Ombaomba na wapiga debe, waanza kuondolewa Dar es Salaam

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
12974299_1486953777985702_5557075689351517954_n.png

Dar es Salaam. Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda limeanza kufanyiwa kazi baada ya karandinga kuanza kuwasomba ombaomba waliojaa katika maeneo mengi jijini hapa.

Makonda alitangaza kuanza kuwaondoa ombaomba hao juzi, huku akipiga marufuku wananchi kuwapa pesa kwa kuwa ndicho chanzo cha kuwapo kwao jijini hapa.

‘Mchakamchaka’ wa kuwaondoa watu hao ulianza juzi usiku katika maeneo ya Mnazi Mmoja, Samora na Kariakoo.

Mwananchi ilizunguka maeneo mbalimbali ambayo aghalabu ombaomba hupenda kukaa, lakini yalikuwa tupu.
matonya ombaomba..jpg

Maeneo hayo ikiwamo barabara ya Morocco, Magomeni Usalama, Fire na Baridi hayakuwa na watu wa kundi hilo.

Mmoja wa ombaomba aliyekuwa na watoto wawili alipomuona mwandishi wa habari hizi katika maeneo ya Fire, alitimua mbio na kujificha pembeni mwa barabara, huku akisema: “Tumetoka Dodoma, hatutaki kurudi.”

Akizungumza na gazeti hili, Makonda alisema ikifika Jumatatu kama hawajajisalimisha Serikali itachukua hatua kali na kuwarudishwa walikotoka. “Kwanza ni kinyume cha sheria, pili ni hatari kwa maisha yao na watoto wanatakiwa warudi shule sasa,” alisema.

Kadhalika, operesheni hiyo licha ya timuatimua kuwakumba ombaomba, wapigadebe nao wameunganishwa katika kundi hilo kwa kuanza kuondolewa kwenye vituo vya mabasi.
13012813_1065083310237595_1157762753843138589_n.jpg

Baadhi ya wapigadebe hao wamedai ni vigumu kwa Makonda kuwaondoa kwa kuwa wanachofanya ni kwa manufaa ya maisha yao na hawana pa kwenda.

Agizo la kutaka ombaomba wakamatwe na kuondokana na vitendo hivyo liliwahi kutolewa pia na waliowahi kuwa wakuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuf Makamba, Abbas Kandoro na Said Mecky Sadiki.

Chanzo:
Mwananchi
 
Wapiga debe ni janga.
Yaani wezi balaaa,ukitaka kujua basi jipindue pale msimbazi au mnazi mmoja wakati wa kugombea gari

Jana wameondoka na side mirror pale njiapanda ya shule ya uhuru, kidogo wanisababishie ajali. Hili tukio lilinifedhehesha sana mkuu.
 
We nenda Kigamboni,kuna ombaomba ana bonge la jumba,na anasomesha watoto wake.
Ukiona mbali nenda kibaha,kuna mwingine amejenga nyumba ya maanaa

Wakihojiwa wankuambia pesa ndogo kwa siku ni elfu kumi.Wanafikisha hadi 50,000 per day.
Na ndio maana baadhi yao huamua kuchukua na watoto wao ili wapige pesa ndefu.
 
mjue mle wengi ni wasaniii,kuna walemavu feki kibaooo
ole wako umpe mia,anakutukana

Sio vizuri kuwatolea maneno mabaya au ya kejeli walemavu lakini huyu mzee namfaham ni mzima na anatembea kabisa kwa miguu yake japo hua anajifanya ni kiwete. Mara nyingi anakua pale posta!
 
12974299_1486953777985702_5557075689351517954_n.png

Dar es Salaam. Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda limeanza kufanyiwa kazi baada ya karandinga kuanza kuwasomba ombaomba waliojaa katika maeneo mengi jijini hapa.

