Ongezeko la mishahara na posho za Wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ongezeko la mishahara na posho za Wabunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sungi, Jul 5, 2010.

 1. Sungi

  Sungi Senior Member

  #1
  Jul 5, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni week iliyopita ambapo Bunge la Kenya lilipitisha ongezeko la posho za wabunge wao. Watapata mshahara wa Ksh. 1.2 milioni (karibu Tsh 120 milioni) na allowance ya Ksh. 851,000 (karibu Tsh 8 milioni) Mishahara mingine iliyopendekezwa kuongezwa ni ya waziri mkuu kshs. 3,246,000 (Tshs. 3 milioni) kwa mwezi, makamu rais kshs. 2,796,000, speaker wa bunge la kenya kshs. 2,796,000 kwa mwezi. Waziri Mkuu Odinga na wabunge wengine wanaelekea kukataa ongezeko hili kwa sababu si haki kwa wananchi wa Kenya ambao ni maskini.

  Sasa turudi hapa kwetu Tanzania. Ni mara ngapi wabunge wa nchi yetu wamepiga kura kujiongezea mishahara na posho bila hata ya kufikiria wananchi wa majimbo yao ambao ndio waliochagua kwenda kuwawakilisha bungeni? Mimi nadhani wabunge wa Kenya wakiongozwa na waziri mkuu wao kukataa ongezeko hili ni jambo ya kizalendo linatakiwa kuingwa na wabunge wa Jamuhuri la Muungano wa Tanzania.

  Source: Daily Nation
   
 2. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Tatizo liko ktk jinsi nchi hii inavyoendeshwa. Nchi inaendeshwa kwa cartel system. Serikali, Bunge na hata Mahakama wote wanapanga mambo mabaya kabisa ktk mfumo wa nchi na kukubaliana yapite. Ndiyo sababu Bunge letu linapandisha mishahara na Rais anakubaliana na maamuzi hayo kwa sababau hata ngazi za juu serikalini huwa wameshaona faida yao.

  Spika Sitta ni mtu asiyestahili kabisa kuwa spika. Siyo kwa sababu amekuwa akipitisha jambo hili, bali ni kwa sababu amekuwa akishabikia maamuzi ya kuongeza mishara na marupurupu ya wabunge. Last time alisema lazima wabunge waishi vizuri! Of course hakusema juu yamaisha ya wananchi na alishangiliwa na wapiga kura wake, yaani wabunge.

  Nadhani ni mtu ambaye ni big-headed kwa sasa hivi na tuko hatarini kuliko wa-Kenya maana faida ya wa-Kenya ni kwamba kuna makundi yasiyokubaliana na yanapingana.
   
 3. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Nastahajabishwa sana na kusikia au kuendelea kwa wabunge kudai nyongeza ya mishahara mbali na mishahara waliyo nayo kwa sasa, Hili swala bado ni kizungu mkuti kwani wabunge wa kenya bado wanaendelea kudai nyongeza ya mishahara na endapo watapitisha hiyo hoja basi ndio watakuwa wabunge wanao lipwa vyema katika East Africa na Bara la Africa kwa ujumla. na huku ukizingatia hawakatwi kodi na ukizingatia kuna umaskini mkubwa tu.

  Sasa mimi nashidwa waelewa hawa viongozi wetu wao ni kutaka kuneemesha matumbo yao? au wako hapo tulipo waweka kwa maslahi ya Jamii zetu na maendeleo kwa ujumla au?

  Raila Odinga (PM-Kenya) amepingana vibaya na wabunge wanao taka kuwepo na ongezeko la mishahara kwa wabunge na kuwaambia watu wa focus na maendeleo ya jamiii na shughuri zingine za kimaendeleo katika taifa la kenya.

  Nadhani nasi twapaswa jifunza nakutambua uwapo mbunge si kuwa wewe waenda kujineemesha ni kulitumikia Taifa lako kwanza "Country First" na kama hali ndio hii basi kipindi cha ubunge kiwe na kikomo kabisa only 10yrs basi period na kiwe cha mafanikio na ndani ya 5yrs huja perform vyema tunakutoa na kuweka mbunge mwingine.

  Nchi nayo iamini sana katika EAC ni Rwanda huko najua fika ndiko kuna uwajibikaji wa viongozi ukicheza tu nje Kagame anasimamia hilo sasa wengine siju wanasimamia hayo au nao ni wao kwanza na familia zao.

  Wajua Kiongozi ni lazima usifike na wananchi wako ndani ya nchi yako then nchi za jirani na mataifa mengine ndiyo yakusifie lakini wananchi wako wanung'unike kwa unayo yafanya bado nawe ujiite ni kiongozi? haifai

  Mfn mdogo tu wa Mbunge John Pombe Magufuli ni mmoja ya wabunge wanaokubalika kwa asilimia kubwa sana ndani ya nchi hii TZ katika uchapakazi..

  Sijui wenzangu wana JF mwasemaje karibuni kwa maoni yenu.
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Tarakimu za Tanzania Shillings zimekosewa hivyo zitapotesha wasomaji wasiojua kukokotoa thamani ya pesa ya kigeni kuwa kwenye shillingi ya kitanzania. Ni vizuri mleta mada akarekebisha hizo tarakimu.
   
 5. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Nilihisi ni tatizo dogo kuliko mada yenyewe.

  BTW, Kwani thamani ya pesa yetu inafahamika? leo hivi kesho vile. Si uliona mahesabu ya mkuu wa nchi akilaani TUCTA?

  Mada yetu ni ulafi wa wabunge wetu, wansiasa wetu na wakuu ktk serikali. Hatufiki kokote hata kama raisi ataomba kuliko Matonya.
   
Loading...