Oral exminations at college/university level

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
5,485
3,740
We often hear of people complaining of poor quality of education at college/university level in Tanzania. There are many factors contributing to this problem.

One of them is forging academic certificates. So, we get students joining colleges/universities without merit and some continue cheating throughout their college/university level.

One way of addressing this problem is to introduce oral examinations so that students are evaluted not only through written work but also oral examinations. This could help reduce irregularities at exams since students' performance will be evaluated in written and oral work.

What are your views on this?
 
Ni kweli kabisa mheshimiwa Oral ndio mwarobaini wa yote.

Mfano kwenye tutorial ndio mwanafunzi anafaa afanye writen exam. akipita hilo somo kwa tutor wake anafaa apambane na Oral ktk somo hilohilo upande wa lecture.
Hii itapunguza watu kukakilili ili wapite mtihani maana Oral professa anamufahamu mwanafunzi kaelewa ama kakalili.
 
Mkamap,asante. In fact, vyuo vingine maksi hutolewa katika haya yafuatavyo: kuna 'class participation', kuna 'assignments', kuna 'class presentation', kuna 'essays', kuna 'tests', kuna 'written examinations', kuna 'oral examinations' na kuna 'general evaluation' kulingana na 'performance' ya mwanafunzi.

Katika hayo yote mwanafunzi hawezi kuibia au ku'forge' cheti kwani atafahamika tu. Mimi nilisoma katika mojawapo ya vyuo hivyo. Na ninajivunia mwanga na elimu niliyoipata.

Ningetaka hata kwetu tuanzishe utaratibu huu na nina imani kwa fufanya hivyo tutaweza kuinua elimu nchini.

Kwa kweli ni aibu kubwa kuwa na wajanja wengi wanaoweza kujiita 'Dr, Prof, etc' bila kuelemika. Kukithiri kwa utapeli nchini ni matokeo ya elimu kuwa duni. Yaani, watu wanasoma lakini hawaelimiki na kwa vile hawajaelimika ni rahisi kujiingiza katika utapeli na ufisadi.

Aliyeelimika anaitumia elimu yake vizuri - kwa faida yake na ya watu wengine.

Elimu lazima imkomboe mwanadamu na siyo kumwingiza kwenye matatizo, umaskini wa kukithiri na hatimaye kumwangamiza kabisa.

'Education should not domesticate but liberate people' (Paul Freire).
 
Hata mimi naunga mkonao hoja hii. Ila jamani pale UD watu wanabebana sana hadi kwenye sponsorship za masters zinazotolewa na chuo, mfano Misanya Bingi yule alokuwa mtanagazaaji wa redio one, jamaa ni kilaza sana lakini alibebwa kishkaji eti hadi akapewa sponsorship ya kusoma masters ya sociology pale na wakati mtu aliyestahili akimwagwa. Unajua akaanza kuwa seminar leader hata kabla hajamaliza masters kama ilivyo kawaida pale ndo ilikuwa vituko kwaani hawezi ku argue wala kuwaambia wanafunzi what is wrong and what is right, mwisho akabaki kila kitu kinachokuwa presented yeye anasema tu very good sasa hii ni hatari ndo maana tunakuwa na watu incopetent, ushkaji umezidi.
 
Kamtu, asante kwa maoni yako. Nasikia hata 'assignments' 'varsity' watu wanafanyiwa. Kama mwanafunzi wa Chuo Kikuu anafanyiwa hata 'assignments', je, kwenye 'test' au 'examination' itakuwaje? Si anaweza kukata roho kama haibii?

Zamani tulikuwa tunasikia 'Nigeria imekithiri kwa utapeli'. Sasa Tanzania nayo inaanza kuingia kwenye utapeli wa aina hiyo tena kwa 'speed' kali. Yaani, utaona watu wamejaa ujanjaujanja wa kipuuzi sana na wanaona kufanya hivyo ndiyo kuelevuka. Aibu gani hiyo!
 
Mkamap,asante. In fact, vyuo vingine maksi hutolewa katika haya yafuatavyo: kuna 'class participation', kuna 'assignments', kuna 'class presentation', kuna 'essays', kuna 'tests', kuna 'written examinations', kuna 'oral examinations' na kuna 'general evaluation' kulingana na 'performance' ya mwanafunzi.

Katika hayo yote mwanafunzi hawezi kuibia au ku'forge' cheti kwani atafahamika tu. Mimi nilisoma katika mojawapo ya vyuo hivyo. Na ninajivunia mwanga na elimu niliyoipata.

