Orodha waliofunguliwa kesi CHADEMA inatisha

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema wanachama na viongozi wake 215 wamefunguliwa kesi katika mahakama mbalimbali nchini tangu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

FreemaN.jpg

CHADEMA imesema wanachama hao wamepandishwa kizimbani katika jumla ya kesi 78 huku wengi wao wakinyimwa dhamana na wale waliopatikana na hatia, walipewa adhabu za vifungo bila ya kupewa fursa ya faini.

Kutokana na hali hiyo CHADEMA inatarajia kuandaa orodha itakayoainisha kesi zote za jinai ambazo bado zipo mahakamani pamoja na kuonyesha aina ya mashtaka na vifungo vilivyotolewa, kwa vyombo vya habari na taasisi za ndani na nje ya nchi.

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Profesa Abdallah Safari aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mrejesho wa kikao cha kamati ndogo ya Kamati Kuu ya Chadema kilichokaa Jumanne.

Katika uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 25, 2015 Rais John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliibuka mshindi kwa kupata kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46 ya kura zote halali.

Nafasi ya pili ilishikwa na mgombea wa CHADEMA aliyeungwa mkono na mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa aliyepata kura 6,728,480 sawa na asilimia 39.97.

Prof. Safari alisema mara baada ya Uchaguzi Mkuu huo kumalizika, viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakikamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya kubambikizwa; kwa kisingizio cha uchochezi.

“Hivi sasa umekuwa ni mtindo kwa mahakama kuwakatalia dhamana wanachama wa CHADEMA bila ya sababu za msingi," alisema Prof. Safari.

"Pia imekuwa ni mtindo kuwahukumu vifungo bila kuwapa fursa ya kulipa faini.”

Prof. Safari alisema katika kikao hicho cha kamati kimetoa wito kwa mhimili wa Mahakama kutekeleza wajibu wake kwa weledi uliotukuka; kuhakikisha kuwa haki inatendeka bila kuwapo kwa vitisho kutoka kwa mtu yeyote.

“Majaji wanapaswa kuiga mfano wa uhuru wa Mahakama na weledi wa majaji wa Afrika Kusini, Zimbabwe na Marekani ambao waliweza kutengua amri batili zilizotolewa na marais wa nchi zao,” alisema Prof. Safari.

Aidha, Profesa Safari alisema Kamati Kuu imetoa wito kwa mawakili kuchukua wajibu mkubwa kuisaidia mahakama kutekeleza majukumu yake kwa weledi kwa kuhakikisha haki inatendeka bila woga, vitisho au vishawishi, pamoja na kutokukubali kutishwa na mtu au asasi yoyote katika kuitetea, kuilinda Katiba na sheria za nchi.

Chanzo: Nipashe
 
Kufanya hivyo si itakuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama?? CDM acheni mahakama ziwe huru na ziamue kesi kwa mujibu wa sheria..
 
Dunia inajua kuwa EDO alishinda. Ushindi wa aliyepo ulikuwa ujambazi kama siyo mapinduzi by the way zile komputa mpaka vya LRHC wale m--bwa wamerudisha. Laana inayokula nchi hamuioni? ona matetemeko, ukame, njaa na msababishi wa majanga hataki hata mlie yaani you must die quitely!! Mbado mbado hadi muone pembe za shetani
 
Kufanya hivyo si itakuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama?? CDM acheni mahakama ziwe huru na ziamue kesi kwa mujibu wa sheria..
Unajua sharia au umekurupuka? Katika sharia siyo kuwa tu mahakama ni kutenda haki bali ni kuonekana kweli imetenda haki. Makosa ambayo hayana dhamana (Capital offence) ni pamoja na kosa mauaji (Murder), Uhaini (Traeason), Ugaidi (Terrorism), Ubakaji, uhalifu kwa kutumia silaha na makosa mengine kama yalivyotajwa katika sheria zetu. Sasa unakuta vikosa vidogo vyenye kustaili dhamana mahakama imekuwa ngumu kutoa dhamana. Hicho kitendo wakiambiwa siyo kwamba wanaingilia mahakama. Au tendo la kumfunga mtu kwa kosa dogo wakati adhabu inatoa au fine au kufungwa kisheria mtu anatakiwa kulipa fine na akishindwa ndio anafungwa, lakini mahakama zinakimbilia kufunga bila kutoa mwanya wa kulipia fine. Ukweli ukisemwa siyo kwamba unaingilia mahakama
 
Haujui kuwa majaji na mahakim ni makada wa ccm mfano Jaji Agustino Ramadhani.aliyechukua form kugombea urais 2015
 
Ukiwa na kesi nyingi ndivyo unavyozidisha kuaminika, kwahiyo kila mtu anapambana ili angalau awe na kesi mbili au tatu.
 
Acha unafiki wewe kama wamekosa unataka wasifunguliwe kesi? Acha wapambane na kesi zao

Mbona nyie mnafanya mikutano hamkamatwi au kwa sababu ni Chama Cha Masogange??Acheni ubaguzi Tanzania yetu sote
 
Back
Top Bottom