Operesheni Sangara yaingia Lushoto; kwa Makamba

Slaa na Chadema asijisumbue Tanga, Nichama cha kichaga na kanisa hivyo ndo kinavyoeleweka, Mbowe amejaribu kupiga masambasort na dege lake lakini hakuna mtu alie mjali. Huko Tanga ni CCM na CUF, Chadema ni ukabila na udini.
 
Slaa na Chadema asijisumbue Tanga, Nichama cha kichaga na kanisa hivyo ndo kinavyoeleweka, Mbowe amejaribu kupiga masambasort na dege lake lakini hakuna mtu alie mjali. Huko Tanga ni CCM na CUF, Chadema ni ukabila na udini.

Bull nadhani CHADEMA inakunyima sana usingizi.Ukweli siku zote hata ukiupindisha vipi,utabaki kuwa ukweli tu.Nakubaliana na wewe kwamba Tanga ilikuwa ni CCM na CUF lakini sio sasa.Katika operesheni hii tumepata wanachama wengi from both two mentioned parties na wengine waliokuwa hawana chama.Kama unabisha subiri mwakani uone kwenye ubunge na udiwani.
 

Naomba mnijuze uwepo wa zitto....YUPO?
 


GS
These guys are doing what they have been taught to preach .Wanaimba wimbo ule ule wa udini , ukabila nk ambayo ndiyo nguzo kubwa ya CCM na CUF . Tuangalie udini tuone kwenye CCM na |CUF kama kipimo ni Mbowe kuwa kiongozi then ndiyo uchaga . Chadema ni chama cha Kitaifa kwa kila hali . Turudi CUF na CCM tuone uongozi umekaa vipi na tuanze kujadili kama ni udini ama ukabila .
 
Hivi ile operation Sangara kule kanda ya ziwa imezaa matunda gani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa?

Kwa kelele tulizoletewa hapa, nilikuwa nategemea CHADEMA wawe na asilimia kubwa ya vijiji na mitaa.

Muhimu ni kuwasha moto na kupata viongozi wa maana kule vijijini na wilayani maana hao ndio wanaandaa ushindi. Vinginevyo tutabaki na yale yale chenga twawala japo goli twafungwa.

Itakuwa kazi kubwa sana CHADEMA kushinda kiti cha ubunge huko Tanga. Inabidi nguvu na mikakati ya ziada.
 

watu wametumia kika mbinu kushinda kwa haki lakini ilikuwa ndoto kubwa . Je kabla swali lako uliona aina na namna uchaguzi ulivyo andaliwa ama wewe unatehgemea kushinda bila kuangalia uhalisia wa mchezo ?
 
Huko Tanaga Chadema washau, CUF imeisambaratisha CCM kwenye chaguzi za serikali za mitaa, Mbunge wa o wa CCM sasa hakubaliki. CUF wamejiimarisha ni nitishio kubwa kwa CCM

Chadema kinaeleweka kama chama cha:
1) One man show- Mbowe ni actor ndie anae run show
2) Uchaga
3) Chama cha kanisa

Chadema lazima kishafishe image ilikikubalike na wananch, kama mtabaki katika State of denial, hamtofika popote. Guys you have to do samething, sio ku-brush off malalamiko ya wananchi. You have been warned!!
 

Kama kweli CUF wamesimama Tanga is well and good . Chadema hawako kuimaliza CUF bali CCM . We need CUF kuwa mbugeni na kushika madaraka pia .
Sasa tolea ushahidi wa madai yako uliyo yatoa hapo juu mana they make no sense . Kmaa una bisha onyesha

1.Uchaga
2.Kanisa
3.Mbowe being a one man show .

Au ni kwa vile hawajasema lolote kuhusiana na mahakamna ya kadhi .Guys huu ujinga mnao utoa hapa mnalishwa na nani ?
 
 


Kaka unachooliza hapa ni sawa na kusema wanaodai CUF ni chama cha Waislamu wakuletee ushahidi.

Ukabila na udini wa CHADEMA ni propaganda kama ilivyokuwa kwa CUF. Hata hivyo CHADEMA kama ilivyokuwa CUF kuna makosa ya kistratejia ambayo wamekuwa wakiyafanya ambayo yamerahisisha kazi ya maadui/washindani wao kuhalalisha propaganda hizo dhidi yao.

Sasa badala ya kung'ang'ania ushahidi ni vizuri kuwashauri wao na vilevile CUF kama wahanga wa propaganda hizi kujinasua mtegoni waliko/ wanakojiingiza wenyewe. Hili halitofanikiwa kwa kuendelea kuulizia ushahidi ambao hautaletewa isipokuwa mikakati maalumu ya kuondokana na vulnerabilities zote ambazo zinawapa nafasi wanapropaganda hasi kufanikisha kazi zao dhidi ya CUF, CHADEMA na hata kwa kiasi fulani na CCM pia...
 

Mkulima
Kweli wewe mkulima hasa,tena yule wa kizamani.Hebu fuatilia vizuri takwimu za chaguzi za serikali za mitaa mwaka huu utagundua kuwa CHADEMA imepanda kwa kiwango kikubwa.Unavyosema kwamba ulitegemea CHADEMA wawe na asilimia kubwa sijui unamaanisha nini.Asilimia kubwa ni ngapi?na je ulitaka CHADEMA iongoze kuishinda CCM? please be precise and specific usikurupuke.
Ndugu yangu usipende kufanya assumption katika mambo ya siasa,siasa sio physics or mathematics useme kwamba let X= 5.Siasa inafanywa field.Hakuna chama chenye uhakika wa unbunge kwa hali iliyoko sas ahivi na ndio maana kila chama ama mgombea ni lazima wafanye kazi ya ziada ili vishinde ama washinde.Hata Sitta mwenyewe hajiamini jimboni kwake.
 
 
Unaonaje ukatusaidia wengi wetu hapa kwa kutuletea hizo facts and datas...

Dont worry nitawapa hizo data but not today ngoja nizicompile kwanza halafu nitakuja na thread ya peke yake ya matokeo ya chaguzi za serikali za mitaa kwa upande wa CHADEMA.
 


- Mkulu GS, please! vipi tena mbona huwa unaleta vitu vya uhakika sana what is this? Okay by the time Dr. Slaa amemaliza kumshugulikia Mkamba taifa litakuwa limenufaika na nini huko Lushoto? Wananchi wa Lushoto watanufaika na nini hasa na hii siku moja Dr. Slaa atakayomshugulikia Makamba?

- I mean hizi siasa za majina ya viongozi mtajifunza lini kuachana nazo? After all the Zittos na Wangwe, bado tu mna hizi za majina ya viongozi? Inasikitisha sana, halafu hii ni breaking news! Kuweni na haurma kidogo na taifa wakuu! huu sio wakati wa nani zaidi kati ya Dr. Slaa na Makamba, huu ni wakati wa kuwaelimisha wananchi kuhusu viongozi wanaofaa na wasiofaaa kwa 2010.

Respect.


FMEs!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…