Ningetaka hata kwetu tuanzishe utaratibu huu na nina imani kwa fufanya hivyo tutaweza kuinua elimu nchini.

Kwa kweli ni aibu kubwa kuwa na wajanja wengi wanaoweza kujiita 'Dr, Prof, etc' bila kuelemika. Kukithiri kwa utapeli nchini ni matokeo ya elimu kuwa duni. Yaani, watu wanasoma lakini hawaelimiki na kwa vile hawajaelimika ni rahisi kujiingiza katika utapeli na ufisadi.

Aliyeelimika anaitumia elimu yake vizuri - kwa faida yake na ya watu wengine.

Elimu lazima imkomboe mwanadamu na siyo kumwingiza kwenye matatizo, umaskini wa kukithiri na hatimaye kumwangamiza kabisa.

'Education should not domesticate but liberate people' (Paul Freire).

Mkuu Heshima yako
Mie pia na mtazamo kama wako na nimejaribu pia kushuhudia wezentu wanavyoendeleza mambo yao na kuendelea Na nikajaribu kubainisha kuhusu Elimu ya Vyuo vyetu ilivyo tofauti na vyuo vilivyomakini vitoavyo elimu bora ma CONSECUTIVES wa UDSM wakanipinga wakasema vyuo vikuu ni UNIVERSE wakapigiana makofi na elimu yetu inaendelea kua duni.

Nikaandika mfumo wetu wa Elimu unahitaji marekebisho watu wakaa kimya wakapuuzia .

Nikaandika kuishutumu UDSM na nikaifungamanisha na kudoda kwa uchumi wetu ma CONSECUTIVE kama kawaida wakapinga wachache tukakubaliana ktk hilo rejea topic hiyo.

Mwisho nami nasisitiza kua UFISADI/RUSHWA/mikataba mibovu Ni matokeo yakutukua na wasomi.Wasomi ni wale walioelimika wakawa waelewa Wengi tunaowaita wasomi ni wa kwenye makaratasi tu.HAkika msomi hawezi kuwa fisadi ,msomi hawezi kuingia mikataba ya kuiuza jamii yake katu.

Huku kutokua na wasomi ndiko kunakopelekea uchumi wetu kudumaa ilihiali tunakilasababu yakuwa matajiri.

Watu utakuta wanapiga kelele ooh CCM OOh CHADEMA,ooh CUF hakika hivi vyama havina ubavu wowote wakukuletea uchumi bora ,vyama ni kama moshi ELIMU ni MOTO ,sasa basi ukitaka kuzima moshi hunabudi kuzima kwanza motto,lakini ukikuta watu wanahangaika kuzuia moshi bila kuzima moto jua watu hao hawajaelimika.

Uchumi wetu hauleweki/mafisadi wamezidi/mikataba ya ulaghai imejaa hii ni kutokana hawajaelimika.Na njia ulizopendekeza ni sahihi kabisa kama chazo cha mchkato wa kurudisha Elimu iliyosahihi nahatimaye UCHUMI BORA. Ma consecutive kubalini kunamatatizo makubwa ktk elimu ya juu ya tz na kubalini mfumo uliopo sasa hauna tija unahitaji mabadiriko ya haraka.
 
