One size doesn't fit all "the element"

One size doesn't fit all "the element"

M2pc

Member
Joined
Jun 14, 2016
Posts
89
Reaction score
59
Na. Nyacki Jr [emoji871]

Kabla mwandishi hajaanza kuandika Chapters ktk utambulisho chini kabisa ya aya kuu aliandika kitu alicho kiita

"ONE SIZE DOESN'T FIT ALL"

kwa akili ya kawaida kabisa hapa maana yake ni kwamba kiatu cha saiz moja hakijawai kuwatosha watu wote.

Mwandishi amejaribu kuzungumza namna ambavyo dunia imekua ikipoteza watu ambao wangeleta matokeo makubwa ktk nyanja mbali mbali kwa kutokutambua baadhi ya vipawa vya watu na uwezo wa watu wengine kwa kutumia FILTER walioipa jina la ELIMU YA KISASA (FORMAL EDUCATION)

elimu ya kisasa (elimu ya kileo) hutumiwa kama kipimo cha uwezo wa watu kuyatawala mazingira yao na dunia kwa ujumla. Maana yake ni kwamba kama mtu yyte atashindwa kwendahana kulingana na matakwa ya mfumo wa elimu ya kisasa basi huyo ataonekana umuhim wwte ktk dunia ya leo.

Mfumo wa Elimu ya kisasa unatambua kitu wanachoita AKILI YA DARASANI (CLASS ROOM INTELLIGENCE) ambapo hapa ili binadam aonekane ana akili ni lazima awe na uwezo wa kusoma na kufauru masomo ya darasani yanayotambulika na universe.

Yaani awe na uwezo wa kupata "A" ya Hisabati, Chemia, Fisikia, Baolojia na Masomo mengineyo.

Elimu ya kisasa imeweka matabaka pia ktk upande wa Level ya Makundi yaakili wenye akili. Kwa maana ya kuwachukulia watu wanao pata alama "A" ktk masomo ya Sayansi km kundi la watu wenye zaidi kuliko makundi yote ,kisha kundi la Wanaofaulu ktk masomo ya Biashara na mwisho kabisa wanaofauru ktk masomo ya Sanaa.

Mfumo wa elimu wa kisasa hautambui Mtu anaezaliwa na ELEMENT. Kwa Lugha nyepesi tunasema "LIONEL MESSI " kwa kua hajawai kupata alama "A" ktk somo lolote ktk mfumo wa elimu ya kisasa basi anachukuliwa km mtu ambae hana akili.

Kitabu cha THE ELEMENT kina jaribu kueleza mapungufu ya dhana ya mfumo rasmi wa elimu ya kisasa km mfumo wenye mapungufu makubwa ktk maendeleo ya kidunia.

Mwandishi anaeleza namna ambavyo watu ambao hawakuwai kabisa kufauru Darasani walivyotumia uwezo wao (ELEMENT ZAO) Kuweza kufanya mapinduzi makubwa ktk sekta mbali mbali za ki dunia.

Mwandishi anajaribu kusisitiza juu ya Umuhimu wa Kutumia Zaidi ya Saizi moja ya viatu (More than one size of shoes) ili viwatoshe watu wote.

Akiwa na maana ya kwamba mfumo unatumika sasa wa elimu ni mfumo baguzi ivyo ni vyema kama mfumo wa sasa ungeweza kujitanua na kutambua uwezo walio nao watu nje ya vitu vichache ambavyo vimewekwa kTanzania rasmi wa elimu.

Nakupa mfn.
Kwa Nchi km Tanzania Mfumo wa Elimu wa Tanzania Unatambua Na kufundisha Masomo rBinaadam

Kwa kawaida tunaamini kila Binaadam anaezaliwa lazima awe na kitu cha Kipekee ambacho anazaliwa nacho.

Sasa ktk nchi ya Watu Mil 50 maana yake nimwingine kwamba kila mtu kati ya watu Mil 50 ana kitu cha kipekee ambacho hakuna mtu yyte anaweza kuwa nacho.