Makonda alitangaza kuanza kuwaondoa ombaomba hao juzi, huku akipiga marufuku wananchi kuwapa pesa kwa kuwa ndicho chanzo cha kuwapo kwao jijini hapa.

‘Mchakamchaka’ wa kuwaondoa watu hao ulianza juzi usiku katika maeneo ya Mnazi Mmoja, Samora na Kariakoo.

Mwananchi ilizunguka maeneo mbalimbali ambayo aghalabu ombaomba hupenda kukaa, lakini yalikuwa tupu.
View attachment 338035
Maeneo hayo ikiwamo barabara ya Morocco, Magomeni Usalama, Fire na Baridi hayakuwa na watu wa kundi hilo.

Mmoja wa ombaomba aliyekuwa na watoto wawili alipomuona mwandishi wa habari hizi katika maeneo ya Fire, alitimua mbio na kujificha pembeni mwa barabara, huku akisema: “Tumetoka Dodoma, hatutaki kurudi.”

Akizungumza na gazeti hili, Makonda alisema ikifika Jumatatu kama hawajajisalimisha Serikali itachukua hatua kali na kuwarudishwa walikotoka. “Kwanza ni kinyume cha sheria, pili ni hatari kwa maisha yao na watoto wanatakiwa warudi shule sasa,” alisema.

Kadhalika, operesheni hiyo licha ya timuatimua kuwakumba ombaomba, wapigadebe nao wameunganishwa katika kundi hilo kwa kuanza kuondolewa kwenye vituo vya mabasi.
13012813_1065083310237595_1157762753843138589_n.jpg

Baadhi ya wapigadebe hao wamedai ni vigumu kwa Makonda kuwaondoa kwa kuwa wanachofanya ni kwa manufaa ya maisha yao na hawana pa kwenda.

Agizo la kutaka ombaomba wakamatwe na kuondokana na vitendo hivyo liliwahi kutolewa pia na waliowahi kuwa wakuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuf Makamba, Abbas Kandoro na Said Mecky Sadiki.

Chanzo:
Mwananchi
Akimaliza kuwaondoa ombaomba,nasikia anakuja kwenye mabaa,na machinga,na boda boda
 
Maamuzi yakukurupuka yalitolewa hao omba omba Makonda amewasaidia nini?
hili tamko la mkuu wa mkoa lina nakisi ya WELEDI na UTU kwa kiasi kikubwa sana, sijajua amelenga kutatua nini au amelenga kuwasaidiaje hawa watu. hivi kuwafukuza pekee kutasaidia kutatua matatizo yaliyowafanya wakafikia hatua hiyo?

Huenda Makonda amelenga kupunguza tatizo la wezi na vibaka kwenye vituo vya magari pamoja na kuondoa ombaomba lakini njia aliyoitumia haisaidii kutatua tatizo na huenda ametumia njia ya kinyama sana, hivi babu kama huyo kumwondoa hapo alipo ataishije ?

Tunapojaribu kutatua matatizo tunapaswa kuwa na weledi tuweze kuona mbali zaidi ya macho yetu, tunaweza kutatua tatizo kumbe tunatengeneza tatizo jingine kubwa zaidi.kama makonda amelenga kuondoa tatizo alipaswa aje na mkakati mbadala wa kuwafanya hawa watu waendelee kusurvive maana kundi kubwa ni jobless sasa wakikosa hata pakujishikiza siku mbili ni nyingi jiji litageuka kuwa jiji la VIBAKA.

Kama Makonda hajaandaa mkakati mzuri wa kutatua tatizo atakuwa anafukia dimbwi la mbu kwa kuchimba dimbwi jingine pembeni. time will tell.
 