Ndugu yangu kama ulikuwa unategemea jibu au mchango wewote ule kuhusu mambo yanayohitaji kutumia akili basi humu ktk jf utakuwa mkiwa siku zote... humu ukitaka upate washabiki na wachangiaji hoja wengi basi anzisha hoja kama "afrika imelaaniwa", "hii inatokea afrika tuu", "waafrika wabinafsi", "waafrika hawana akili ukilinganisha na watu wengine" n.k na ukitaka wakushabikie hasa basi uongezee na kuandika kwa lugha ya KIINGEREZA basi hapo mtajibishana mpka kukuche lkni kama unaandika mambo yenye AKILI na ya MAANA kama hayo uliyoorodhesha hapo juu hupati mtu na ndio maana unaona hii hoja imechangiwa mara tano tuu... hii inaonyesha ni jinsi gani uwezo wa kiakili wa watu wengi humu ulivyokuwa mdogo, kwa mfano mimi huwaga nawauliza humu kila siku kuna haja ya mtu kuandika hoja yeyote ile kiingereza wakati sisi wote humu lugha yetu ya kwanza ni KISWAHILI? sipati jibu...
sasa kurudi ktk hoja yako ninakubaliana na wewe 100% kuhusu chimbuko la matatizo yetu yoote yanayotukabili nchini mwetu nayo ni UBORA WA ELIMU YETU na hiyo inaanzia chini kabisa na sio chuo kikuu tuu, ni bado hatujaweza kuweka msingi imara ktk elimu yetu ya chini kwa maana nyingine mfumo wetu hautuandaii vyema kuweza "kuelimika" kutumia msemo wako, vyema na kuweza kufanikiwa na masomo ya chuo kikuu... kwa mfano ktk maisha yangu yoote nchini mwetu sijawahi kusikia hata siku moja serikali ikiongelea urekebishwaji na uboresishwaji wa mitaala ya shule za msingi sekondari, mfumo uliopo ndio ule ule alioacha mkoloni... kuna mambo mengi hapa kwa mfano ukweli ni kwamba ktk nchi yetu lugha ambayo inatumiwa na kueleweka bila matatizo yeyote na watu wetu ni KISWAHILI sasa ni kwa nini mtoto afundishwe masomo yote kiingereza?? mimi nikichukulia uzoefu wangu shule ya msingi tulifundishwa kila kitu kiswahili, baada ya hapo nikabahatika kusoma tabora boys ambayo ilikua inajulikana kama shule maalumu kwa watu wenye vipaji maalaumu, na kule kila kitu kikabadilika ghafla na kuwa kiingereza na ukweli ni kwamba mimi pamoja na wenzangu tulipata shida sana na tukawa hatuelewi mwalimu anachosema kwa hiyo tukawa tuna buruzwa tuu na miaka inakwenda.. swali langu ni kwamba Je ni kwa nini mtu anashindwa kuliona hilo?? hauwezi ukafanikiwa ktk masomo yako vizuri kama hata lugha unayofundishiwa hauilewi vizuri...

Na hii inajionyesha ktk mambo mengi nchini mwetu sasa ukija kwenye mikataba ni kwa nini mkataba uandikwe kiingereza? kwa nini usitafsiriwe? Je hauoni kwamba kama mkataba ungeandikwa kwa lugha yetu yule aneusoma labda ingeongeza uelevu wake na kisha labda ingesaidia kiasi fulani?
kwa hiyo mambo ni mengi na yote chanzo chake ni kimoja nacho ni kuutambua na kuukubali UKWELI nakisha baada ya hapo kuanza kuufanyia kazi, na mimi nafikiri kwanza kabisa tukubali kwamba sisi kiingereza sio lugha yetu hivyo basi haiwezekani kama mtu amezaliwa na kukulia tz kuweza kukimudu vizuri kiingereza kiasi cha kuweza kuelewa vizuri kinachoongelewa darasani au kwenye vitabu (mtanzania wa kawaida ni yule anaeshi magomeni au sinza au temeke)...
na baada hapo basi mimi nina imani mambo yataanza kwenda vizuri, napenda ukumbuke pia kwamba nchi ni ya pekee ktk mengi ktk dunia hii, sisi ni wa pekee, matatizo makubwa ambayo jamii zingine zinakabiliana nayo sisis hatuna.. hata nchi zilizoendelea mimi nafikiri pia wbado wana matatizo makubwa ya kutatua kuliko sisi.. kwa hiyo tunaweza kutatua matatizo yetu haraka sana ikama watu kama wewe na mimi na baadhi ya wengine hatutachoka kufanya kile ambacho tumejaliwa kuwa nacho nacho uwezo wa kuuona ukweli....
 
Mawazo yako mazuri sana
Lakini hilo tatizo la lugha tuliliona tukalijadili ktk maada ya "udsm ndio chazo cha mfabao wa elimu" tukakubaliana wachache tuandike vitabu vya kiswahili tukakaribisha wadau watusaidie kutafasiri maneno ya kiswahili lakini badala yake hawaonekani tembelea ama bofya hapa www.elimupedia.com/index.php?...ti_ya_Hisabati
http://www.elimupedia.com/index.php?...ti_ya_Hisabati

Mpango upo taratibu kwa sababu watanzania hawajui wanachotaka.
 
kuhusu huo mjadala naona ulinipita kwa bahati mbaya na sikuweza kupata nafasi ya kuujadil, nimejaribu kufungua hizo websites lkni naona hazikubali Je unaweza kusahihisha hilo, asante..
 