Kwa lugha nyingine tunaweza kusema kua Tanzania ina Jumla ya Vipaji vya kipekee Mil 50 ambavyo unaweza usivipate mahali kokote duniani.

Lkn kwa sababu mfumo wa elimu zetu hautambui Uwezo wa asili wa binaadam nje ya Elimu ya mambo 11 tu ya kimapokeo, km nchi Tumejikuta tukipoteza Matunda ya Uwezo wa Asili (Natural Intelligence ) ambao kila mwananchi wa Tanzania anao.

Ktk The Element kipengele cha ONE SIZE DOESN'T FIT ALL mwandishi ameeleza stori kuhusu Mwanamuziki wa Jaz nguli Dunia Paul McCartney.

Anasema Anakumbuka Mwanzoni mwa miaka ya 60 wakati anapelekwa Shule kusoma.

Moja ya Wanafunzi ambao alikutana nao shule Alikua ni Paul McCartney. Wakati huo Mc Cartney alifahamika km Mwanafunzi mkorofi asie na akili kabisa darasani.

Paul alikua anaaga nyumbani akiwa amevaa nguo za Shule na kujifanya anaenda shule lkn mwisho wa siku alikua hafiki shule anaenda Pembezoni mwa jiji la Liverpool uswahilini kwenda Kujifunza Kuimba na kupiga gitaa.

Muziki ndo kitu ambacho paul alikipenda. Hakuwai kujua Hisabati hakuwai kujua kabisa kuhusu Fiziksi.

Paul alipenda muziki na kwa kua alipenda muziki paul alijifunza Muziki na kuufanya muziki.

Maana ya The Element ni eneo ambalo kitu tunachopenda kufanya kinapokutana na kitu tunachoweza kufanya.

Kwa lugha rahisi tunasema Pa

ul alitambua Element yake.

Na baada ya kutambua, Alifikia Kuacha Shule (kitu alichoshindwa kabisa) na kuanza kuimba.

Bahati mbaya sana Muda mchache Baada ya Paul kuacha shule, wamiliki wa Shule aliokua akisoma Paul na Robertson walishindwa kuendesha huduma za Elimu na Kulazimika Kubadiri matumizi ya yale majengo yaliokua ya shule.

Wakatu huo Paul McCartney alikua ameshatoka na kuwa Miongoni mwa Wasanii wakubwa wa muziki wa Jaz duniani.

Anguko la huduma ya elimu kupitia chuo cha Liverpool Institute of Education lilipelekea wanafunzi wengi kuacha chuo na wengine wengi zaidi ku amia ktk vyuo vingine.

Baada ya Miaka kadhaa kupita yale majengo yaliokua yakitumika km chuo wamiliki waliyabadiri matumizi na kutengeneza Kumbi kubwa na ya kisasa ya burudani ambapo Paul McCartney alikua akienda kutumbuiza hapo akiwa na bendi yake.

Kumbi hii ilkuja kuwa kumbi maarufu zaidi ya burudani kwa bara la ulaya ambayo baadae Kikajengwa chuo cha Muziki hapo hapo.

Ktk hali ya Kushangaza yule Mwanafunzi ambae Alipuuzwa wakati anasoma na kuonekana km hakuwa na Akili, safari hii ndio Aliteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Sanaa. Kwa maana nyingine Paul McCartney alipata dili na kupewa ukuu ktk Chuo kilichopewa jina la LIPA (Liverpool Institute of Physical & Fine Arts).

One size doesn't fit all but finally paul has got wat fit him.

Je Ungependa kujua nini kiliendelea? Tulia hapa hapa.

