Openi University wameanza kutoa majina ya waliochaguliwa

Openi University wameanza kutoa majina ya waliochaguliwa

GEMO

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2016
Posts
250
Reaction score
277
Habari wakuu, awali ya yote nawasalimu, natumai mu wazima wa afya.

Kwa wale wote waliotuma maombi ya kujiunga na chuo kikuu huria Tanzania, napenda wafahamu kuwa majina ya waliochaguliwa kujiunga na kozi mbali mbali kwa ngazi tofauti tofauti yameanza kutolewa.
Endelea kutembelea tovuti ya chuo kikuu huria tanzania kupata taarifa mbali mbali zikiwemo zinazohusika na admission.

Trh 24 Aug Open University walitoa majina ya batch one kwa wale waliomba kujiunga na kozi za Post graduate ikiwemo Master na Phd.
Majina yako hapa https://www.out.ac.tz/files/news/2017_2018_DISPLAY_BATCH ONE.pdf

Pia kuna wale wenye mapungufu katika viambatanisho wameelekezwa nini cha kufanya tembelea tovuti utajua kwa kina.

Lengo la kuanzisha uzi huu ni kuwakutanisha wadau wanaotarajia kuanza masomo hivi karibuni na wale wanaoendelea ili tuweze kusaidiana na kushauriana kuhusu masuala ya kitaaluma.Elimu ya chuo kikuu huria ina changamoto zake tofauti na mfumo wa kawaida.

Kupitia uzi huu tunaweza kukutana na kujadiliana kwa ukaribu zaidi, chuo hiki ni kikongwe kina wanafunzi mikoa yote ya Tanzania na nje ya nchi, kwa mfumo wake wa elimu ya masafa ( distance learning) sio rahisi kukutana ana kwa ana.

Lakini kwa kutumia teknolojia tunaweza kufanya discussion, ku share learning materials kama vitabu na articles, kushauriana na kubadilishana uzoefu.

Andiko hili nimewakusudia zaidi waliomba kusoma kozi za post graduate chuo kikuu huria Tz, ninatambua kuwa wapo waliomba kusoma kozi za digrii ya kwanza, wapo pia wanaoendelea na kozi hizi. Wao pia kwa kadri watakavyoona inafaa kutumia uzi huu kukutana wanaweza kuanzisha utaratibu wao kama vile kutumia telegram maana wao ni wengi zaidi.

Nimalizie kwa hii quoatation ya Henry Ford “Coming together is the beginning. Keeping together is progress. Working together is success.”

Wale wote tuliochaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu huria tuje pamoja fahamu ya kuwa umoja na ushirikiano ni muhimu sana utarahisisha elimu hii ya masafa.

Asanteni.
 
Karibu kiongozi, kwa kutumia teknolojia tutashirikiana kutimiza malengo.
 
Nataka niapply masters by thesis in physics
Ni vipi muda umeisha?
 
Muda haujaisha kiongozi
 
Nataka kuapply degree ya sheria Mwaka huu muda bado upo
 
Fuatilia uone kama wanatoa hiyo programme BTW kuna faculty of science ,technology and environmental studies.
Changamoto mojawapo ya kozi za science zinazohitaji practical sio rahisi kutolewa kwa mfumo wa masafa.
 
Zimatolewa bila shida..muda wa practical ukifika kuna sehemu huwa wanapelekwa kufanya
 
Zimatolewa bila shida..muda wa practical ukifika kuna sehemu huwa wanapelekwa kufanya
Sio rahisi kufanya hivyo...Je open wanatoa kozi za medical?
Open wamebase kwenye social science.
 
Kuna dogo nataka asome hapo OUT lakini kuna course mbili zinanichanganya tofauti yake ...BA Sociology and BA social works ....hii mbona kama zinafanana? Kama yupo anayejua kiundani tofauti yake nijue cha kumshauri maana wengi wananipa tofauti za masomo yao lakini ukichunguza ni kama course moja....
 
Mkuu umecheki prospectus?
Yamkini imeeleza tofauti zake.
 
Sio rahisi kufanya hivyo...Je open wanatoa kozi za medical?
Open wamebase kwenye social science.
Soma prospectus yao ujue ni maeneo gani ya science wanatoa...maana naona umebisha tu kumbe hata chuo hukijui
 
Wakuu habr nimeapply open degree ya kwanza na field back wa menipa mpak admission number je hapo nakuwa nimesha chaguliwa au ??
 
Soma prospectus yao ujue ni maeneo gani ya science wanatoa...maana naona umebisha tu kumbe hata chuo hukijui

Haina haja ya kubishana mkuu....comment yangu ya mwanzo nilimshauri mdau afuatilie kwenye faculty of science, technology nd environmental studies.

Niliweka tahadhari kuwa kozi zenye kuhitaji practical zina changamoto zake kuzitoa kwa mfumo wa masafa.

Hasa zile zinazotumia muda mwingi maabara mfano MD/Engineering huwezi subiri mpaka vyuo vingine wawe likizo ndipo Open wapeleke wanafunzi wakajifunze.

Lakini kama kozi haihitaji muda mwingi maabara inaweza kutolewa kwa masafa.

NB : Ni kweli sikijui chuo hiki sina uzoefu kihivyo.
 
Poa mkuu..ila hiyo link haifunguki
 
Hivi degree za open unapata loan kutoka heslb
 
Ndio unaweza pata mkopo....kuzingatia vipaumbele vya serikali na uwezo wa bodi kuhudumia
 
Karibu ujiunge unaruhusiwa kabisa...Lengo ilikuwa ni kwa Post graduate student ila kutokana na uhitaji na umuhimu wa kushauriana na kisidiana mambo mbali mbali tutapanua wigo wa kushirikiana.
 
Back
Top Bottom