Mkuu samahani naona saizi hizi hazifungui contents zake Na muasisi wake ni Binmaryam ama haipatikani kwa mda ama imekitisha tamaa kutokana nakua hakuna mchango watu wanachangia.lakini jaribu tena kuitembelea baadae
 
...ninakubaliana na wewe 100% kuhusu chimbuko la matatizo yetu yote yanayotukabili nchini mwetu nayo ni UBORA WA ELIMU YETU na hiyo inaanzia chini kabisa na sio chuo kikuu tu, ni bado hatujaweza kuweka msingi imara ktk elimu yetu ya chini kwa maana nyingine mfumo wetu hautuandai vyema kuweza "kuelimika"...kwa mfano ktk maisha yangu yoote nchini mwetu sijawahi kusikia hata siku moja serikali ikiongelea urekebishwaji na uboresishwaji wa mitaala ya shule za msingi sekondari, mfumo uliopo ndio ule ule alioacha mkoloni... kuna mambo mengi hapa kwa mfano ukweli ni kwamba ktk nchi yetu lugha ambayo inatumiwa na kueleweka bila matatizo yeyote na watu wetu ni KISWAHILI sasa ni kwa nini mtoto afundishwe masomo yote kiingereza?? mimi nikichukulia uzoefu wangu shule ya msingi tulifundishwa kila kitu kiswahili, baada ya hapo nikabahatika kusoma tabora boys ambayo ilikua inajulikana kama shule maalumu kwa watu wenye vipaji maalaumu, na kule kila kitu kikabadilika ghafla na kuwa kiingereza na ukweli ni kwamba mimi pamoja na wenzangu tulipata shida sana na tukawa hatuelewi mwalimu anachosema kwa hiyo tukawa tuna buruzwa tuu na miaka inakwenda.. swali langu ni kwamba Je ni kwa nini mtu anashindwa kuliona hilo?? hauwezi ukafanikiwa ktk masomo yako vizuri kama hata lugha unayofundishiwa hauilewi vizuri... Na hii inajionyesha ktk mambo mengi nchini mwetu sasa ukija kwenye mikataba ni kwa nini mkataba uandikwe kiingereza? kwa nini usitafsiriwe? Je hauoni kwamba kama mkataba ungeandikwa kwa lugha yetu yule aneusoma labda ingeongeza uelevu wake na kisha labda ingesaidia kiasi fulani? Kwa hiyo mambo ni mengi na yote chanzo chake ni kimoja nacho ni kuutambua na kuukubali UKWELI nakisha baada ya hapo kuanza kuufanyia kazi, na mimi nafikiri kwanza kabisa tukubali kwamba sisi kiingereza sio lugha yetu hivyo basi haiwezekani kama mtu amezaliwa na kukulia Tz kuweza kukimudu vizuri Kiingereza kiasi cha kuweza kuelewa vizuri kinachoongelewa darasani au kwenye vitabu (mtanzania wa kawaida ni yule anaeshi magomeni au sinza au temeke)...

Kimsingi, nakubaliana na wewe kwa hoja ulizozijadili. Kwanza, ni kweli elimu yetu ina matatizo kuanzia elimu ya msingi, sekondari hadi chuo kikuu. Mwalimu fulani alikuwa akisema elimu ya msingi ina matatizo sana na yanaletwa na uongozi mbaya ngazi za juu. Alisema waalimu wanapewa malengo, wakiambiwa 'ushindi ufikie asilimia fulani'.

Kwa hiyo, wanafanya juu-chini wanafunzi wao wawe karibu na ushindi huo ili kulinda kibarua chao. Hiyo inatoa mwanya wa rushwa (kuibia mitihani na kununua vyeti bandia). Alisema pia yeye alishapata matatizo kwa kuwa na msimamo wa kuwakatalia waalimu wenzake alipoambiwa awaachie wanafunzi wajaribu bahati yao.

Kwa hilo, alilaumiwa na waalimu na wanafunzi kuwa haitakii shule yake ushindi mzuri. Hivyo, aliwekwa kwenye listi ya kufukuzwa na akaamua aondoke pale (shule ya binafsi) na kuajiriwa shule ya serikali. Alisema pia hata huko anakumbana na matatizo yaleyale.

Pili, lugha siyo tatizo - tatizo ni waalimu kukosa motisha au kuwa na waalimu wasio na uwezo mkubwa na utaalamu wa kufundisha. Baadhi ya waalimu hawataki kuulizwa maswali darasani. Wanataka wanafunzi waelewe tu hata kama hawajafundishwa vizuri kiasi cha kuelewa.