Tukijaaliwa tunaeza endelea [emoji871]
 
The element, mwandishi anazungumzia kipaji (talent) ambapo kila mwadamu huzaliwa na kipaji chake maalumu na uwezo wa ndani kabisa wakupambanua nakuyakabili maisha. Japo jamii huamini katika mfumo wa elimu wa kisasa yaaan formal education, ikijiaminisha kwamba ili mtu ufikie malengo fulan maisha ama ufanikiwe ni sharti upitie mfumo huo, nadharia ambayo si sawa hata kidogo. Kwa maana kwamba unaeza tumia kipawa ulichojaliwa na Mungu kuyakabili maisha yako. Vile vile mwandishi anaonyesha kuwa hata mfumo huu wa formal education bado ni mfumo baguzi kwa hautoi fursa sawa kwa wote na ni wa matabaka kwa maana kwamba hutumia Masoma rasmi ktk syllabus kugawa wanafunzi katika matabaka "Alama" wazipatazo ktk mtihani wale wenye A's huonekana vipanga na wale F's huonekana vilaza, na ilihali wanavipaji lin lukuki ila wanakuwa wahanga wa mfumo. Mwandishi ana challenge mfumo huo wa elimu ambao ni too general kwa kusema size moja haiwezi wafiti wote. Hivyo anahamaisisha mfumo unaoweza ku custermize na kumeet ama kutambua talent mbalimbali na kuziendeleza.
:[emoji1593]
 
"THE ELEMENT"
[emoji94]

Baada ya jana kusimlia kidogo kuhusu Phase inayosema "ONE SIZE DOESN'T FIT ALL " Ikiwa na maana ya saizi moja ya kitu chochote haijawai kuwatosha watu wote. Kwa maana ya saizi moja ya kiatu au saiz moja ya nguo haiwez kuwatosha watu wote. Haiwez kuwatosha kwa sababu watu tunatofautiana. Kuna watu wanene wanaohitaji saizi nene na kuna watu wembamba ambao watahitaji saizi nyembamba. Kuna watu warefu na kuna watu wafupi. Kuna watu wakubwa na watu wadogo.

Unapoleta Saiz ya aina moja haitawatosha watu wengi.

Ikimbukwe mfn huu wa haya maneno ulikua una relate na mfumo wa Elimu wa sasa. Mfumo ambao unafananisha na Size Moja ya Kiatu au nguo. Wakati wahitaji wa Elimu ni wengi. Matokeo yake dunia imekua ikipoteza mamilioni ya talents za watu ambao wangeweza kuwa na matokeo makubwa ktk nyanja mbali mbali.

Leo tunaangazi kwa kifupi mambo mawili. Moja ni Nafasi ya mabadiriko (A PACE TO CHANGE) Pamoja na maana ya Title ya The Element na misingi yake.

Mwandishi baada ya kueleza mfumo wa elimu aligusia kidogo kuhusu Kitu alichokiita "A Pace to Change" alijikita zaidi kuzungumzia namna ambavyo Dunia inakimbia kwa nguvu ya Teknolojia pamoja na Demografia.

Anasema Kwa makadirio ya kawaida kabisa Binaadam ambae amezaliwa leo kuna uwezekano mkubwa aka staafu kazi mnamo mwaka 2070.

Changamoto kubwa ni kuwa hakuna uhakika kwamba Hali ya mfumo wa uendeshaji dunia ktk nyanja zote muhim ilivyo sasa itakua ivyo ivyo mnamo mwaka 2070.

Akatolea mfn Mpk mwanzoni mwa Mwaka 90 dunia haikuwai kuwa km ilivyi leo. Hakukua na mapinduzi ya Ki digitali, wla matumizi ya Teknolojia km Laptops na Power Points.

Anasema Dunia ya leo inalazimisha Watu waliozaliwa kabla ya kuzaliwa kwa Digitali ku kimbizana na matakwa ya Kidigitali akitolea mfn kuwa Mapokeo ya Kidigitali ya sasa kwa watoto waliozaliwa wakati wa digitali ni sawa na Kujifunza Lugha mama ( Mother Tongue ) wakati kwa wazee waliozaliwa kabla ya digitali ni sawa na Lugha ya pili (Second Language).

Msisitizo ukiwa ni umuhim wa mfumo kutambua zaidi uwezo wa asili wa kila mtu dhidi ya matawa ya mfumo wa elimu yenye mlengo wa kimapokeo ya kale.

