Ombi kwa Mheshimiwa Halima Mdee

Ombi kwa Mheshimiwa Halima Mdee

Dopas

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2010
Posts
1,151
Reaction score
392
Habari hapo chini ni sehemu ya habari iliyoandikwa katika gazeti la Uwazi la 14/10/2014 ikieleza aliyoyaona Mheshimiwa Halima Mdee alipokuwa mahabusu wiki iliyopita. Ameorodhesha mambo matano.
Binafsi nimeguswa na yote, lakini kwa namna ya pekee nimeguswa na hili la hawa wasichana wa kazi za ndani, kuwekwa mahabusu kwa kesi za kubambikizwa.

Ombi langu kwa mheshimiwa ni kuwa suala kama hili lisiishie magazetini, natumai yeye kama mwakilishi wa wananchi imemuuma sana suala hili, nadhani atalifanyia kazi haraka zaidi kadiri uwezo wake utakamporuhusu. Ikiwezekana kulifikisha katika meza ya haki za binadamu.

MBUNGE wa Jimbo la Kawe jijini Dar na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha), Halima James Mdee ambaye aliwekwa Mahabusu ya Gereza la Segerea, Dar kwa saa kumi na mbili amesimulia mambo matano mazito aliyokumbana nayo hali iliyomfanya atokwe machozi

Akizungumza na mwandishi wa habari hii mwishomi mwa wiki iliyopita, Mdee licha ya kuponda utendaji kazi mbovu wa serikali kuhusu mahabusu, aliyataja mambo hayo kama ifuatavyo:

WAFANYAKAZI WA NDANI NA KESI NDOGONDOGO
Alisema alipofika mahabusu aliwakuta wasichana wadogo ambao baadhi yao ni mahausigeli wakamlalamikia kwamba wamekaa ndani kwa muda mrefu bila kesi zao kusikilizwa.

Alisema kwa uchunguzi wake alibaini kuwa wasichana hao wa kazi za ndani, kesi zao zilifunguliwa kwa kubambikwa na mabosi wao pale wanapodai malipo, hivyo wao husingiziwa wizi au kosa lolote.

UBOVU WA CHAKULA
Pia Mdee alisema chakula cha mahabusu hakiridhishi kutokana na kupikwa bila kiwango na kuwa na michanga, wakati mwingine hakiivi.

MAHABUSU KUKAA MUDA MREFU BILA KESI KUSIKILIZWA
Jambo jingine alilodai kukumbana nalo Segerea ni mahabusu kukaa kwa muda mrefu kati ya miaka 4 hadi 7 bila kesi zao kusikilizwa kwa kisingizio cha upelelezi kutokamilika.

MACHANGUDOA KUWASHAWISHI MABINTI
Katika sakata lingine, Mdee alisema wanawake wengi waliokamatwa kwa makosa ya kujiuza usiku (machangu) wanaopelekwa mahabusu wamekuwa wakiwashawishi wasichana wadogo, hasa mahausigeli wanaofikishwa humo.

"Wasichana hao huwashawishi mahausigeli kiasi kwamba wanapotoka mle mahabusu na wao wanakwenda kujihusisha na ukahaba na biashara ya madawa ya kulevya kwa vile baada ya kutoka hawapewi nafasi na mabosi wao kuendelea na kazi," alisema Mdee.

MAHABUSU WA KIKE KUADHIBIWA NA ASKARI WA KIUME
Jambo lingine aliloligundua Mheshimiwa Mdee ni kitendo cha askari wa kiume kutoa adhabu kwa maabusu wa kike badala ya kuadhibiwa na wanawake wenzao kitendo ambacho alisema kimekuwa kikiwadhalilisha mahabusu hao.

Hata hinyo, Mdee alimuomba Waziri wa Sheria na Katiba, Asha rose Migiro kuanzisha utaratibu wa safari za kushtukiza magerezani na kuzungumza na mahabusu ili kusikiliza kero zao na kuzitatua.

Jumanne iliyopita, Mdee alifikishwa katika gereza hilo saa 11 jioni ambako alilala hadi kesho yake saa 1 asubuhi kwa madai ya kufanya maandamano haramu kwenda Ikulu ya Dar.
 
Kuna vijana wengi tu.mmemaliza sheria hapa.ndio pa kuanzia kazi
 
Hivi yeye kule Segerea walimfanyia nini?? Mbona hajaandika...
 
Kuna "mabwege" humu wataleta siasa hata kwenye jambo zito kama hili....
 
hii nchi imechoka kuanzia viongozi hadi wananchi. utakuta mtu anatetea upuuzi km huu utadhani yeye haimhusu hata ndg yake tu yanaweza kumkuta. ingekuwa nchi zenye kufuata sheria wangefuatilia lakini kwa vile ni mpinzani... tupa kule.
 
kama walimuua mwangosi na bado wakapandishana vyeo, hilo alilosema mdee watalijali vipi? haki Tanzania itaanza kupatikana mara tu,ccm itakapotoka madarakani
 
Msipende kuijaribu system!! Mkiguswa kidogo kelele nyingi.....tunamkaribisha mwingine.
 
Back
Top Bottom