa na subscribers wengi ukiacha mbali mamilioni ya watanzania wanaotumia huduma ya mpesa..na ni kwanini hawa vodacom hawadisclose financial statement zao(audited report)? Je watakua wana evade kulipa kodi?...Ni kweli Rostam Aziz anamiliki 35% ya kampuni hii?

Jambo lingine la kushangaza sana katika orodha hii ni kutokuwepo kwa kampuni kubwa za madini. Katika orodha hii kuna kampuni moja tu ya madini, Resolute. Kampuni hii ina mgodi mmoja tu uliopo Nzega. Mgodi mkubwa zaidi nchini ni Geita Goldmine unaomilikiwa na AngloGoldAshanti, haimo katika orodha. Kampuni ya AfricanBarrickGold inamiliki migodi 4, North Mara, Buzwagi, Tulawaka na Bulyanhulu. Hii ndio kampuni kubwa ya madini kuliko zote mpaka kufikia hatua ya kujoin London stock of exchange,haimo katika orodha.

On top of that, Mohamed Entreprises uzalishaji wake ni sawa na asilimia 4 ya uzalishaji wa nchi (GDP). Haimo katika orodha.
Bakhresa Group of companies ni moja ya kampuni kubwa nchini zenye mafanikio makubwa katika mauzo ya nje. Kimsingi mwaka 2010 mafanikio makubwa katika kuuza ndani ya Afrika Mashariki, yanatokana na kampuni hii. Ziada tuliyonayo dhidi ya nchi nyingine za EAC katika mauzo nje kimsingi ni ziada ya Bakhresa Group, haimo katika orodha.

Kwa uelewa wangu makampuni huwa yanalipa corporate tax at the rate of 30%...au vigezo vimebadilika wakuu?
 
i. Tanzania Breweries Ltd. (Shilingi Bilioni 165.4);
ii. National Microfinance Bank (Shilingi Bilioni 108.6);

iii. Tanzania Cigarette Company (Shilingi Bilioni 92.1);

iv. National Bank of Commerce (Shilingi Bilioni 89.9);

v. CRDB Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 79.2);

vi. Tanzania Ports Authority (Shilingi Bilioni 76.8);

vii. Tanzania Portland Cement (Shilingi Bilioni 73.4);

viii. Airtel (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 63.6);

ix. Tanga Cement Company Ltd. (Shilingi Bilioni 43.6);

x. Standard Chartered Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 40.0);

xi. Citibank (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 35.7);

xii. Resolute (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 32.1);

xiii. Tanzania International Container Terminal Services (Shilingi Bilioni 25.9);

xiv. Tanzania Distillers Ltd. (Shilingi Bilioni 13.4); na

xv. Group Five International (PTY) Ltd. (Shilingi Bilioni 9.5).
 
ni hawa hawa Vodacom wanaogoma kulipa hata ushuru wa mabango halmashauri ya jiji

Exim bank pamoja na ukubwa wao wamezidiwa na Citibank na Standard Chartered
 
i. Tanzania Breweries Ltd. (Shilingi Bilioni 165.4);
ii. National Microfinance Bank (Shilingi Bilioni 108.6);

iii. Tanzania Cigarette Company (Shilingi Bilioni 92.1);

iv. National Bank of Commerce (Shilingi Bilioni 89.9);

v. CRDB Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 79.2);

vi. Tanzania Ports Authority (Shilingi Bilioni 76.8);

vii. Tanzania Portland Cement (Shilingi Bilioni 73.4);

viii. Airtel (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 63.6);

ix. Tanga Cement Company Ltd. (Shilingi Bilioni 43.6);

x. Standard Chartered Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 40.0);

xi. Citibank (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 35.7);

xii. Resolute (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 32.1);

xiii. Tanzania International Container Terminal Services (Shilingi Bilioni 25.9);

xiv. Tanzania Distillers Ltd. (Shilingi Bilioni 13.4); na

xv. Group Five International (PTY) Ltd. (Shilingi Bilioni 9.5).
Sijajua chanzo na ukweli wa hizi takwimu.Hata hivyo kwa haraka nimeona vitu viwili vyenye ujumbe kwa watanzania.Kwanza ni jambo la aibu kwamba kampuni za kuuza ulevi na sigara ndizo zinazoongoza kwa kulipa kodi.Hiki ni kipimo cha jinsi gani taifa la Tanzania ni la walevi.Ubaya wa kodi hizi ni kuwa inaonekana ni faida machoni lakini hasara yake ni kubwa kuliko faida yake.
Jengine ni kupitwa kwa CRDB bank na NBC.Ukiangalia wingi wa wateja wa Crdb utadhani ina mapato makubwa saana.Bila shaka NBC yenye wateja wachache wanapata faida zaidi kupitia akaunti zao za Islamic ambazo hawaziingizii riba.
 
Kwa kweli inashangaza sana yaani Vodacom kodi hawakufikisha hata bilioni 9.5 (reference kwa kampuni la mwisho hapo kwenye orodha) wakati ndo kampuni kubwa kuliko yote nchini? Kumbe mbwembwe zao za kusaidia jamii huwa ndo kichaka cha kujifichia? Kumbe ndo maana kila wakati wa bunge wanakwenda kuwapa chakula na mziki wabunge ili wawanyamazie kwa huu uhuni wao? Kwa hili itanifanya sasa nipunguze matumizi yangu ya simu ya Vodacom.
 
Back
Top Bottom