Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,194
- 297
Ninachosema mimi ni kuboresha elimu yetu kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu. Na njia niliyoipendekeza inamsaidia mwanafunzi kujenga uwezo wa kujifunza, kuelezea alichojifunza kwa kuandika na kuongea. Kwa ujumla ni njia nzuri zaidi ya kumjengea mwanafunzi 'learning skills' - uwezo zaidi.
Nilisema mwanafunzi anapimwa kuanzia kushiriki kwake darasani, 'class presentation', 'written assignments', 'tests', 'written exams' na 'oral exams'. Vyote hivi vitamsaidia mwanafunzi kuongeza maarifa kwa kujenga uwezo wa kujieleza kwa maandishi na kuongea.
Wanafunzi wengi na hata watu wengine kwa kukosa nafasi ya kujenga uwezo wa namna hiyo wanashindwa kujadili hoja kikamilifu na ndiyo maana hata kama mtu anajua kitu fulani anashindwa kukijadili au kuwafanya wengine wakielewe vizuri. Ndiyo maana baadhi ya watu hawajui kujadili hoja. Wanajua kusema na wanategemea anayelezwa 'kumeza' kila kitu na akiulizwa anachukia.
Mkuu Magobe,
Nafikiri unachoonglea ni sawa kabisa kama unashauri kuwa isiwe ni mtihani tu bali iwe ni ushiriki wa ujumla kwa wanafunzi katika mijadala darasani, debate clubs n.k. ikiwa ni sehemu ya corse work yao. Kwa hilo nakubaliana na wewe.
Lakini kama hatutakuwa na waalimu walio na elimu nzuri, hatutaweza kuwa na wanafunzi walio na elimu bora likewise. Pia mfumo mzuri wa uhakiki wa waalimu na ufundishaji unahitajika. Mwalimu angepaswa kupimwa kulingana na kiwango cha kufaulisha wanafunzi, badala ya kuwa na waalimu wenye uhakika wa mishahara yao bila kujali ufaulu wa wanafunzi wake.