OMBI KWA WAZIRI MKUU

baro

JF-Expert Member
May 12, 2014
3,063
3,877
Kwanza nianze kwa kukupongeza Waziri mkuu KASSIM MAJALIWA namna unavyokula bega kwa bega na wazembe kazini,

Baada ya salamu Waziri mkuu, kwa sasa una ziara ya kikazi katika kanda ya ziwa na tetesi ni kuwa 9/03/2016 utakuwa katika mkoa wa kagera wilaya ya missenyi hasa katika kiwanda cha sukari cha kagera sugar ,

Waziri mkuu, sisi wafanyakazi wa nafasi za chini tunaomba tutoe ombi la kuonana na sisi maana miaka yote viongozi wakubwa wakija hatuonani nao ,

Mambo yetu ya msingi tunayotaka tukueleze ni yafuatayo;

1. AJIRA ZA WAGENI
Mh Waziri mkuu kama ilivyo katika taasisi nyingine binafsi ,hapa kagera sugar kuna wageni wengi sana hasa kutoka India , Uganda na Kenya ambao wanafanya KAzi ambazo sisi watanzania tunauwezo nazo , mfano kuna wahindi wametoka India wapo katika shell za mafuta za kiwanda na wanalipwa kama expert wa kuweka mafuta katika matank ya gari huku wakilipwa mishahara minono ambayo haiendani na KAzi wanazofanya , watanzania walifukuzwa waliokuwa wanafanya hizo KAzi kwa sababu ya kusingiziwa ni wezi jambo ambalo si kweli wakat watanzania wako shell walikuwa wanalipwa 400000 na mlinzi 150000 wakat kwa sasa hao wahindi wanalipwa kati ya 4,000,000 hadi 5,000,000 kwa KAzi hiyo hiyo , sababu kuu ni kuwa GM ni mhindi , assistant GM ni mhindi na Accountant ni Mhindi , waswahili wako post za chini chini

2, VIBALI VYA KAZI
Mwaka Jana kulikuwa na kamata kamata ya wasio na vibali nchini hapa kagera sugar wahindi wengi hawana vibali pia hawana ujuzi wowote ( expertise ) hivyo uhamiaji walikuwa wakija hukimbia kujificha na baadae hurudi , kwa sasa wameanza tena kurudi baada ya hali kutulia ,

Hivyo mh Waziri mkuu tunakuomba ukifika kagera sugar ufike idara ya FMT uone wazawa tulivyo watumwa ndani ya nchi yetu pale wamejaa wazungu , wakenya na waganda kwa KAzi za ufundi mchundo na veta ambazo sisi wengi tunaziweza lakini wapo hao wageni wanaolipwa kama expert

Pia , uombe ufike shell ujionee mwenyewe hali ilivyo , hivyo mh Waziri mkuu tunakuomba usiishie ofisini na kudanganywa kupelekwa shambani baadae uondoke tunakuomba na hayo maeneo pita ujue kero zetu , pia tunafukuzwa ovyo bila sababu za kueleweka wengi waliofukuzwa KAzi wapo bunazi wamekaa na tulifukuzwa ili hizo nafasi wapewe wageni
 
Hii inaashiria ombwe katika uongozi wa Dr. Magufuli. Naona ile 'tatizo ni mfumo' bado haijapatiwa jibu. Mh. Magufuli fanya warm up zaidi kwa kuwa hata sheria Kama ya Makosa ya Mtandao) zinatumika kukuwekea wingu ili usipate kujua ukali wa miale toka kwa raia.
 
Back
Top Bottom