Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
AGIZO la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwaondoa Ombaomba jijini Dar es Salaam lagonga mwamba.
Ombaomba hao kwameonekana barabarani wakiomba kama ilivyokuwa kawaid yao.
Makonda alitoa agizo kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwaondoa Ombaomba wote wanaoomba barabarani ifikapo Aprili 18 mwaka huu.
OPERESHENI hio imegonga mwamba kutokana na kukinzana na baadhi ya mamlaka katika kuwaondoa omba omba hao.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam leo , Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam (CP),Simon Sirro amesema kuwa operesheni ya kuondoa omba omba imeshindikana kutokana na baadhi ya mamlaka kushindwa kuhusishwa.
Amesema kuwa wanaendelea kujipanga kwa kuhusisha mamlaka zote ili kuweza kutekeleza operesheni hiyo kwa ufanisi.
Amesema kuwa kuna omba omba wengine wameweza kuondoka baada ya tangazo kutolewa hivyo waliobaki waondoke kutokana na operesheni itakayoanza hata angalia uso wa mtu.
Source: Michuzi