Orodha ya marais waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa madarakani

steve_shemej

JF-Expert Member
Nov 26, 2015
1,092
1,433
BAADA ya wiki iliyopita kuwaletea marais wa Afrika waliofia madarakani. Yaani walikuwa wakiongoza nchi zao wakakumbwa na mauti. Wiki hii tunawaletea marais waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa madarakani.

ABRAHAM Lincoln: Alikuwa Rais wa 16 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1865 jijini Washington kwa kupigwa risasi kichwani kwa nyuma na John Wilkes. Alikuwa amekaa na mkewe. Bastola iliyotumika inaitwa Deringer.

INDIRA Priyadarshini Gandhi: alikuwa Rais wa India. Aliuawa mwaka1984 kwa kupigwa risasi na walinzi wake, Satwant Singh na Beant Singh jijini New Delh, India.

JOHN Francis Kennedy ‘JFK’: Ni Rais wa 35 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1963 mjini Dallas kwa kupigwa risasi na Lee Harvey akiwa kwenye gari la wazi barabarani.

LAURENT Desire Kabila: Alimng’oa madarakani Rais Mabotu Seseko wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, lakini mwaka 2001 akauawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa ni walinzi wake.

THOMAS Isdor Noel Sankara: Alikuwa Rais wa Burkina Faso Alitawala nchi kwa miaka 4 hadi 1984 alipouawa kwa kupigwa risasi na Blaise Compaore ambaye hivi karibuni ameikimbia nchi hiyo.

WILLIAM Richard Tolbert Jr: Alipigwa risasi mwaka 1980 katika mapinduzi ya kijeshi akiwa Rais wa Liberia. Samuel Doe akiwa na cheo cha sajenti ndiye aliyetajwa kumuua.

MUHAMMAR Muhamad Abu Migar al Ghaddaf: Alikuwa Rais wa Libya kwa miaka 42. Aliuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa kwenye vurugu za kisiasa mjini Sirte, Libya, Oktoba 20, 2011.

ABEID Amani Karume: Alikuwa Rais wa Zanzibar tangu mapinduzi ya mwaka 1964. Aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa anacheza bao mwaka 1972 na mtu ambaye hakuwahi kupatikana.

Jean Baptist Ouedraogo: Aliitawala Burkina Faso kwa mwaka mmoja tu, 1982-83. Aliuawa kwa kupigwa risasi na Thomas Sankara ambaye alichukua madaraka ya kuiongoza nchi hiyo kabla na yeye kupinduliwa.

marais.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna Rais Marekani alikufa Kwa kipindupindu. Indira Gandhi hakuwa rais.

Mutharika alikufa Kwa kutopewa huduma ya kwanza baada ya heart attack.
Kama amna editing kwenye huu uzi, basi nikupe pole mzee baba kwa kukurupuka kuchangia
 
Nasomaga historia zao hawa watu... Sankara kumbe nae aliua?

Sent using Jamii Forums mobile app
Eeh captain Thomas sankara aliuawa baada ya kupinduliwa na rafiki yake compaore,
Kuna mwingine nae aliitwa Sajenti Samweli Doe,alikuwa noma yule kijana,nae akauawa na majeshi ya Prince Johnson akishirikiana na Charles Tylor,Hawa walikuwa wamarekani weusi waliorudi nyumbani kutoka US.
 
Eeh captain Thomas sankara aliuawa baada ya kupinduliwa na rafiki yake compaore,
Kuna mwingine nae aliitwa Sajenti Samweli Doe,alikuwa noma yule kijana,nae akauawa na majeshi ya Prince Johnson akishirikiana na Charles Tylor,Hawa walikuwa wamarekani weusi waliorudi nyumbani kutoka US.
Hiyo Liberia sasa eti?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom