Shida kubwa ya wasanii WENGI ni kuangalia fursa iko wapi waitumie hata ikiwa kwa Ibilisi wataenda hukohuko kuifuata fursa ndiyo maana wanakosa msimamo wa kusimamia wanachoamini, leo anasema hivi kesho vile, leo anakosoa hiki kesho anakipongeza hichohicho(siongelei mtu hapa naongelea watu), hakuna kitu kibaya kama kujipendekeza kwa wakuu na watawala wa dunia maana utakuwa umechagua kushiriki udhalimu wao, nabii Eliya alishindana na mfalme Ahabu, Yohana mbatizaji wa Yordani alimkosoa mfalme Herode kwa kumuoa mke wa ndugu yake mpaka jambo hilo likafikia Yohana kukatwa kichwa, lakini leo tunaona wanafiki wakubwa wanaojiita 'waimbaji wa Injili na wachungaji' na 'viongozi wa dini' mbalimbali wakijipendekeza kwa viongozi wa kisiasa kwa ajili ya matumbo yao mpaka wameshindwa kukemea maovu yanayofanywa na watawala, ".....Watu wengi hutafuta upendeleo wa mkuu bali hukumu ya kila mtu hutoka kwa BWANA(Mungu)....."-MITHALI 29:26