Ombi Langu kwa Viongozi Wakuu wa Nchi

The Retired Planner

Senior Member
Sep 22, 2015
166
241
Ili kuleta mabadiliko chanya na kuweka historia katika nchi hii, viongozi wakuu wa nchi mna nafasi kubwa sana kama mtatumia utaifa wenu na kutuongoza katika ile nchi ya ahadi ambayo watanzania wengi wangependa siku moja kuiona kwa sababu kama ni suala la rasilimali, basi si jambo la kuuliza hapa Tanzania. Kama mtaona inafaa, basi niaminini mimi ya kuwa tunaweza kuibadilisha Tanzania katika historia ya ulimwengu huu.

Watanzania wenzangu pamoja na viongozi wa nchi hii kwa ujumla, ina niuma sana pindi ninapoona kwanini pamoja na rasilimali zote hizi ambazo Mungu alitujalia tunashindwa kuzisimamia na kuifanya nchi yetu kuwa ya mfano hapa Duniani.

Ni kweli kabisa kuwa mifumo iliyokuwa imewekwa hapo awali katika nchi ndio chanzo cha haya yote yanayoendelea. Lakini kama tukiamua kwa nia ya dhati kabisa tunaweza kubadilisha haya hata kwa kipindi kifupi tu. Tuachane na siasa za kichama kwani sio msingi wa kimaendeleo. Tuungane kwa Umoja wetu kufanya kazi kwa ajili ya nchi yetu.

Ni ombi langu kwa viongozi wakuu wa nchi hii wasimamie haya mapendekezo yangu kwa ajili ya ukuwaji wa nchi yetu Tanzania.

1. Tujenge motisha ya kazi kwa wananchi wetu ili wajue nini dira ya nchi. Hapa ni lazima viongozi wakuu wasimame kidete kuliongelea kwa kujenga Imani kwa wananchi kuwa sasa ni muda wa kazi. Milango ya kazi iwe wazi kwa kila Mwananchi aidha kwa kuajiriwa ama kwa kujiajiri. Turahisishe kabisa taratibu zote za kiusimamizi (kodi ipunguzwe) ili kuweza kuvutia watu wengi kuingia katika jambo hili na kufanya kazi. Jamii yote ikiingia kazini basi kuwa na uhakika kabisa kodi nyingi itakusanywa na hata ukwepaji kodi utapotea

2. Tuachane na uonevu wa aina yeyote ile, tusimamie utawala wa sheria kwa kila jambo linalotokea nchini. Hapa wote ambao waliipeleka nchi katika uozo huu na kama ushahidi upo, sheria ichukue mkondo wake.

3. Tufungue milango ya uwekezaji kutoka nje lakini tuweke mikakati ya usimamizi bora ili kukusanya mapato stahiki. Taratibu zote za kiusimamizi ziwe bayana (kodi ipunguzwe) ili kuweza kuvutia wadau wengi kuingia katika jambo hili na kuleta mabadiliko chanya.

4. Nchi ina eneo kubwa sana kimipaka, hivyo kilimo cha Kisasa kinaweza kuwa ni mpango Dhahiri wa kuiinua nchi endapo tu viongozi wetu wataweka nia katika usimamizi wake.



Yote haya yanawezekana hata kwa kuchukua mfano mmoja kutoka nchi ya China ambayo kimsingi imekua kwa kasi sana kuanzia miaka ya 90. Mambo makubwa mawili yaliyofanywa na China ni,

1. Utawala Bora (Usimamizi bora wa Sheria) na

2. Kufungua Mipaka ya nchi yao kwa Uwekezaji kutoka nje

Nawahakikishia kuwa, kwa kufanya hayo uongozi wa awamu hii ya tano utaweka historia hapa duniani na Tanzania itakuwa gumzo la dunia hii.


Ni Ombi Langu Sasa, Viongozi Tuyachukue Haya Na Kufanya Bila Kumwogopa Mtu

TRP
2017
 
Back
Top Bottom