Kuna Watanzania wanaofahamu lugha ngeni vizuri sana: Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, Kichina, Kiarabu... na hata lugha zingine za Afrika. Mimi naamini kuwa mwanafunzi akifundishwa vizuri lugha yoyote ataelewa tu. Tatizo kwetu hapa ni kwamba wanafunzi wanafundishwa kukariri majibu ya mitihani na siyo kukuza ubunifu, uwezo wa kufikiri na kuhoji vitu na kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya jamii au mazingira yanayowazunguka. Elimu ya namna hii haijengi bali inabomoa tu.

Vilevile elimu lazima ijenge dhamiri njema na maadili mema (informed conscience & moral standing) ili kwamba mwanafunzi anapohitimu masomo yake awe pia na uwezo kwa kutofautisha chema na kibaya na siyo kuona hivyo viwili vikifanana. Elimu inayokuza ubinafsi haiwezi kamwe kuwa elimu bora na haijenge dhamiri/maadili mema.

Tuondokane na elimu inayotufanya tuendelee kula mapanki, kuua kundi fulani la watu na kutumia baadhi ya viungo vyao au kuwaingilia watoto wetu kinyume na maumbile ili tufanikiwe kibiashara, kuharibu miundo mbinu ili tufanye biashara ya vyuma chakavu, kuingiza bidhaa feki, kuendela kuvaa 'Kafa Ulaya' na kufuja mali ya umma.

Tatu, hata lugha yetu ya Kiswahili hatuijui vizuri. Tunaongea Kiswahili kibaya (siyo sanifu) kama tusivyoweza Kiingereza (sanifu). Ndiyo maana mimi naamini tatizo siyo lugha ni ubora wa elimu nzima ndio tatizo. Hata lugha zetu za kiasili hatuzijui sawasawa. Na tukishaondoa Kiingereza (tunachosingizia), hata baadaye tutaona Kiswahili kinatushinda na tutaanza kujifunza kwa lugha zetu za asili.

Na baadaye tutaona pia hatuwezi na tutarudia lugha za kigeni. Kuondokana na tatizo hili, kwanza tuwe na waalimu bora (waliobobea vizuri katika masomo wanayofundisha na wapewe nafasi za kujiendeleza) na wapewe motisha.

Nne, baada ya kuwa na soko huria, serikali yetu imeshindwa kabisa kusimamia vizuri vipaumbele: elimu, afya, usafiri na huduma nyingine muhimu. Kwa upande wa elimu, tunaona kuna vitabu vingi sana ambavyo havijahakikiwa vizuri (yaani, vina makosa mengi ya kitaaluma na lugha) likini vitabu hivyo vimeruhusiwa kutumika shule za msingi na sekondari. Elimu imekuwa mradi wa watu fulani wajanja na badala ya kuipanua na kuiboresha wanaendelea kuiangamiza. Watanzania, tuamke!
 
When you call for oral exams, what level do you have in mind for its implementation?
MUCHS has oral exams, though I do not know of recent if it is still in practice or not.
 
I meant at college/university level and I had in mind apart from that, class participation, class presentation, essays, tests, written examinations and overall evaluation of students (encouraging students in areas they show talents or advising them to improve in areas they haven't grasped much.

This, of course, has to go hand in hand with addressing the teachers' woes. I'm sure if we try to implement what we can we will certainly make some improvements. If we give up and think we have no resources (and, therefore, we need to apply for funds - which we end up misusing them, we'll keep on retrogressing.
 
Magobe, You have all good intentions, I only wish wishes were horses. I dearly call for the same and I share similar sentiments. I am at the same time weary and skeptical of the system that has been in place for a long time now.
I think oral exams work better at a higher level than the first degree and would be more efficient there as a means of evaluation and measurement. Undergraduate degree oral exams would be a disaster for now since numbers, practices and policies are not in favor of having oral exams implemented.

However, your point of encouraging students to participate is one that I think is very important in the case of undergrads. The only hurdle we have is the over-reliance on past materials "madesa" and reluctance of lecturers to look for new information. Such practices encourage production of low level knowledge graduates with outdated information, who also lack motivation in learning new information.
 
I would only support the idea under one condition: that it would, at one time, yield expected results. But with what I know of Tanzanians, people will still come up with forgeries of their persons!
The system is so rotten in this country, that you actually have difficult time persuading people there is ever a possibility of life with no frauds and cheating.
Remember we, Tanzanians, spend more resources in frauds than we do in right things.
 
