Orientetion course kwa wateule ni muhimu sana

Nyakarungu

JF-Expert Member
May 1, 2011
472
377
Ndugu zangu huu ni ushauri tu na usije ukatafasriwa vinginevyo.

Ni vyema tukafurahi kwa nchi yetu kusimamiwa na kuwepo kwa nidhamu ya utumishi, lakini tuendelee kubadirika na kujifunza na kuiishi nidhamu kama hiyo tunayoitamani

Kwa sababu tupo tunaoshangilia sana tunapoona mtu anatumbuliwa huku tukisahau na sisi kwenye zamu zetu tunashindwa kuwa na nidhamu ya kutosha, tupo wapiga dili wengi tu, lakini kwa sababu wengine ni wako nje ya mfumo wa serikali kwa maana ya kuwajibishwa na rais,basi tunashangilia tu, zamu yetu inakuja, itafika tu, tunapolilia mabadiliko ya mfumo tusidhani lipo jiwe au ndoo ya kokoto itabaki na hali yake ya mfumo wa awali

Tuanze kuchukua hatua ya kubadilika, tuanze kubeba mfumo mpya wa kujiweka mikono safi ingawa tulizoea njia za mikato, LAKINI tujifunze hali hii mpya wakuu, tuwizi na tuutapeli na tuuongo tudogodogo nato tukipata mbolea tutakuwa majipu makubwa, hivyo tuanze kujifunza maisha mapya wakuu

Kushangilia kutumbuliwa kwa mtu huku na sisi mikono yetu inatapakaa damu ni hasara yetu wenyewe
Ajali kama za mama Kilango zinawatokea hasa viongozi wanadanganywa na wasaidizi wao kisha nao wanaamini bila kutaka kujiridhisha
Lakini pia wasaidizi huwa wana tabia ya kupima kitaaluma wakubwa wao, wakigundua competence yao ni hafifu hutumia mwanya huo kuwadanganya

Mimi nashauri orientation Course kwa nafasi kama hizi ambazo ni za kiutawala za kuteuliwa na rais bila kujali taaluma, mfano Waziri, RC na DC ni muhimu sana kwao, vinginevyo DED, RAS na DAS wanaweza kuwa wasumbufu sana watakapoletewa viongozi hao wenye taaluma tofauti na jukumu walilopewa.

Kwa mfano, waziri wa kilimo yeye amesoma uchumi, lakini anakuwa na katibu mkuu wa wizara hiyo mwenye taaluma ya kilimo, au waziri wa afya kasoma sheria halafu anakutana na katibu mkuu wake ni Dr MD, unategemea kitu gani linapokuja suala la technical kama sio waziri kushangaa shangaa tu,au aliyesoma sanaa anapewa wizara ya biashara anakutana na katiu wake mkuu ni mwanauchumi, kwa hali kama hizi bila kuwapa orientation course watakuwa wazugaji tu kwenye ofsi

Mtemi Nyakarungu.
+255 754 459 572
 
Back
Top Bottom