Orodha ya majenerali wa JWTZ toka liundwe

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2016
Messages
4,604
Points
2,000

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2016
4,604 2,000
Kwetu hatuna marshal. Tunaishia four star general. Hata hivyo pia marehemu Kiwelu Tumainieli alifikia kuwa jenerali ingawa hakuwa Mkuu wa majeshi
Dah! Mkuu hiyo arguement yako naona kama ligi ambayo siwezi kuishiriki sawasawa, maana ninayokueleza nina uhakika nayo.

Cheo kutovaliwa siyo kwamba hakipo.
Muundo wa vyeo vya Jwtz baada ya private (plain shirt) kuna Lance corporal hadi (Field) Marshal.

Vyeo vya jeshi huvaliwa kutokana na sifa pia muundo.
Unaweza kuwa na sifa lakini muundo kama hauruhusu, hauwezi kuvalishwa cheo husika.

Pia muundo unaweza kuruhusu, lakini mtu mwenye sifa ya kuvaa cheo hicho akakosekana.

Pia nimekueleza generali kinaanzia ubrigedia.
Huyo Kiwelu unayemsema kastaafu na cheo cha Lt gen na siyo gen.
 

Threesixteen Himself

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Messages
7,815
Points
2,000

Threesixteen Himself

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2013
7,815 2,000
Mayunga, Waitara Walikuwa Balaa

Ila Mwamunyange Kaacha Historia Kubwa Kiasi Baada Ya Kubadili Jeshi Kuwa La Kisasa"

JWTZ Ndio Jeshi Linaloongoza Afrika Kufanya Operation Hatari Za Chini ( Vita Ya Chini) Kuliko Jeshi Lolote Lile"

!
!
Mh.... Tumeanza Kuoeana Matango Pori Sasa.
 

Ndinani

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2010
Messages
5,634
Points
2,000

Ndinani

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2010
5,634 2,000
Kwetu hatuna marshal. Tunaishia four star general. Hata hivyo pia marehemu Kiwelu Tumainieli alifikia kuwa jenerali ingawa hakuwa Mkuu wa majeshi
Huyu General Kiwelu alifariki lini? Nakumbuka baada ya kuwa Mkuu wa mkoa wa Kagera aliamua kustaafia huko. Umauti ulimfika akiwa huko huko Kagera?
 

jamvimoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Messages
560
Points
500

jamvimoto

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2015
560 500
Mimi nitaanza kuwatambua wakichua na wakikalia kiti cha magogoni kidogo,wanasiasa nimewakinai,wanajilipa mamilion kwa kupiga kabobo bungeni na majukwaani huku watendaji waskistaafu masikini,kujitoa ufahamu kusifia hata upumbavu na kupewa shave.Jembe si jembeee!!!
 

Malafyale

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2008
Messages
12,770
Points
2,000

Malafyale

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2008
12,770 2,000
Uzi huu Ni kwa ajili ya kuwatambua majenerali wote wa JWTZ toka iundwe mwaka 1964 tukitambua umahiri wao katika kuiweka Tanzania yetu salama

Mimi naanza na Hawa wachache ninaowakumbuka

Twalipo
Musuguri
Kiwelo
Mayunga
Makunda
Mboma
Mabeyo
Mwamunyange
Shimbo
Waitara
Muhidini

Endeleza list yako sio vibaya pia katika kunogesha tukapata matendo yao ya ushujaa katika utumishi wao.

Tuwaenzi hawa kama Israel inavyowaenzi majenerali wake wa IDF wote wako wikpedia sisi tunashindwa nini?
HAUPO sahihi kabisa.
Wengi hapo ni ma Major General na ma Luten General
Majeneral walio wahi kuwepo TZ ni
Twalipo
Msuguri
Mboma
Waitara
Mwamunyange
Mabeyo
Hao wote juu waliwahi kuwa CDF ndiyo maana ni Generals,Sarakikya aliwahi kuwa CDF kwa cheo cha Major General
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
31,414
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
31,414 2,000
Mimi nami niliwahi kufanya kajiutafiti cha majina ya majenerali hao nikishabihanisha na dini zao, nilishangaa na nikauliza humu

P
 

superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Messages
2,698
Points
2,000

superbug

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2018
2,698 2,000
HAUPO sahihi kabisa.
Wengi hapo ni ma Major General na ma Luten General
Majeneral walio wahi kuwepo TZ ni
Twalipo
Msuguri
Mboma
Waitara
Mwamunyange
Mabeyo
Hao wote juu waliwahi kuwa CDF ndiyo maana ni Generals,Sarakikya aliwahi kuwa CDF kwa cheo cha Major General
Lengo la uzi sio wakuu wanmajeshi cdf Bali ni yeyote aliyewahi kuwa luteni jenerali meja jenerali brigedia jenerali au jenerali wa jwtz kumbuka Hawa ni watu muhimu Sana katika taifa lolote Lile imagine tunawakumbuka wakuu wa mikoa na ma dc wa miaka ya tisini themanini ila tunashindwa kuwatambua na kuwaenzi wapiganaji wetu hii ni aibu
 

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
16,685
Points
2,000

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
16,685 2,000
superbug,

..ngoja nijaribu kuiweka sawa hoja yako.

..ktk JWTZ ngazi ya Jenerali inaanzia na cheo cha Brigadier-General.

..Brigadier-General ni One Star General.

..Major-General ni Two Star General.

..Lieutenant General ni Three Star General.

..General ni Four Star General.

..Nafasi Mkuu wa Majeshi au CDF imekuwa ikishikwa na Majenerali kulingana na muundo na ukubwa wa jeshi letu.

..wakati JWTZ inaanzishwa mwaka 1964 mkuu wa majeshi alikuwa na cheo cha Brigadier.

