FikraPevu
JF-Expert Member
- Jan 2, 2010
- 304
- 236
TANZANIA inakabiliwa na changamoto ya kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi bila kujengewa vyema stadi za kujua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK). Pichani hapo juu ni shule ya msingi Ndonga Wilayani Nyasa mkoani Ruvuma na hapa ni wanafunzi wa darasa la tatu wakisomea mazingira haya, hali hii inachangia utoro na kuongeza idadi ya wajinga nchini.
Changamoto hiyo inasababisha kuwepo kwa ongezeko la wahitimu wa elimu ya msingi wanaohitimu ngazi hiyo ya elimu bila kuwa na stadi za KKK hali inayochangia kuwepo kwa ongezeko la idadi ya wajinga nchini na hivyo nchi kukosa maarifa na kusababisha ongezeko la umasikini miongoni mwa jamii yetu.
Kwa mfano, mwaka 2012, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya, ilitajwa kuwa na wanafunzi zaidi ya 11,000 waliohitimu ngazi ya elimu ya msingi bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu.
Kwa upande wake, taarifa ya Idara ya Elimu ya Watu Wazima wilayani Tunduru, Mkoa wa Ruvuma, inasema asilimia 27 ya watu wazima wilayani humo, sawa na watu 32,333 ya watu wote wa wilaya hiyo wanaokadiriwa kufikia 118,083, walikuwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu mwaka 2011.
Utafiti uliofanywa mwaka huo huo wa 2011 na taasisi moja binafsi nchini katika shule za sekondari Namatuhi na Ndongosi, zilizoko Kata ya Muhukuru, wilayani Songea, Ruvuma, ulionyesha kwamba karibu nusu ya wanafunzi wote wa shule hizo walikuwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu.
Wanafunzi kuendelea kusomea katika vibanda kama hivi Taifa litaendelea kuwa na idadi kubwa ya watu wajinga
Katika tafiti mbalimbali za aina hiyo, imekuwa ikibainishwa kwamba idadi wanafunzi wanaojiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika mikoa mbalimbali nchini, wastani wa wanaojiunga na ngazi hiyo ya elimu bila kuwa na stadi hiyo ya KKK ni kati ya wanafunzi 200 na 400.
Takwimu hizi zimetokana na Taarifa za Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) zilizokusanywa katika mikoa Tanzania Bara katika miaka ya hivi karibuni. Tangu nchi hii ipate Uhuru mwaka 1961, historia inaonyesha kwamba yapo mambo mengi mazuri yaliyofanyika katika utekelezaji wa Sera na Mipango ya Elimu ya Watu Wazima (EWW).
...
Habari zaidi soma=> http://www.fikrapevu.com/ongezeko-la-ujinga-ni-chanzo-cha-taifa-kukosa-maarifa/