Operation Sangara ya CHADEMA leo yaingia Ulanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Operation Sangara ya CHADEMA leo yaingia Ulanga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtanke, Aug 10, 2012.

 1. M

  Mtanke JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 282
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Operation Sangara pamoja na vuguvugu la mabadiliko leo imeingia Ulanga Mashariki ikitokea Kilombero. Mikutano imefanyika kwenye Kata 8 na Vijiji zaidi ya 24. Kesho itakuwa ni Kata 8 za Ulanga Magharibi na keshokutwa itakuwa ni Kata 4 za Mashariki na 4 za Magharibi.

  Ikikumbukwe Operation ni kwa ajili ya kujenga mtandao wa CHADEMA vijijini na kwenye vitongoji. Hivyo pamoja na Mikutano pia kumekuwa kukifanyika uchaguzi wa Chama kuanzia Vitongoji hadi ngazi ya Kata. Mh. Mponda amelazimika kurudi Jimboni ghafla baada ya kuwasahau Wananchi wake kwa muda mrefu.
  [​IMG]
   

  Attached Files:

 2. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  No retreat no surrender nataka wapige mpaka bagamoyo.....go Dr go go go nothing comes for nothing.....
   
 3. only83

  only83 JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Ama zao ama zetu...wametunyanyasa sana hawa wakoloni weusi. Hakuna kulala mpaka kieleweke. Tulianza na YAWE, tunaendelea na YAWE, tutamaliza na YAWE.
   
 4. M

  Mnyonge Namba1 JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Na hatimaye kijiji chote cha Msoga kitavua gamba na kuvaa gwanda
   
 5. P

  Prince Hope JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 2,167
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Wao wana pesa, Sisi tuna Mungu!
   
 6. M

  Mnyonge Namba1 JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mponda kaja kuvua gamba nini?. Kama ndio, mpeni kadi ila Jimbo 2015 asahau kabisa kulipata.
   
 7. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hongereni Mungu awe nanyi daima
   
 8. maria pia

  maria pia JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 516
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  huku c ndo kwa yule mama kombani?dadadekiiii Dr.piga mpaka kieleweke
   
 9. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2012
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Hii ni ilani kwa chama changu cha mapinduzi, hawa jamaa kwa kuikanyaga Ulanga kwa miguu watayaona mengi, DC mitti na ile issue yake mauaji ya maguba, unyanyaswaji wa wananchi itete na wawindaji, mgogoro wa mashamba, mvutano wa kuhasimiana ndani ya CCM ulanga yote utapata sura mpya, aidha uchaguzi wetu ndani ya chama utaleta sura ya mageuzi ya kichama na kurejesha mshikamano,

  CCM ni lazima iwe ya kwanza kutambua umuhimu wa malinyi kupewa wilaya sasa, na yeyote atakayewania uongozi wa chama anapaswa awe na maono hayo na ayaweke hadharani au la uchaguzi huu utazalisha virusi vya ebola kama CCM wilaya ya sasa itaendelea kuingángánia malinyi isijitenge na mahenge kwa sababu ya ubinafsi wao wa kule mlimani Mahenge...., ni kipindi ambacho CCM tunapaswa kufanya maamuzi magumu kwa faida ya wengi, tuache mafungu yenye manufaa ya kupita tu na kwa wachache, kwanza jamii halafu mimi ndio wimbo ulio bora kwa siasa za sasa.

  CCM ipokee ujio huu wa CHADEMA ulanga analytically kuelekea uchaguzi wa wilaya hii kichama, ccm ianze sasa kujipambanua kisera na muelekeo wenye kujibu kiu ya muda mrefu ya kupata maendeleo ya kweli ulanga west. Sisi tunajua uranium ipo kule kwa bibi kalembwani Ihowanja na Kilosa kwa mpepo ,twafahamu ardhi yetu ni bora kwa kilimo cha kisasa na mpunga ni additional value yetu na huo ndio msingi wetu wa kungángánia songea road, lakini kama ccm haitatamka sasa 2012 kuwa mradi wa uranium uko mpakani mwa ulanga west na namtumbo cdm watasema na kutupiga bao......kwanini tuwe mabubu kwa makausudi tena kwa ubinafsi tuanze leo kusema ukweli na tuwapokee kwa hekima, tujipange na tuwajibu kisera,kimkakati na kwa maendeleo.

  Wito kwa bro. Mponda, wagombea wa CCM wilaya Liguguda, kidaula,nalyoto na yule jamaa wa minepa, wekeni wilaya mpya ya malinyi kama agenda na kete yenu ndani ya CCM na pia 2015 kijimbo na urais....hapo tutaeleweka kuwa tunajali maslahi ya wengi, pia tutajihakikishia kulinda historia ya uhuru wa tanganyika na hivyo kuwa na haki warithi halali wa uhuru,

  Huwezi kuididimiza Malinyi kama unaheshimu harakati za mji ule ktk kuleta uhuru wa nchi hii, Malinyi ni urithi wa historia ya uhuru wa Tanganyika ...siasa za sasa hazitaki unafiki, tuwe wakweli leo kwa salama ya kesho, malinyi ni wilaya mpya ifikapo 2015, nani muwezeshaji hilo la kwenu wanasiasa ccm vs cdm
   
 10. M

  Mnyonge Namba1 JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  FDR.Jr naomba tuwasiliane kupitia kwa aliyekuwa mgombea wenu wa udiwani kata ya Itete Njiwa 2010.
   
Loading...