Mzururaji
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 1,558
- 1,274
Wakat CHADEMA wakiendelea na maandalizi yao ya operation UKUTA ambapo wamepanga kuzunguka nchi nzima kwa kufanya mikutano mimi kwa upande wangu naona sasa hizi ni dalili za jaribio la wazi la mapinduzi kwa serikali inayoongozwa na Mhe, JPM.
Bara la afrika na nchi nyinginezo duniani tulizoea kuona mapinduzi mengi kutokea jeshini ambapo wanajeshi hujikusanya wale wenye uchu wa madaraka halafu hupindua serikali halali iliyowekwa na wananchi na wakiingia madarakani huvua magwada na kuanza kuongoza kiraia kuna mifano ya maraisi wengi ambao mpaka Leo wanaongoza lakini waliingia kwa style hiyo mtu kama Museveni na Kagame hawa ni mifano ya mapinduzi ya kijeshi
Lakini kwa sasa bala la Africa linashuhudia style mpya ya mapinduzi, haya yakiongozwa na vyama vya upinzani, Asasi zisizo za ki Raia. Hapa huitwishwa maandamano yasiyo ya kikomo na mikutano isiyo na mwisho mpaka Lengo la wanasiasa hawa la uchu wa madaraka kutimia
Kwanza; Kwa historia ya hivi karibun mapinduzi mengi kwa nchi za afrika yalifanikiwa kwa kupitia style hii ya maandamano na mikutano isiyo na kikomo ambayo yalianza kutangazwa kwa masikhara hivi lakini jinsi siku zilivyosonga mbele ndivyo yalipozidi kupanda chati mpaka kupelekea kushindwa kuyadhibiti nchi kama Misri chini ya Hosn Mubarak, Morocco, Syria na nchi nyinginezo. Maandamano ya aina hii yamewezekana baada ya maandalizi ya mizaha kama haya yaliotangazwa ya UKUTA
Pili; Nia ya mwanasiasa yeyote ni kukamata dola hapa ndipo utakapoona njia mbalimbali zikitumia ambayo ya mwisho huwa kama hii ya maandamano nchi nzima kwa kukaidi katazo halali kutoka mamlaka halali kabisa la kuzuia maandamano ama mikutano yenye dalili ya uvunjifu wa amani kwa nchi nzima hivyo kupelekea mapinduzi
Baada ya mapinduzi ya aina hii ndipo mlolongo wa uvunjifu wa amani ukiendelea kama mauaji ya raia wasio na hatia pato la taifa kushuka, wizi ubakaji na mambo mengine kama hayo.
Hivyo basi kwa kumshauri Mhe, raisi wahenga walisema mchelea mwana kulia hulia yeye yaan ukicheka na hii mizaha kama ya UKUTA ipo utakimbia hii nchi ukaishi uhamishoni huku ukiwaacha wanasiasa wenye uchu wa kwenda ikulu kwa njia yoyote wakiwa ikulu
CHADEMA ya sasa imekamatwa na watu wa aina hiyo ambapo wamekuwa wakiitafuta ikulu wa miaka mingi sana na kwa gharama kubwa sana hapa ndipo utakapoona juhudi kama fedha ikibidi usaliti wa wao kwa wao na njia nyinginezo ovu hapa ndipo utagundua operation UKUTA ndio njia ya mwisho waliyokuwa wanaisubiri kwa hamu sana kama tiketi ya kuwapeleka ikulu ya Tanzania
Mhe Rais kupitia dola wekeni mikakati imara ili kuweza kudhibiti hali hii mapema sana kabla haileta machafuko na uvunjifu wa aman kwa mzaha zaha mwisho hutumbua usaha na hapa tunasema mzaha mzaha nchi inaweza kutumbukia kwenye machafuko.
Mwisho, Niwashauri viongozi wa CHADEMA wote kwa ujumla kuanzia tawi mpaka taifa kuingia katika operation UKUTA mkiwa na familia zenu yaani baba mama na watoto kwani ninyi ndio mtakaofaidika na baada ya maandamano kabla ya sisi wananchi mnaosema mnatupigania
Pia Mhe, raisi endelea kuboresha maisha ya wananchi wako ili upate uungwaji mkono kutoka kwa wananchi wako wa kawaida kwa ujumla wao wakiweko wafanyakazi wakulima na wafanyabiashara hapa ndo utaona umuhimu wake kama yaliyotokea UTURUKI ambapo wananchi kwenye nia Njema na wakawaida kabisa walijaribu kuzima jaribio la mapinduzi, hawa wananchi walijua fika hii ni kete ya nchi yao kuingia kwenye machafuko.
Kwa sasa acha niishie hapa nikaendelee na jukumu langu la uzururaji huku niendelea kuiombea nchi yangu.