Mtihani kwa Makonda huu.
Tunatibu homa sio ugonjwa. Suluhu ya kudumu kuhusu ombaomba haiwezikuwa suala la Dar peke yake. Lazima kuhusisha wanakotoka!
 
hili tamko la mkuu wa mkoa lina nakisi ya WELEDI na UTU kwa kiasi kikubwa sana, sijajua amelenga kutatua nini au amelenga kuwasaidiaje hawa watu. hivi kuwafukuza pekee kutasaidia kutatua matatizo yaliyowafanya wakafikia hatua hiyo?
huenda Makonda amelenga kupunguza tatizo la wezi na vibaka kwenye vituo vya magari pamoja na kuondoa ombaomba lakini njia aliyoitumia haisaidii kutatua tatizo na huenda ametumia njia ya kinyama sana, hivi babu kama huyo kumwondoa hapo alipo ataishije ?
tunapojaribu kutatua matatizo tunapaswa kuwa na weledi tuweze kuona mbali zaidi ya macho yetu, tunaweza kutatua tatizo kumbe tunatengeneza tatizo jingine kubwa zaidi.kama makonda amelenga kuondoa tatizo alipaswa aje na mkakati mbadala wa kuwafanya hawa watu waendelee kusurvive maana kundi kubwa ni jobless sasa wakikosa hata pakujishikiza siku mbili ni nyingi jiji litageuka kuwa jiji la VIBAKA.
kama Makonda hajaandaa mkakati mzuri wa kutatua tatizo atakuwa anafukia dimbwi la mbu kwa kuchimba dimbwi jingine pembeni. time will tell.

Ulichosema ni kweli tupu hapa tunaleta tabia za ki Idd Amin, hebu tuwaulize serikali wameboresha makazi ya wazee pale nungwi? tuseme ukweli leo hawa wanaotembelea mavx tuwapeleke kule bahi tukawabwage chini ya mti tu tuwaache wataishi hata wiki pale? Hawa wazee waliojichokea kwa kutokwa jasho la kulitumikia taifa leo unawafurumusha kama mbwa koko wa jalalani kweli? hawa wazee walitakiwa wapewe pensheni na bima za afya waweze kujikimu kimaisha.

Munafurumusha ombaomba wapigadebe machangudoa wala mtatui tatizo mutakuwa munazungushana kama paka na panya chumbani. Huku ni kujitakia kukosa thawabu, mzee yusuf makamba aliyehakikisha matonya anenda kufia mbali yuko wapi leo? Idd Amin aliyeamuru viwete wakusanywe kwenye tipa mji mzima yuko wapi leo? Hitla aliyeamua kuwakusanya wakoma na kuwasweka ndani yuko wapi leo?
 
12974299_1486953777985702_5557075689351517954_n.png

Dar es Salaam. Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda limeanza kufanyiwa kazi baada ya karandinga kuanza kuwasomba ombaomba waliojaa katika maeneo mengi jijini hapa.

Makonda alitangaza kuanza kuwaondoa ombaomba hao juzi, huku akipiga marufuku wananchi kuwapa pesa kwa kuwa ndicho chanzo cha kuwapo kwao jijini hapa.

‘Mchakamchaka’ wa kuwaondoa watu hao ulianza juzi usiku katika maeneo ya Mnazi Mmoja, Samora na Kariakoo.

Mwananchi ilizunguka maeneo mbalimbali ambayo aghalabu ombaomba hupenda kukaa, lakini yalikuwa tupu.
View attachment 338035
Maeneo hayo ikiwamo barabara ya Morocco, Magomeni Usalama, Fire na Baridi hayakuwa na watu wa kundi hilo.

Mmoja wa ombaomba aliyekuwa na watoto wawili alipomuona mwandishi wa habari hizi katika maeneo ya Fire, alitimua mbio na kujificha pembeni mwa barabara, huku akisema: “Tumetoka Dodoma, hatutaki kurudi.”

Akizungumza na gazeti hili, Makonda alisema ikifika Jumatatu kama hawajajisalimisha Serikali itachukua hatua kali na kuwarudishwa walikotoka. “Kwanza ni kinyume cha sheria, pili ni hatari kwa maisha yao na watoto wanatakiwa warudi shule sasa,” alisema.

