Opinion: The State of Software Development in Tanzania

Kuna wafanyakazi mabogus wengi sana upande wa serikali linapokuja swala la IT - wanaweza kukubali au kuthamini kitu chochote bila kuquestion kwa sababu tu kimetengenezwa na mzungu! Kuna taasisi moja humu nchini ilitengenezwa mfumo na wazungu, mtanzania mmoja alipoifanyia auditing kwa kujitolea alikuta kuna security vulnerabilities na matatizo mengine mengi ya kimfumo, zaidi ya 100. Cha ajabu bosi aliyewakodi hao wazungu ili apige dili badala ya kuchukua ushauri akamchukia na kumletea visa.
 
Uzi mzuri sana na kwa kuongezea kuna vijana wa chache ambao wanafanya real programming wana design vitu matata , tatizo ni kqamba hata serikali yenyewe haiwapi support.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…