singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetoa msimamo na kusisitiza kwamba operesheni dhidi ya wahamiaji haramu na wageni wanaofanya kazi nchini bila vibali halali, itakuwa endelevu na kugusa maeneo yote, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa nyumbani.
Tunaipongeza wizara hiyo kwa kutekeleza kwa vitendo sheria inayolinda maslahi ya Watanzania. Hakuna ubishi kwamba Tanzania kwa sasa ina wataalamu wengi na wasomi wa kutosha katika maeneo mengi, kiasi cha kuhitaji kupewa kipaumbele cha ajira kwenye maeneo ya taaluma husika, kabla ya wageni.
Ni lazima tukiri pia kuwa yapo maeneo machache yenye wataalamu wachache, hivyo kuhitaji kutoka nje. Lakini pia, zipo taratibu za kuwapata wataalamu hao ambao, hata hivyo, hulazimika kuwafundisha wazawa mambo muhimu kuhusu taaluma hizo na kuwapa uzoefu, ili baada ya muda fulani waweze kusimama wenyewe kuendesha majukumu yaliyokuwa yakitekelezwa na wageni hao.
Wiki iliyopita, Idara ya Uhamiaji iliwatia mbaroni wahamiaji haramu 79 kutoka nchi 15 duniani kwa kosa la kuishi nchini bila vibali huku wakifanyakazi wasizokuwa na taaluma nazo ambazo imeelezwa kuwa zingeweza kufanywa na Watanzania.
Katika zama hizi ambapo karibu kila nchi duniani inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wake, Tanzania ina haki kama nchi nyingine kuimarisha vita dhidi ya watu wanaotunyang’anya haki ya kufanyakazi halali ili kujiingizia kipato.
Operesheni dhidi ya wahamiaji haramu ina umuhimu wa pekee katika nchi yetu kama kweli tunataka kuleta maendeleo na ustawi wa taifa letu. Ni muhimu pia kusisitiza kwamba kila mwananchi mahali alipo anapaswa kushiriki operesheni hii kwa kutoa taarifa sahihi kwa mamlaka husika pindi anapofahamu kuhusu wahamiaji haramu na wanaofanya kazi bila vibali.
Watu hao tuko nao mitaani na wengine tunaishi nao jirani kwenye vitongoji na vijiji vyetu hivyo tusiwaonee aibu bali tuwaripoti mahali panapostahili ili hatua zichukuliwe dhidi yao. Watanzania ni wakarimu, na hilo lilidhihirika tangu enzi za Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika, ambapo ndugu zetu wengi waliokuwa wakiendesha harakati hizo walikaribishwa nchini kuziendeleza na kisha kurejea makwao baada ya uhuru.
Nchi hizo ni pamoja na Zimbabwe, Msumbiji, Angola na Afrika Kusini. Tulijitahidi kwa kutoa ushirikiano wa kutosha hadi masuala yote ya ukombozi wa Afrika yalipokamilika. Kwa ufupi, Tanzania haina ugomvi na wageni bali inawataka wafuate sheria kuingia nchini na kufanyakazi.
Kwa suala hili, kama ulivyo utamaduni wetu wa kushirikiana kwa upendo huku tukidumisha amani, Watanzania hatuna budi kuhakikisha tunahusika kuhakikisha operesheni hii inafanikiwa huku tukisaidia kuiimarisha.
Kwa kufanya hivyo, tutalinda ajira zetu na kuipeleka nchi kwenye maendeleo yanayotakiwa huku ustawi wa nchi ukishamiri. Lengo letu kwa pamoja liwe kufikia uchumi wa kati. Kama hivyo ndivyo, ni lazima pia tutambue kuwa hatuwezi kuufikia ikiwa tutashindwa kushirikiana na mamlaka zetu kulinda na kutetea haki zetu za msingi ikiwemo ajira.