Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,393
- 33,965
- Thread starter
-
- #21
Maishapopote,Mzee wangu nimemjua mzee mwariko tokea nikiwa mdogo mwaka 84-85 alikua maarufu sana na alishamchongea baba wa taifa kifimbo chake
Mzee mwariko yupona amejaribu mara kadhaa kupata nafasi ya kuwa mbunge wa moshi mjini kupitia ccm ila hakupata nafasi....
ukimtaja unanikumbusha utoto wangu...Mtaa wa Kenyata street, nikienda mtaa wa chini kuzurura na kuchungulia wakicheza ngoma kwa mzee mwariko...
MUNGU AMBARIKI...NA AKUBARIKI
Nawe mdini tu huna loloteHebu ficha upumbavu wako, hakuna unachotaka kukipandikiza hapo
Maalim Mohammed SaidThomas Sankara,
Hakika nitakuwa nawafahamu.
Uzi unataka kuusoma na maneno ya shombo unayo, hebu usituchafulie Uzi Sisi huwezi nenda kwenye majukwaa mengine, ukiona.mtu anaandika neno "mdini" mjini kaja baada ya shule au ndio walewale. Povu ruhusa maana kipo unachokitafuta. Mdini mdini hovyo umelazimishwa kuusoma?Nawe mdini tu huna lolote
Acheni udini karne ya 21Uzi unataka kuusoma na maneno ya shombo unayo, hebu usituchafulie Uzi Sisi huwezi nenda kwenye majukwaa mengine, ukiona.mtu anaandika neno "mdini" mjini kaja baada ya shule au ndio walewale. Povu ruhusa maana kipo unachokitafuta. Mdini mdini hovyo umelazimishwa kuusoma?
Kolola,Acheni udini karne ya 21
Nnangale,dunia ina maajabu yake dini ni jambo la imani ni kweli Mohammed angetaka ikiwezekana wote tuwe waislam ingawa haiwezekani hata mimi hapa ningependa wote mfuate imani yangu kwani naona niko sawa hivyo Mohammed yuko sawa kwa anacho Fanya kama kaandika kuhusu waislam tu hao ndio anaowafahamu na wewe andika unaowafahamu lkn siyo kulalamika.
Kwahiyo kupotea kwake ni tatizo la nani?OMARI MWARIKO NANI ANAMFAHAMU?
Huyo hapo chini aliyevaa kofia ni Omari Mwariko.
Nimemfahamu Omari Mwariko nakua na nasoma shule ya msingi Moshi katika miaka ya 1960.
Miaka hiyo Omari Mwariko alikuwa mtu maarufu sana.
Omari Mwariko ni msanii bingwa katika kuchonga na kazi zake zimeonyeshwa hapa nchini, Uingereza na Marekani.
Lakini kwa miaka mingi akawa kapotea katika ulimwengu wa usanii akawa haonekani wala hasikiki.
Siku moja miaka 13 iliyopita niko Moshi ghafla nikakutananae barabarani.
Nikamsalimia na nikajitambulisha kwa kumtajia jina la ndugu yake Athmani Upepo.
Hili jina "Upepo," si jina lake ila alipachikwa kwa ajili ya uwezo wake wa kukimbia mbio kwa kasi kubwa.
Nakumbuka utotoni Moshi kila mtu alikuwa na lakabu yake.
Kulikuwa na Ali Maresi.
Hili jina "Maresi," alipewa kwa uhodari wake mpirani kuwa akitanguliziwa pasi mpira akadodoshewa kwa mbele na kuupokea mabeki hawampati na atafunga goli.
Kulikuwa na Athumani Makufuta.
Kisa cha jina hili ni kuwa tukisomeshwa somo la Hand Craft Majengo Middle School na Mwalimu anaitwa Fritz (sina hakika na "spelling").
Huu ulikuwa mwaka wa 1963.
Mwalimu Fritz alichukia sana mwanafunzi kuchora kisha akafuta.
Adhabu yake ni viboko papo kwa papo.
Athumani akafuta na akala mboko sote darasani tunashuhudia.
Athumani Mfinanga toka siku ile akawa Athumani Makufuta.
In Shaa Allah iko siku nitaandika kuhusu haya majina na kuwatafuta wahusika ili tucheke.
Nitaanza na "Toligogo" Omari Matola golikipa hodari amefariki miaka michache iliyopita.
Sote tulikuwa wanafunzi wa Mwalimu Juma darsa yake baina ya Maghrib na Isha Msikiti wa Ijumaa.
Jina hili ukimwita lilikuwa na staili yake maalum.
Unalitamka kama vile unaimba.
Rafiki yangu Allah amrehemu kila nilipokutananae iwe Dar es Salaam au Moshi Mtaa wa Chini akiniadhimisha kwa mapenzi makubwa.
Turudi kwa Omari Mwariko.
Omari Mwariko alinipa muda wake na alipoona namdadisi sana kuhusu kazi zake pale pale akanikaribisha nyumbani kwake Njoro ili anioneshe baadhi ya vinyago alivyokuwa amechonga.
