msumeno
JF-Expert Member
- Aug 3, 2009
- 2,826
- 1,730
Waungwana kaka yenu nakaribia kurudi nyumbani baada ya kuishi hapa DRC kwa Takriban miaka 2.
Katika kipindi chote nilichokaa hapa nimejifunza mengi sana ila leo nitazungumzia kuhusu hawa jirani zetu Wanyarwanda.Maana nimekua nikipita hapa mara kwa mara. Kwa kifupi ondoeni dhana potofu kuhusu hawa jamaa maana mimi dhana hiyo tayari nimesha ifuta. Wengi wenu kama sio wote mnadhani kuwa wanyarwanda ni watu ''wasio poa'' au ni wenye majivuno labda wengine mnadhani eti hawatupendi Watanzania.
Dhani hizi ni potofu kweli kweli, mwanzoni nikipita hapa sikua nikiongea kiswahili ili nisitambulike maana niliogopa kweli hawa jamaa. Baadae nikagundua dhana yangu sio sahihi kabisa na Mungu anisamehe.
Hawa jamaa hawana shida kabisa na wageni hasa Watanzania. Nimekaa Hoteli mbali mbali hapa nikiwa transit kwenda DRC au kurudi Home Tanzania, na kote huko nimechukuliwa vizuri sana tu.
Sio hotel tu , nimepanda boda boda, nimefika masokoni, msikitini , madukani kote huko hawa jamaa ni wakarimu sana na nimetendewa vizuri kwa kweli.
Wacha niweke mifano michache hapa mnielewe, nasisitiza michache mana nimengi nimeyaona positive.
1. Nikitoke DRC kurudi home ( niko njiani) tukiwa pale Kingarama Restaurant nikapata shida kidogo ya chenji ya Dollar kwa FRC ya Rwanda ili nipate Supu, wakati nikitaka kutoka nikatafute nje chenji mzee mmoja akasema kumwambia mhudumu mwache apate hiyo supu nitalipa mimi kama 'felistation' maana walitufunga kombe la CHAN huyu mzee alijua mimi ni Mkongo, nikala na wala hakukaa kuni bore kwa vile ameninunulia supu alitimua.... nikashangaa maana DRC husema hawa jamaa hawawapendi
2. Mh PK alitoa ma Bus kadhaa kuja pale Gisenyi kuchukua mashabiki wa DRC bure ili waje washangilie timu yao .... BUS zilijaa wakongo na walilindwa na wakarudi kwa amani.
3. Nilipofika Kigali na baada ya kuchukua Hotel, nikataka kwenda Masjid kusali , nikauliza Reception , kwa mshangao akadakia jamaa mmoja na kuniambia ''msikiti uko mbali ila subiri nitakupeleka maana naelekea njia hiyo hiyo huyu hakua musilam na hakua akinijua , ni tax man tu alie leta mteja pale. Njiani tulipiga soga sana.
4. Nikiwa hapa kwa siku ya pili na ticketi yangu ikiwa ya jioni nikaona ni negotiate nikae mpaka jioni kwa kulipa kidogo chumba maana check out ni saa tano asubuhi... Manager akasema ''kaa tu usilipe chochote , karibu tena wakati mwingine''.
5. Huko mitaani niliko kwenda kutembea jana usiku, nilikutana na ukarimu sana hasa unapouliza direction na mengine. hawa jamaa wana smile sana na sio ya smile ya kinafiki au ya kutegemea kitu
(a) Kitu nimegundua labda unaweza sema cha kushangaza au sio kizuri ni kwamba watu hapa hawaongelei siasa sana , ni aghalabu kukuta watu wakiongelea siasa hapa tofauti na home TZ kila mtu politician
(b) Printing media sio nyingi ila TV station wanazo nyingi tu
(c) Polisi ni vijana na hawacheki cheki wako serious kweli ila ukiuliza kitu wanakujibu vizuri tu
(e) Rushwa hapa sio sana labda niseme hakuna, polisi akikumata unaandikiwa charge hakuna zile za kuvutana nyuma ya gari na watu wanatii sheria kweli kweli
(f) Ule mfumo wa ukusanyaji kodi kila duka hapa, na kuna ka machine kama ka fingure print sijauliza ni ka nini ila ni ka mamlaka ya Kodi ya Rwanda. ( hapa nikakumbuka zile machine zetu sijui zilishia wapi maana zilileta sintofamu)
(g) Taxi zina Automatic Counter kama za Europe
NIMEONA MENGI WACHA NIACHIE HAPA NA WENGINE WACHANGIE MAANA NATUMAINI KUNA WENGI WAMEPITA HAPA PIA, WITO WANGU KAMA UNA JIRANI YAKO MNYARWANDA USIMTENDEE VIBAYA HAWA WATU WENGI WAO NI WAZURI SANA KWETU