Ombaomba wadharau agizo la mkuu wa mkoa warudi tena viwanjani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,870
34,357
omba omba.jpg

ombaomba mjin Dar.jpg

Baada ya kutimuliwa ombaomba warejea tena katika jiji la Dar es salaam.

Siku chache baada ya agizo la mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda la kuwafurusha ombaomba katikati mwa jiji la Dar, ombaomba hao wameonekena tena katika barabara za jiji hilo.

Omba omba hao wanadai kwamba wamekosa mahala pa kuenda ama makwao.

Sasa maafisa wa polisi kanda maalum ya jiji wamepanga upya kuwaondoa ombaomba hao wanaosababisha bugdha jijini kwa kuomba watu pesa, chakula na pia kuchafua jiji.

Mkuu wa mkoa Paul Makonda anasema ataweka mbinu mpya za kuwasafarisha na kuwatafutia makaazi.

Omba Omba ni maarufu sana katika nchi zote duniani na juhudi za kuwaondoa mijini zimegonga mwamba katika nchi nyingi.

Austaralia, Canada, Colombia na Nigeria ni miongoni mwa nchi zilizo na watu wengi ambao hawana makwao,wanarandaranda barabarani.

Chanzo: CRI Kiswahili
 
Back
Top Bottom