Yes, Jim you're right. But I know not all Tanzanians are corrupt and may be we could start from there. It will take time but certainly in the long run it will make a difference.

We have structural corruption and so nearly every part of the country smells corruption. But those who are not corrupt can influence their family members and close friends and if this continues, we will eventually change something.
 
This reminds me when I sent some few cents to a relative home. The lady was really skeptical about whether she would get the money. She even asked if she has to borrow some money from a friend before she goes to the post office just incase if they would want something in return.

I told her to go empty handed but with proper ID, she got the money and still does not believe its possible. She thinks it was just plain luck.

This is to say, such people who do not know that there is no need to pay up for what you rightfully require is part of the brunt that such practices are going on today. If people just refuse to take part i some forms of corruption that could be a staring point.

There are a lot of brochures being distributed to educate people about corruption, but my dear friend its useless since the same people take it as received knowledge that you have to bribe regardless of whether you are told not to.

People long time ago would come to UDSM with offers of 3 - 4 Million just to get admission and yet their children have distinctions as good as DIV 1. I was so surprised at this poor man who choses to ignore that his daughter is eligible and still wants to bribe his way. No wonder such people are taken advantage of by some twisted clerics in the admission office during these times. This is an experience way back in 1997. I do not know if such is still in practice.
 
We often hear of people complaining of poor quality of education at college/university level in Tanzania. There are many factors contributing to this problem.

One of them is forging academic certificates. So, we get students joining colleges/universities without merit and some continue cheating throughout their college/university level.

One way of addressing this problem is to introduce oral examinations so that students are evaluted not only through written work but also oral examinations. This could help reduce irregularities at exams since students' performance will be evaluated in written and oral work.

What are your views on this?

Mkuu Magobe,

Nafikiri nitakuwa peke yangu kukataa hili wazo lako maana kiukweli halitasaidia zaidi ya kuwaonea wachache watakaokuwa wameamka vibaya siku ya intaviyuu.

1. Kuamua ubora wa mwanafunzi aliyesoma miaka zaidi ya 13 kwa intaviyuu ya dakika 15 sidhani kama ni uamuzi bora na wa haki.

2. Mwanafunzi yeyote ambaye amefoji kuingia chuo, kama hamnazo, semesta moja tu inamtosha kufungasha virago. Lakini kama kafoji na zimo, ni vema tukawa nao wengi wa aina hiyo maana watasaidia nchi kwa kuongeza wasomi wenye maajina ya daladala.

4. Kinachotakiwa kwenye vyuo vyetu ni kuongeza passing mark ili wanaomaliza wawe wasomi kwelikweli na sio wabangaizaji. Vipimo viwe kama ifuatavyo; A=100-95, B=94-91, C=90-85, D=84-80. Chini ya hapo iwe ni fail.

5. Kila siku wanafunzi wote wawe wanapewa homework za kutosha ili wasifikirie hata wakati wa kutongozana au kunywa ulabu. Wakishindiliwa kwa kiasi hicho wengi watapata hizi marks bila shida yoyote na watakuwa graduates bora kama China wanavyozalisha wasomi.

Cheers.
 
Ninachosema mimi ni kuboresha elimu yetu kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu. Na njia niliyoipendekeza inamsaidia mwanafunzi kujenga uwezo wa kujifunza, kuelezea alichojifunza kwa kuandika na kuongea. Kwa ujumla ni njia nzuri zaidi ya kumjengea mwanafunzi 'learning skills' - uwezo zaidi.

Nilisema mwanafunzi anapimwa kuanzia kushiriki kwake darasani, 'class presentation', 'written assignments', 'tests', 'written exams' na 'oral exams'. Vyote hivi vitamsaidia mwanafunzi kuongeza maarifa kwa kujenga uwezo wa kujieleza kwa maandishi na kuongea.

Wanafunzi wengi na hata watu wengine kwa kukosa nafasi ya kujenga uwezo wa namna hiyo wanashindwa kujadili hoja kikamilifu na ndiyo maana hata kama mtu anajua kitu fulani anashindwa kukijadili au kuwafanya wengine wakielewe vizuri. Ndiyo maana baadhi ya watu hawajui kujadili hoja. Wanajua kusema na wanategemea anayelezwa 'kumeza' kila kitu na akiulizwa anachukia.
 
Back
Top Bottom