Page 94
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 5,204
- 15,198
Wasalaam Wanabodi.
Kumekuwa na dhana kuwa jicho la marehemu huacha picha ya kitu cha mwisho kabla ya kupoteza fahamu na baadae kukata roho. Dhana hii imekuwa ikiaminiwa sana na wauwaji na kufikia hatua ya kuwatoboa watu macho wakiamini wanapoteza Ushahidi katika jicho la mhusika. Je, hili lina Ukweli?
OPTOGRAPHY ni nini?
Ni mchakato wa kuangalia 'optogram', picha iliyopo katika sehemu ya 'retina' katika jicho la kiumbe.
Baada ya kuzuka kwa habari hizo na kuenea kwa kasi katika karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20, ilimlazimu Wilhelm Kuhne, mwanafiziolojia mwenye asili ya Kijerumani kulifanyia kazi utafiti na kutoa majibu kama kuna uwezekano wa hayo yasemwayo.
Kuhne alifanya utafiti mwingi kwa kutumia Wanyama mbalimbali na baadae Sungura Albino ndiye aliyetoa majibu yenye kuridhisha. Kuna hatua alizifuata (sitaweza kuzielezea hapa) na kweli ilitoka picha yenye mfanano wa kile kilichokuwepo kabla ya Sungura kuuwawa.
Baada ya Kuhne kufanikiwa katika wanyama, alikuwa na Shauku sana kujaribu kama uwezekano huo upo kwa binadamu. Mwaka 1880, Kuhne aliendelea na utafiti wake kwa kutumia jicho la
Gustav Reif aliyehukumiwa kifo cha kuchinjwa kwa njia maarufu sana "Guillotine" baada ya kuwauwa watoto wake. Baadae macho yake yalitolewa na kuwasilishwa kwa Kuhne aliyefanya uchunguzi wake na baadae kuchora picha ambayo hata hivyo hakikuendana na chochote kilichokuwepo wakati wa kukatwa kwake sshingo.
Optography kama njia ya Uchunguzi wa Mauaji.
Baada ya Kuhne kufanikiwa katika tafiti yake haswa kwa Wanyama kama vyura na Sungura, Polisi maeneo mmbalimbali walianza kutumia macho ya marehemu (aliyeuwawa) kama moja ya njia za kufanikiwa kumpata muuwaji.
Mwaka 1888, polisi nchini Uingereza aliitumia njia hiyo kama moja ya hatua za kumpata aliyehisiwa muuwaji. Hata hivyo haikuleta majibu
Dr Ayres, mmoja kati ya wataalamu waliomsaidia sana Kuhne, aliikosoa kama njia inayoweza kuleta majibu ya kuridhisha katika kupata picha ya mauaji. Alisema alirudia kufanya utafiti na kupata picha za Optogram lakini hazikuwa toshelezi katika kupata picha ya muuwaji au mazingira kabla ya kifo chake. Hii ni kuhitimisha kuwa ni kitu kisichowezekana.
Dhana ya Optography nchini Tanzania.
Kumekuwa na mauaji ya kutisha sana na mbaya zaidi wauaji hutoboa macho baada ya kuwauwa. Hufanya hivi wakiamini kuwa watapoteza ushahidi wa wao kujulikana katika uchunguzi.
Naomba tuipuuze sasa hii dhana ya kutoboa marehemu macho baada ya kufanya mauaji.
Kutoboa watu macho huleta tafrani sana na mara nyingine wakati wa kuaga, marehemu hatazamiki kabisa.
Nawaomba wote wale wanaoua, msiwatoboe macho maana hakuna jinsi mtaweza kujulikana kwa macho ya miili hiyo mfu.
Tupeni haki yetu ya kuwapumzisha wenzetu kwa sura angalau za kutazamika kidogo.
Hitimisho.
Nimelazimika kuandika haya baada ya kusikia vifo vingi vya kuuwawa watu na kutobolewa macho. Inauma sana kuuwawa kwa wenzetu lakini inauma zaidi ukisikia wamefanyiwa vitu vya ajabu ikiwa ni pamoja na kutobolewa macho.
Mungu atusaidie.
Nawasilisha.
NB: Sijatoa Somo hili ili kuwasisitiza watu kuua, bali ni kuomba huruma ya kutotobolewa macho ya marehemu baada ya Mauaji.
Nisieleweke vibaya