Nafikiri anachokisema gombe ni
wanafunzi wafanye presentation mfano ana present topic ya Atom mbele ya wanafunzi harafu profesa naye anakua kama mwanafunzi anamsikiliza na wanafunzi wengine pamoja na prof wanamuuliza maswali,hii ina eliminate uwezekano wa kughushi kwa aina yoyote ile.
Pili wanafunzi wanafanya Oral yani mbele ya kabineti la ma prof wasomo ma prof wawili watatu kwenda mbele ,mfano mwanafunzi anaelezea topic mbili tatu ,hii pia inatoa nafasi makini.
Tatu mwanafunzi wakati wa tutorial mfano anakua anatoka mbele anakwenda kukokotoa swali na kuelezea kwanini kakokotoa vile na sivinginevyo hapo pia anapata maksi zake.
Mwisho anaingia mtihani wa kuandika pia anapata maksi zake inapigwa jumla inatafutwa wastani anapata maksi zake.
Hii inamaana mwanfunzi anaanza kukusanya maksi tangu mwanzo wa term hadi mwisho,ni uonezi ama kuwahadaa watu kwa kumu jaji mwanafunzi aliyosoma miezi sita anayaandika kwa saambili ama moja.
Asante sana Mkamap. Kwanza, chuo nilichosoma mimi tulikuwa tunafanya hayo niliyoyaeleza hapo juu. Mwanzoni nilipata shida sana kwa 'oral examinations' lakini baadaye niliona ilinijengea uwezo na niliweza kupata maksi nyingi zaidi hata kuzidi 'essays' na 'written examinations'.
Naamini hata kwa wanafunzi wengine itakuwa vigumu mwanzoni tu kwa vile hawajazoea lakini kwa baadaye ni njia nzuri sana ya kumjengea mwanafunzi uwezo wa kujieleza, kuondoa woga wa kuzungumza au kueleza kitu mbele ya wengine (public speaking) na pia atakuwa na uwezo wa kujieleza kwa kuandika na kuongea.
Tatu, chuo chetu kilikuwa kinawafikiria 'mara mbili' wale waliokuwa wanafaulu sana au kupata maksi za chini. Yaani, kazi zao zilikuwa zinasahihishwa tena na 'external examiners' ili kuhakikisha kuwa mtu anapata maksi ambazo ni zake kweli. Hii iliweza kuwasaidia wanafunzi waliolalamika wameonewa na pia iliweza kubaini wenye tabia ya kuibia.
Nne, waalimu wetu tulikuwa tunawafanyia 'evaluation'. Kama wanafunzi wengi watampa mwalimu fulani alama za chini sana (wakati wa 'evaluation') basi uongozi wa chuo baada ya kuridhika na 'evaluation' hiyo waliweza kusitisha mkataba wa mwalimu huyo kufundisha au waliweza kumshauri kurekebisha namna yake ya ufundishaji. Hali hii iliwafanya waalimu wetu kuwa waangalifu sana na kweli walikuwa wakifanya kazi kwa bidii na maarifa. Mfumo mzima wa utowaji maksi au 'evaluation' ya waalimu, kwa maoni yangu, ulikuwa 'fair'.
Tano, mwanafunzi alikuwa anapewa nafasi ya ku'present' 'paper' yake ya mwisho mbele ya jopo la waalimu (internal & external examiners) na kuulizwa maswali kadhaa kuhusiana na paper yake hiyo. Kila mwalimu aliweka alama zake kwa yale maswali aliyouliza.
Maksi alizopata mwanafunzi pamoja na maksi zingine zote, ziliwekwa pamoja kwa mgawanyo, mfano: Class presentation (5 marks), Class participation (10 marks), assignments (15 marks), tests (20 marks), written examinations
(25 marks) na oral examinations (25 marks). Maksi hizi zote zilitafutiwa wastani na kisha kuchukua, mfano, alama 40% na ile paper ya mwisho alama 60%. Alama hizi zote ndizo zilizomwezesha mwanafunzi kupata diploma au digrii ya kiwango fulani.
Haya niliyojifunza naona yote au baadhi yake kutegemea na mahitaji yetu yanaweza kusaidia, kama yatafuatwa, kuboresha elimu yetu kwa 'levels' zote hapa kwetu Tanzania. Mimi naamini Watanzania wakifundishwa vizuri watafanikiwa kabisa na kwa hiyo hakuna cha kusingizia lugha au nini. Tatizo ni moja tu mfumo wa ufundishaji ni mbaya, tuna waalimu ambao hawana maandilizi mazuri na hawana motisha katika kazi yao.