Omar-Al-Bashir na tafsiri ya Demokrasia

Omar-Al-Bashir na tafsiri ya Demokrasia

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
520
Reaction score
2,932
Kuondolewa madarakani Omar al-Bashir kumezidi kuongeza maana ya Demokrasia na kutokea kwake.

Omar -Al-Bashir aliingia madarakani mwaka 1989 akiwa na cheo cha Jeneral ,akiondoa serikali iliyokuwepo wakati huo.

Kuondolewa kwa Bashir kumejawa na sababu lukuki kadhaa ni kupanda kwa Bei ya mkate(price of bread), kutokuwa na Uhuru (freedom),kutokuwa na amani,Haki(justice), rushwa,kitendo chake cha kutaka kubadili katiba na kukaa miaka mingi madarakani takribani miaka 30.

Kundi ambalo limekuwa mstari wa mbele ni kundi la wasichana (wanawake) 70% na vijana ambao kwa umri wamezaliwa wakati Bashir akiwa kiongozi ndani ya miaka 30 (1989-2019).

Sababu ya wanawake kuwa mstari wa mbele ni hasa kuchoshwa na sheria zinazowanyanyasa mfano, (Islamisation &Arabisation policies) kutungiwa sheria kandamizi kama Msichana wa miaka 10 kisheria anaruhusiwa kuolewa hii imepelekea kuwepo na ndoa za lazima na watu wazima (forced marriage) na kuondoa haki ya kupata elimu,adhabu viboko hadi 40 kwa mavazi ambayo sio mazuri(kuvaa suaruali) hasa kwa wanawake ,pia kuhalalisha ubakaji ktk ndoa(Marital rape,mfano kesi ya Nourah Hussein ) na kukamtwa kwa waandishi wa habari.

Sasa ukiangalia kwa jicho la kiongozi wa kidemokrasia ni wazi utajua kuwa Sudan hakukuwa na Demokrasia iliyokuwa inaliliwa na watu wake.

Neno,"Demokrasia kama mamlaka ya watu nchini sudani halikuwepo bali ni viongozi kuamua namna watakavyo sababu maamuzi yalikuwa ya wachache."

Hata Bashir aliwahi sema Sudan ni nchi ya kidemokrasia .

Ila Ricardo Blaugh katika kitabu chake cha #Outbreaks of Democracy# anasema kila mtu ana amini yeye ni Mwanademokrasia ,hata madikteta wana amini kuwa wanawakilisha matakwa ya wananchi na pia ni wanademokrasia ( Uk1 ).

Ricardo ana kata kusema Demokrasia ni mfumo uliopo katika serikali ,au mfumo unaotokea tokea ndani ya utawala au taasisi zake (institutional designing/form) anapinga hii ,yeye anasema Demokrasia hutokea pale ambapo Raia wanapoingia mgogoro na utawala wao ,ambapo katika mgogoro huo inapelekea watu na utawala wao kutathimini upya mahitaji yao ili kuondoa yale wasiyoyataka na hii hufanyika katika makubaliano ya pamoja hapo ndio hasa Demokrasia hutokea.

"Democracy mushrooms into a political spaces vacated upon the loss of order and is aided by crisis"

"In outbreak of democracy conflict works ,it some how generates cohesion"

"It causes people to re-evaluate their preference and needs ,it brings about consesus"

Hivyo walichofanya Sudan,dhidi ya Bashir wao wanaona hiyo ndio njia sahihi ya kuleta Demokrasia kama alivyosema Ricardo Blaugh ,hivyo wanasubiri serikali nyingine,hivyo wanategemea waliyoyapinga yatarekebishwa katika utawala ujao ili kuwepo na Demokrasia waitakayo

Ila bado kuna waandishi wengine na wasomi wana kinzana na Ricardo Blaugh ,Kama Anthony Downs,Robert Dahl,Schumpter , Huntington,Schmitter hawa wanasema uwepo wa Demokrasia ni proces na hutokea katika mfumo wa utawala.(institutional designing/form.

Swali, Je, Demokrasia hiyo wataipata ?

Shukrani.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa uelekeo uliopo Sudani inaonekana kitakachofanyika ni kuweka MVINYO WA ZAMANI KWENYE CHUPA MPYA.
They might not achieve what they longed for!
 
Back
Top Bottom