Ni kweli ugumba ulikuwepo tangu zamani lakini sasa hivi kuna ongezeko kwa wote wanawake na wanaume. Matatizo ya low sperm count yamekuwa mengi kuliko ilivyokuwa miaka ya huko nyuma. Kwa wanawake matatizo ya mauvimbe, PID, kuziba mirija nayo yamekuwa mengi sana. Hata cancer za via vya uzazi pia zimeongezeka kwa wanaume na wanawake pia. Sababu ziko nyingi sana. Kuna wanaozaliwa na ugumba ambao sasa hv ni wengi tu, na wengine wana develop ugumba ukubwani. Wengine wanajitakia wenyewe kutokana na matumizi mabaya ya madawa etc etc, na wengine ugumba unawapata kutokana na exposure ya vitu kama mionzi, madawa ya mimea etc etc. Ila kwa sasa technology imeimprove sana, kila mtu ana uwezo wa kuzaa, hata waliopita menopause 😜