Nilifika nyumbani kwake na akanionyesha kazi zake na akachukua muda kunifungulia maktaba aliyohifadhi picha zake toka ujana wake alipoanza kuchonga.View attachment 1698508
Prince...Mzee habari...!
mimi naomba unifafanulie juu ya huyo muasisi mzalendo STEVE MHANDO japo nipate profile yake kwa uchache ama kwa urefu...nitafurahi sana kumfahamu mtu huyo
Tangawizi,Kwahiyo kupotea kwake ni tatizo la nani?
Old is GoldOMARI MWARIKO NANI ANAMFAHAMU?
Huyo hapo chini aliyevaa kofia ni Omari Mwariko.
Nimemfahamu Omari Mwariko nakua na nasoma shule ya msingi Moshi katika miaka ya 1960.
Miaka hiyo Omari Mwariko alikuwa mtu maarufu sana.
Omari Mwariko ni msanii bingwa katika kuchonga na kazi zake zimeonyeshwa hapa nchini, Uingereza na Marekani.
Lakini kwa miaka mingi akawa kapotea katika ulimwengu wa usanii akawa haonekani wala hasikiki.
Siku moja miaka 13 iliyopita niko Moshi ghafla nikakutananae barabarani.
Nikamsalimia na nikajitambulisha kwa kumtajia jina la ndugu yake Athmani Upepo.
Hili jina "Upepo," si jina lake ila alipachikwa kwa ajili ya uwezo wake wa kukimbia mbio kwa kasi kubwa.
Nakumbuka utotoni Moshi kila mtu alikuwa na lakabu yake.
Kulikuwa na Ali Maresi.
Hili jina "Maresi," alipewa kwa uhodari wake mpirani kuwa akitanguliziwa pasi mpira akadodoshewa kwa mbele na kuupokea mabeki hawampati na atafunga goli.
Kulikuwa na Athumani Makufuta.
Kisa cha jina hili ni kuwa tukisomeshwa somo la Hand Craft Majengo Middle School na Mwalimu anaitwa Fritz (sina hakika na "spelling").
Huu ulikuwa mwaka wa 1963.
Mwalimu Fritz alichukia sana mwanafunzi kuchora kisha akafuta.
Adhabu yake ni viboko papo kwa papo.
Athumani akafuta na akala mboko sote darasani tunashuhudia.
Athumani Mfinanga toka siku ile akawa Athumani Makufuta.
In Shaa Allah iko siku nitaandika kuhusu haya majina na kuwatafuta wahusika ili tucheke.
Nitaanza na "Toligogo" Omari Matola golikipa hodari amefariki miaka michache iliyopita.
Sote tulikuwa wanafunzi wa Mwalimu Juma darsa yake baina ya Maghrib na Isha Msikiti wa Ijumaa.
Jina hili ukimwita lilikuwa na staili yake maalum.
Unalitamka kama vile unaimba.
Rafiki yangu Allah amrehemu kila nilipokutananae iwe Dar es Salaam au Moshi Mtaa wa Chini akiniadhimisha kwa mapenzi makubwa.
Turudi kwa Omari Mwariko.
Omari Mwariko alinipa muda wake na alipoona namdadisi sana kuhusu kazi zake pale pale akanikaribisha nyumbani kwake Njoro ili anioneshe baadhi ya vinyago alivyokuwa amechonga.
Nilifika nyumbani kwake na akanionyesha kazi zake na akachukua muda kunifungulia maktaba aliyohifadhi picha zake toka ujana wake alipoanza kuchonga.View attachment 1698508
OMARI MWARIKO NANI ANAMFAHAMU?

Amezeeka lakini bado anaonekana mtundu mtuduOMARI MWARIKO NANI ANAMFAHAMU?

Wapuuze wanaosema ni uislam. Kama mtu umekulia kwenye mazingira ya Uislam bila shaka habari na kumbukumbu nyingi zitakuwa kwenye mazingira uliyokulia. Mimi umenifunua kitendawili kimoja. Wakati nikiwa mdogo kabisa napita Moshi mjini nilikuwa naona maandishi ''Mwariko's". Kutokana na udogo wangu sikuweza kujua kwa nini Mwariko's ni maarufu sana. Leo ndiyo nimejua kumbe alikuwa msanii. Asante na usikatishwe tamaa.Kolola,
Kila siku nawaandika Waislam kwa kuwa ndiyo jamii nilimozaliwa ndani yake na kukulia.
Hali hii ndiyo iliyotawala maisha yangu kuanzia utoto wangu hadi ukubwani.
Macho...Wapuuze wanaosema ni uislam. Kama mtu umekulia kwenye mazingira ya Uislam bila shaka habari na kumbukumbu nyingi zitakuwa kwenye mazingira uliyokulia. Mimi umenifunua kitendawili kimoja. Wakati nikiwa mdogo kabisa napita Moshi mjini nilikuwa naona maandishi ''Mwariko's". Kutokana na udogo wangu sikuweza kujua kwa nini Mwariko's ni maarufu sana. Leo ndiyo nimejua kumbe alikuwa msanii. Asante na usikatishwe tamaa.