Ombwe la uongozi linawatesa Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ombwe la uongozi linawatesa Watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kupelwa, Aug 5, 2012.

 1. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  Deogratius Temba


  TAIFA linakabiliwa na ombwe kubwa la uongozi na kukosekana kwa viongozi waadilifu, wenye utu, wanaojituma na wazalendo ndiyo maana maendeleo yaliyokusudiwa hayafikiwi na wananchi wanazidi kuwa maskini siku hadi siku.


  Kukosekana kwa uongozi thabiti na imara wa kuliongoza taifa letu, kumesababisha hali ya taifa kwa ujumla na kwa mtu mmoja mmoja kuzidi kuwa mbaya na kusababisha matatizo yasiyo na kikomo.


  Kuna msemo usiopendwa sana na viongozi hasa wanaposikia wananchi wanalalamika na kuutamka “ afadhali wakati wa mkoloni kuliko hivi sasa,” Watanzania wanafikiri ni afadhali wakati ule ambao kila mtu alikuwa na uhakika wa kuishi kuliko leo.


  Hali ni tofauti, nchi imejaa kila aina ya matatizo. Ongezeko la vibaka, majambazi, rushwa, ufisadi, njaa, mfuko wa bei, unyanyasaji wa kijinsia, ukandamizaji wa maskini au walalahoi, kutungwa kwa sheria kandamizi na mengine.


  Hali hii inahatarisha amani ya taifa, kila Mtanzania anatembea kwa hasira na chuki akiamini kuwa anaibiwa, anadhulumiwa, amani ya taifa hili ipo wapi? Ubakaji wa haki za msingi za wenzetu kama wafanyakazi wanavyofanyiwa huku ukipigiwa vigelegele na makofi na wabunge.


  Viongozi wetu wameshindwa kutathmini safari ya taifa mahali lilipo na linapokwenda, angalia jinsi migomo na maandamano yalivyoshamiri kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.


  Migomo imekuwa kwa awamu, tukimaliza mmoja unafuata mwingine na hatupati ufumbuzi wake, na viongozi wanahitimisha kwa vitisho na kutumia dola.


  Mfano hai wa haya, ilianza kwa wauza mafuta, madaktari, madereva wa malori ya mizigo, daladala, walimu, sasa unafuata wa wafanyakazi wote nchini na tayari wameanza wa kampuni za madini, wakimaliza unakuja wa waandishi wa habari na wahariri wao wakilalamikia sheria mbovu ya magazeti namba 6 ya mwaka 1976.


  Wanahabari wataandamana kudai haki yao ya kufanya kazi kwa uhuru bila kushambuliwa na kufunguliwa mashitaka kila mara kama ilivyo kwa mwandishi Samson Mwigamba, Mhariri Absalom Kibanda na Theophil Makunga.


  Tutakapomaliza mgomo wa waandishi wa habari, wanafunzi wa shule za msingi watakuwa wanagoma kupinga mgomo baridi wa walimu unaoendelea chinichini, wakati huo huo, kaka zao wa vyuo vikuu watakuwa wakidai posho ya kujikimu vyuoni kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).


  Kwa sababu ya mfumo mbaya tulionao, migomo itaendelea ambapo, wamiliki wa mabasi watagoma kupinga kupanda kwa ushuru, kodi ya zima moto, barabara mbovu na gharama za mafuta, itafuatia mgomo wa wakulima ambao nao watapinga mfumo wa Stakabadhi Ghalani ambao hauwanufaishi ipasavyo.


  Mfumo huu umechangia kushuka kwa ufanisi katika kilimo na kukumbatiwa kwa wawekezaji wakubwa kwenye sekta ya kilimo kuliko wazawa.


  Mgomo mwingine ambao serikali isipochukua hatua utatokea, ni wa waganga wa kienyeji, waosha maiti, masheikh, wachungaji, mapadri na maaskofu, walaji, watalii na awamu nyingine ya migomo itakuwa ya wafungwa, Magereza , Mahakama na Polisi ambayo inaweza kuleta balaa sasa.


  Tunaomba Mwenyezi Mungu atuepushie tusifike huko, lakini tusipokuwa makini ni rahisi kufika. Tusipuuze wala kudharau.


  Migomo mingi inapofuatana hivi, inaibua chuki, hasira na uhasama kwa wananchi dhidi ya serikali yao, matokeo yake ni kuvunjika kwa amani, sote tutalia na kusaga meno. Tuchukue hatua, viongozi watulie watatue migogoro ya jamii na si kuwapuuza na kutukana.


  Tangu mgomo wa madaktari, nimekuwa nikifikiria sana jinsi serikali yetu inavyojitahidi kutatua matatizo ya wafanyakazi na wanafunzi kwa mgongo wa mahakama, badala ya kutatua tatizo, unakimbilia mahakamani, au kuwakamata wahusika na kuwafungulia mashitaka.


  Kila mtu anajiuliza hivi hawa viongozi kwanini wanakimbilia mahakamani na si kutatua tatizo?


  Je, unaweza ukamlazimisha mwalimu, daktari akafanye kazi? au bado serikali imebaki kwenye imani za kizamani kuwa ‘ualimu na udaktari ni kazi za wito?” Serikali imesema haitaki migomo, inataka nini kwa wafanyakazi wake? Je, waende darasani wangali wana njaa? Je, ni aina gani ya mgomo wanautaka?


  Ni huu baridi ambao wanataka kusikia kuanzia sasa ili watoto wa maskini waumie zaidi? Je, wanataka kuwaona madaktari hospitalini wakiwaacha wagonjwa wakijifia? Walalahoi wa taifa hili ambao hawawezi kusoma shule za gharama kubwa, kutibiwa au kupata huduma katika taasisi za binafsi wanateseka kwa kukosekana kwa uongozi bora katika taifa lao.


  Afadhali tuwe na mgomo ambao umetangazwa na tunajua hakuna anayetibu wagonjwa au kufundisha kuliko kuwa na mgomo wa kufundisha uongo.


  Jamani, tunakoelekea siko, tunahitaji kuchukua hatua za haraka kuliokoa taifa hili. Ombwe la uongozi ni kikwazo, tunahitaji uongozi wa Tanzania mpya! Mungu ibariki Tanzania.
  CHANZO :MAKALA TANZANIA DAIMA
   
 2. tonnyalmeida

  tonnyalmeida JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 226
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Worth reading! siku zote Uongozi unaanzia Juu (IKULU) na sio kwa wananchi.

  Nlishangaa JUZI katika hotuba ya RAis ya mwezi uliopita alipoongea kupitia wahariri wa vyombo vya Habari anasema ETI KUGAWA WIZARA YA NISHATI NA MADINI MDA MDA UMEBAKI MCHACHE KUELEKEA 2015 hivo NGOJA SISI TUMALIZIE WATAKAOKUJA WATATUMIA BUSARA ZAO............... AMAIZING Wenzie wanapanga mipango ya miaka 100 bila kujua kama watakuwepo au laaa yeye hata ya miaka 3 kashindwa kupanga eti mda umebaki mfupi


  NIKAGUNDUA KUMBE KWA SASA NCHI IMEKUWA INGAGED KWENYE AUTO-PILOT INAJIENDESHA ILI 2015 AIACHIE HALAFU MTAJIJUA KAMA MTATUA SALAMA AU LAAAA..So bad aiseeeeeee
   
Loading...