"Sijajua tunataka wabunge wa aina gani - nilisifia hizi kanuni mpya za Chama Cha Mapinduzi CCM upande mmoja kuwa imeongeza watu wengi kupiga kura na kupunguza rushwa ila nikaonesha hatari ya utaratibu wa kurudisha majina matatu kwamba italeta shida sana kwa wale wabunge wanaosimamia haki za jamii na kusema itatuletea wabunge waoga zaidi kwa kuwa wanajua kuna kukatwa (kuenguliwa kwenye mchakato)
Soma pia: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Mimi nilidhani kila anayeomba ubunge angepigiwa kura ndani ya chama ndio uteuzi ufuate badaye ili kuwapa nafasi wanachama wa CCM wachague mtu wanayemtaka. Naamini kabisa wana CCM mfumo huu mpya wa kurudisha majina matatu inaweza leta mpasuko mkubwa sana ndani ya CCM kama usipoangaliwa upya
Baada ya uchaguzi huu nashauri CCM wafanye mapitio ya kanuni hizi mpya za uchaguzi ili kutoa zaidi demokrasia ndani ya chama. Malalamiko ya watu kukatwa kwa ngazi ya Wilaya ni mengi - pamoja na kwamba wilaya sio hatua ya mwisho lakini ina sehemu kubwa kushawishi uamuzi na pia kumbuka hawa ndio watasimamamia pia uchaguzi na ndio watakuwa muda wote na wagombea
Kwahiyo hata mtu waliyempendekeza tofauti akirudishwa sijui watashirikiana naye vipi. Kukatwa Wilayani inawezekana kabisa na badaye kurudishwa, hata mimi wakati nagombea uenyekiti UVCCM Ngorongoro nikiwa chuo mwaka 2008 walikata jina Wilaya na kurudishwa huku juu badaye. Ni matumaini kuwa haki itatendeka katika hatua zinazofuata na watu kama kina Mpina wakarudishwa."-Wakili Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania
Chanzo: Jambo Tv