..Sam Hagai Mirisho Sarakikya alipandishwa cheo toka Captain kuwa Brigadier na kuteuliwa kuwa CDF wa kwanza mwaka 1964.

..Chief of Staff wa kwanza nadhani alikuwa Elisha Kavana. Kama sijakosea cheo chake kilikuwa Major.

..Sarakikya nadhani alipanda cheo na kuwa Major General. Baadaye aliteuliwa na kuwa Waziri wa Michezo, halafu akawa balozi Ethiopia, Nigeria, na Kenya.

..CDF wa pili alikuwa ni Abdalah Twalipo. Kabla ya uteuzi wake alikuwa RC mkoa wa Ziwa Magharibi. Sasa hivi tunauita mkoa wa Kagera. Twalipo alipandishwa cheo toka Colonel na kuwa Major General.

..Wakati wa Major General Twalipo kulikuwa na Chief of Staff anaitwa Brigadier Nkwera. Sijui huyu aliteuliwa wakati wa Sarakikya au la. Lakini najua alitumikia kipindi fulani na Major General Twalipo kabla hajahamishwa kwenda kuanzisha Rubada [ Rufiji Basin Development Authority ].

..Baada ya Brigadier Nkwera alifuatia Lt.Col.Tumainieli Kiwelu ambaye alipandishwa cheo na kuwa Brigadier na kuteuliwa kuwa Chief of Staff.

..Vita vya Kagera vilianza Mkuu wa Majeshi / CDF akiwa na cheo cha Major General. Na wakati wote wa vita hiyo Mkuu wa majeshi alikuwa ni Major General Abdalah Twalipo.

..Sina uhakika kama kulitokea mabadiliko wakati wa vita vya Kagera au baada ya vita hivyo.

..Abdalah Twalipo alipandishwa cheo na kuwa Lieutenant General akiwa bado ni CDF.

..Ma-Brigadier walioongoza vita vya Kagera walipandishwa vyeo na kuwa Major Generals.

..Baada ya Abdalah Twalipo nafasi ya CDF ilishikwa na David Musuguri akiwa na cheo cha Lieutenant General.

..Nadhani Musuguri alitumikia pamoja na Chief of Staff Major General Imran Kombe, na baadae Major General Martin Mwakalindile.

..Wakati Mwalimu Nyerere anastaafu aliwapa nishani waTz mbalimbali wakiwemo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

..Katika tukio hilo pia Mwalimu aliwapandisha cheo Abdalah Twalipo na David Musuguri kutoka Lieutenant General kuwa General.

..Twalipo ndiyo alikuwa wa kwanza kuvikwa cheo hicho, halafu akafuatiwa na Musuguri.

..Raisi Mwinyi alipokuwa Raisi alifanya mabadiliko ya CDF na CS.

..Major General Ernest Mwita Kyaro alipandishwa cheo kuwa General na kuteuliwa kuwa CDF.

..Raisi Mwinyi pia alimpandisha cheo Major General Tumainieli Kiwelu kuwa Lieutenant General na kumteua kuwa CS.

..Raisi Benjamin Mkapa naye alifanya mabadiliko ya CDF na CS ambapo aliwateua Robert Mboma na Geofrey Sayore.

..Katika mabadiliko hayo Raisi Mkapa alimpandisha cheo Lt.Gen.Kiwelu kuwa General na kumteua kuwa Balozi wa Tanzania Ufaransa.

NB:

..Raisi Mkapa kabla hajastaafu alimpandisha cheo Balozi Major General Sam Hagai Mirisho Sarakikya kuwa General.

..Major General Silas Mayunga na Imran Kombe walipandishwa kuwa Lieutenant General lakini sijui ni Raisi yupi aliwapa vyeo hivyo.

..Ernest Mwita Kiaro alijiunga na jeshi akiwa Private na ameshika vyeo vyote jeshini isipokuwa Lieutenant General.

..Tumainieli Kiwelu ndiye pekee amewahi kuwa Chief of Staff au Mnadhimu Mkuu wa JWTZ mara mbili. Na ndiye General pekee ambaye hakuteuliwa kushika wadhifa wa CDF au Mkuu wa Majeshi.
 

eddy

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2007
Messages
11,813
Points
2,000

eddy

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2007
11,813 2,000
Mimi nitaanza kuwatambua wakichua na wakikalia kiti cha magogoni kidogo,wanasiasa nimewakinai,wanajilipa mamilion kwa kupiga kabobo bungeni na majukwaani huku watendaji waskistaafu masikini,kujitoa ufahamu kusifia hata upumbavu na kupewa shave.Jembe si jembeee!!!
Mbona yupo tayari ikulu, rais gani anapiga pushup Kama sio mjeda
 

Ulimakafu

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Messages
21,702
Points
2,000

Ulimakafu

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2011
21,702 2,000
Uzi huu Ni kwa ajili ya kuwatambua majenerali wote wa JWTZ toka iundwe mwaka 1964 tukitambua umahiri wao katika kuiweka Tanzania yetu salama

Mimi naanza na Hawa wachache ninaowakumbuka

Twalipo
Musuguri
Kiwelo
Mayunga
Makunda
Mboma
Mabeyo
Mwamunyange
Shimbo
Waitara
Muhidini

Endeleza list yako sio vibaya pia katika kunogesha tukapata matendo yao ya ushujaa katika utumishi wao.

Tuwaenzi hawa kama Israel inavyowaenzi majenerali wake wa IDF wote wako wikpedia sisi tunashindwa nini?
Kwa muundo wa JWTZ generals wanaanzia Brigedia Generali mpaka Generali hivyo ni wengi, na uliowataja hapo juu baadhi hawakufikia full general.
 

Forum statistics

Threads 1,343,347
Members 515,021
Posts 32,781,651
Top