Kadhalika, operesheni hiyo licha ya timuatimua kuwakumba ombaomba, wapigadebe nao wameunganishwa katika kundi hilo kwa kuanza kuondolewa kwenye vituo vya mabasi.
13012813_1065083310237595_1157762753843138589_n.jpg

Baadhi ya wapigadebe hao wamedai ni vigumu kwa Makonda kuwaondoa kwa kuwa wanachofanya ni kwa manufaa ya maisha yao na hawana pa kwenda.

Agizo la kutaka ombaomba wakamatwe na kuondokana na vitendo hivyo liliwahi kutolewa pia na waliowahi kuwa wakuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuf Makamba, Abbas Kandoro na Said Mecky Sadiki.

Chanzo:
Mwananchi

Dah, pole zake kijana Le Mutuz, sijuwi nduguze watazaliana kwenye madaraja gani mwaka huu maana walikuwa wanalimezea mate kweli daraja la Kigamboni ila Makonda aliwashitukia mapemaaa!
 
Mtihani kwa Makonda huu.
Tunatibu homa sio ugonjwa. Suluhu ya kudumu kuhusu ombaomba haiwezikuwa suala la Dar peke yake. Lazima kuhusisha wanakotoka!
Yusuf Makamba alifanya haya haya, Mama chipungahelo alifanya hayahaya, Kaka ditto alifanya hayahaya na tatizo liko palepale, hakuna hata siku moja tatizo la kijamii likatatuliwa kipolisi, hapa analichochea moto tu, kuhangaika na dadapoa wapiga debe ombaomba ni mambo ya kitoto tu haya, cha kushangaza hata watu na akilizao kama kamanda zero nae anakokotwa humohumo.
 
Ulichosema ni kweli tupu hapa tunaleta tabia za ki Idd Amin, hebu tuwaulize serikali wameboresha makazi ya wazee pale nungwi? tuseme ukweli leo hawa wanaotembelea mavx tuwapeleke kule bahi tukawabwage chini ya mti tu tuwaache wataishi hata wiki pale? Hawa wazee waliojichokea kwa kutokwa jasho la kulitumikia taifa leo unawafurumusha kama mbwa koko wa jalalani kweli? hawa wazee walitakiwa wapewe pensheni na bima za afya waweze kujikimu kimaisha.

Munafurumusha ombaomba wapigadebe machangudoa wala mtatui tatizo mutakuwa munazungushana kama paka na panya chumbani. Huku ni kujitakia kukosa thawabu, mzee yusuf makamba aliyehakikisha matonya anenda kufia mbali yuko wapi leo? Idd Amin aliyeamuru viwete wakusanywe kwenye tipa mji mzima yuko wapi leo? Hitla aliyeamua kuwakusanya wakoma na kuwasweka ndani yuko wapi leo?
anachokifanya Makonda ni kuwageuza hawa watu kuwa sehemu ya kutafutia sifa za kijinga bila kuzingatia utu wao. kuwaondoa posta na mnazi mmoja is not a solution. ni kuwafanyia uonevu simply si wazazi wake au ndugu zake na kwa sababu yeye ana mamlaka ya kuwaondoa anaamua kufanya hivyo. this is an ill reasoned decision ever seen.
 
Yesu alimkuta kipofu kwenye mlango wa sinagogi hakumpiga teke alimponya na akaenda kuwashuhudia watu wamataifa, leo wewe unamkuta kipofu kwenye mlango wa kuingia msikitini unaanza kumkwida na kumdhalilisha, hivi amekosa ushauri wa namna ya kumaliza hili tatizo kweli? amewaona USAID au UNICEF wakashindwa kumpatia ushauri mzuri wa kuondokana na hili tatizo, yeye anatembea kwenye VX huyo ombaomba wa mtaa wa zanaki anamkera nini?
 
Back
Top Bottom