Mwandishi akaenda mbali zaid kwa kutolea mfn Binti yake.

Anasema siku moja aliwa amekaa kwenye bustani nyumbani kwake, binti yake alitoka shule. Wakati huo akiwa na Miaka mi nne. Akamletea assignment ambayo alipewa shule.

Assignment ilikua ya masomo ya hesabu. Somo ambalo mwandishi hakuwai kulijua kabisa wala kulipenda akiwa shule. Na mwandishi ana kili kuwa hakuwai kusoma wala kuchagua kusoma masomo ya hesabu.

Ivyo wakati mtoto wake anamletea yale maswali na kwa sababu ni elementary school akamfanyia vzuri yale maswali. (Maswali ya hesabu za primary school).

Yule binti akatengeneza tabia ya kumpelekea baba ake maswali yote yanayo mshinda. Bahati mbaya sana baba yake alikua ni mzuri sana kwenye masuala ya lugha pamoja na uchoraji.

Binti akiwa na Umri wa miaka kumi na nne, akapewa assignment ya hesabu inayoitwa QUADRATIC EQUATIONS. Akapiga weee akashindwa. Ikabidi airudishe nyumbani kwa baba.

Baba yake alipoona tu ile hesabu akamwambia binti

"Mwanangu Nimekupeleka shule na ninakulioia ili ujue izo hesabu. Itakua haina maana mimi nikikusaidia izo hesabu. Istoshe kazi ya mwalimu wako ni kukufanya ww ujue izo hesabu sio kuleta nyumbani mimi nikudaidie.

Sasa nasema kaa pale ufanye izo hesabu mpk utakapo pata majibu. Na ukipata majibu usiniletee. Mpelekee mwalimu aka hakiki"

Hapo mzee alikua ana jistiri na aibu. Hesabu hajui. Ila hakuwa ana taka binti yke ajue km yeye hajui hesabu.

Baada ya binti kufanya na kumaliza akapeleka kwa mwalimu na kujikuta kakosa yte.

Aliporejea nyumbani baba ake akamwambia kweli umekosa yte lkn je ni nini unaweza kupata zote?

Binti akajibu naweza kuchora. Baba akamwambia fanya sana unachoweza kufanya.

Baada ya miaka kadhaa binti alikua moja ya watu maarufu sana ktk sekta ya uchoraji.

Mwandishi anasisitiza juu ya umuhim wa kutumia nafasi ktk kufanya mabadiriko (a pace to change).

Anaeleza maana ya Title ya the element kama kituo ambacho kinakutanisha
 
Ahmed Mohamed:
Tunazaliwa na uwezo wa asili kila mtu(natural capacity) kwa maana kila mtu ana kabila lake,lakini tatizo linakuja pale tunapo associate na watu ambao sio makabila yetu.Unapotambua kabila lako inabidi uwatafute watu wa kabila lako kwa maana wao wanaiona dunia the way wewe unavyotaka kuiona INSIGHT-Listen and learn from people who have already been where you want to go.Kingine katika kusupport kabila lako kuna kundi la watu tunawaita Mentors je huwa tunao hawa watu katika kuover come vikwazo katika kuelekea element zetu.Je mentor anakuwa na nafasi gani kwetu,well mentor lazima aweze kurecognize yaani kutambua element ya mtu sababu sometime mtu waweza kuwa na kitu flani ndani yako na usitambue but kuna jicho la tatu ambae ni mentor yeye muda mwingine anaweza kurecognize,pia mentor lazima awe na encouragement kwetu sisi yaani aweze kumuhamasisha mtu kuishi ile element yake.Pia kuna kitu tunaita Facilitating pia mentor ana play role kubwa katika kumpa mtu some ideas and technique katika kuishi kabila lake.Pia kuna kitu tunaita Stretching kwa maana mentor atakupa mkazo katika kupambana kwenye vikwazo tunavyo kutana navyo.So The Element mbali na kutafuta uwezo wako wa asili pia inatukumbusha nafasi kubwa walizo nazo mentors.
 
Back
Top Bottom